Electro College kwenye uchaguzi wa USA ni nini?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,335
Naomba kufahamishwa hilo na pia faida zake ni zipi
Je Nchi yetu inaweza kutumia Electro collage votes?
 
Ni kura 3 au zaidi kutoka kila jimbo nchini marekani ambayo huleta jumla ya wapiga kura 538 ambao huchagua rais na makamu wake lakini uchaguzi wa makamu wa rais zaidi hutokana na kura za senate.

Na wapiga kura hawa wa electro college idadi yao ni sawa na masenate na huteuliwa na vyama vyao kutoka majimbo ya marekani.

Na kura hii hupigwa jumatatu ya kwanza baada ya jumatano ya kwanza ya mwezi desemba baada ya uchaguzi.

Baadae popular vote ndio huamua mshindi kwani ndio sum of all vote.
 
Kwanza kabisa, hakuna kitu kinachoitwa "Electro College" wala "Electro Collage" katika uchaguzi wa Marekani!

Kilichopo ni kitu kingine kabisa kinachoitwa ELECTORAL COLLEGE.

Bila shaka hicho ndicho ulichotaka kukifahamu!

Electoral College ni bodi ya wapiga kura ambayo huwakilisha majimbo yote ya uchaguzi katika kupiga kura ya Rais pamoja na Makamu wa Rais.

Wajumbe wa Electoral College huteuliwa kutoka katika kila jimbo ili kuwakilisha majimbo hayo katika uchaguzi.

Bodi inakuwa na jumla ya wajumbe 538 ambao ndio idadi kamili ya kura zote za uchaguzi ambapo kura 270 au zaidi huamua mshindi katika uchaguzi.

Kwa mujibu wa katiba, kila jimbo lina mamlaka ya kuamua jinsi ambavyo wateule hao (electors) wanachaguliwa ambapo idadi yao katika kila jimbo huendana na idadi ya wajumbe katika bunge la Senate na Baraza la Wawakilishi (The House).

Maana yake ni kuwa, idadi kamili ya wajumbe wote ni sawa na idadi ya wajumbe katika Senate pamoja na Baraza la Wawakilishi lakini pia wajumbe wengine watatu (3) kutoka jiji la kiserikali la Washington D.C. kulingana na katiba ya Marekani.

Hivyo, idadi ya wajumbe wa Senate wapatao 100 hivi sasa pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wapatao 435 ambazo ndizo nafasi za uwakilishi katika majimbo sambamba na wajumbe watatu (3) kutoka Washington D.C. hupelekea idadi ya wajumbe kuwa 538 ambao ndio hupiga kura ya Rais pamoja na Makamu wa Rais, kura inayofahamika kama electoral vote.
 
Huh...what??

Kwanza wala haiitwi ‘electro college’.

🤣
 
Pia mazani kuna majimbo yana kura nyingi kuliko mengine nazani wanaangali Uchumi, Jimbo la California ndo lina kura nyingi lama sikosei, likifuatiwa na wakina Texas na wakina New York,

Uteuzi huwa unaangalia vigezo vipi?
 
Utaratibu wa kupiga kura kuwapata hao 'wajumbe' ukoje? Maana kila jimbo linakuwa na vyama zaidi ya kimoja mfano Democrat na Republican, na wananchi wa vyama tofauti?
 
Back
Top Bottom