Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,695
- 1,696
Makamda na Wakuu wa JF;
Nyeti zilizofika katika dawati la Superman zinasema wale TRIANGLE TRIPPLETS aka PEMBETATU PACHA aka RACHEL inasemekana wakekataa kujibu barua walizopewa hivi karibuni zikiwataka wajieleze kwa nini wasifukuzwe uongozi na uanaachama wa Chama Cha Magamba CCM.
Nyeti zinasema kuwa EL amesema mwenye ushahidi dhidi yake na mwenye ushahidi wa nani anapaswa kuondoka CCM kwa ufisadi aje nao na hivyo wote wamekataa katu katu kusema wala kujibu kitu.
Inasemekana kuwa ni kweli RACHEL wamekuwa na vikao vyao vya siri na mpaka sasa wamekutana mara mbili tangu watoke Dodoma kwenye vikao vya CC na NEC.
Nyeti zinasema kuwa mara baada ya Vikao vya CC. Mkuu wa Kaya alimwita EL kule Ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma majira ya saa nane usiku na akamuuliza kuwa imekuwaje Makamu Mwenyekigoda wa Chama Cha Magamba Mh. PM akakutaja na wewe waziwazi kuwa ni FISADI na je tutafanikiwa mikakati yetu tuliyopanga huko nyuma? (NB: Hii ni Mikakati ya Boyz II Men ya EL kuwa Next pale Magogoni). Hata hivyo EL alimjibu Mkuu wa Kaya kuwa bado anatafakari kilichotokea ndani ya CC na kumwambia JK ampe muda na atarudi na jibu.
Inasemekana EL alikaa kama nusu saa na kisha akaondoka. Desk la Superman limehabarishwa kuwa EL alikwisha jua mpango wa JK wa kumtosa kwa kumzungunguka pasipo kuharibu urafiki wao. Hata hivyo hadi leo hii JK bado hajapewa jibu.
Pamoja na yote hayo RACHEL wamechukizwa zaidi na maneno ya Dogo Nape na Kada Chiligati na Mukama ambao wanaaendelea kuwapa siku 90 wajitoe au watoswe kwa kuwa eti wao ni MAFISADI.
Naye Mu-Iran RA inamesemakana kama anataka bora Jahazi sasa liingie maji na wote wazame. Yaani kama noma na iwe noma.
Kuna mengi sana yatakuja baada ya mapumziko ya Pasaka from 28th May 2011 ambacho kitakuwa na Mishindo Mkuu.
Update 1: Easter Sunday - 24th April 2011
Rais JK, leo akiongea katika Tamasha la Muziki wa Injili uliohusisha vikundi vya kwaya toka nchi mbalimbali alisema:
"Katika kushughulikia swala la mafisadi, haki itatendeka na hawatamuonea haya mtu yeyote"
Source: ITV News Bulletin of 8.00 PM
Update 2: Monday 25th April 2011:
RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu. Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.
Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu. Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.
Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu. "Ujasiri wa Rais wetu ni ujasiri aliopewa na Mwenyezi Mungu pamoja na dua tunazomwombea, tunaomba kujivua gamba huko kuwe kwa ukweli na kusiishie hapo tu," alisema Askofu Ndegi.
Baada ya kumaliza kusema hayo, Askofu huyo aliomba maaskofu wengine waliokuwepo ukumbini kumwekea mikono Rais sehemu waliko na kumwombea dua ya kumpa ulinzi, ujasiri na hekina katika uongozi wake.
Lakini Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini na kuwataka wananchi kuvumiliana baina ya watu wa dini mbalimbali na kutowasikiliza watu wanaohubiri habari za udini kwa lengo la kutaka kuleta mafarakano nchini. Tamasha hilo ambalo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, lililenga kuchangisha fedha za kusaidia yatima, watu wenye ulemavu na mahitaji kwa wanawake wasiojiweza.
Source: HabariLeo
Peace and Love
Respect.
Superman.
QED