EL marudio ya mazungumzo yake na waandishi Monduli kurusha TBC1 saa 3 Usiku wa leo.

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Kukosekana kwa gamba lolote kuchangia aliyoyasema E Lkukosoa au kuunga mkono kunatoa picha gani?
 
TBC1 wametangaza kuwa leo saa 3 usiku watarusha kipindi maalumu kuonesha kilichojiri katika mkutano wa EL na waandishi wa habari siku ya Jtano huko Monduli.

Katika tangazo lao, EL ameoneshwa akirudia kusema kuwa yeye na JK hawakukutana barabarani!!

Update...Nimemwona na kumsikia akiongea haya hapa (summary)....Najua si mapya but ..naweka tu for those who may be interested!!

  1. Kumhujumu JK…hawezi kumhujumu, hawakukutana barabarani….ni uongo unaotakiwa kupuuzwa
  2. Kuwachochea vijana…..hakuwachochea kwa sababu hakuwa nchini. Alikuwa Germany kwa ajili ya matibabu. Vijana always ni radical…tusiwajukumu. Tuzungumze nao. Ni taasisi muhimu kwa chama chochote cha siasa. Sikufahamu, sikupanga wala sikukuhusika.
  3. Sasa imetosha..Hataendelea kuvumilia kuchafuliwa. Atachukua hatua kwa magazeti yaliyomchafua. Kuanzia sasa, no more. Imetosha
  4. Ombi..vyombo vya habari visaidie nchi. Tuache kuandika watu kwa sababu ni hatari
  5. Uchumi wa dunia uko taabani…ametaja nchi nyingi zenye matatizo. Viongozi na vyombo vya habari wamehagaika kutafuta suluhu. Tz kuna matatizo mengi, ya uchumi wan chi yetu…Tshs inaporomoka sana, bei ya vyakula inapanda sana, inflation imepanda pia (14 to 16%)…hali ya maisha itakuwa mbaya sana. Pia kuna tatizo la ajira kwa vijana (it is a time bomb)!
Maswali
  1. Ajira kwa vijana: Mjadala mrefu na mpana unatakiwa, eg. Private sector involvement! Serikali ijenge viwanda…kwa kukopa. Pesa zipo.
  2. Mustakabali wa CCM: Hana wasi wasi, chama kitavuka salama, chini ya uongozi wa busara wa JK
  3. Kila jambo kuhusishwa na urais 2015: Hata yeye anashangaa sana..Waandishi waache kuandika chokochoko
  4. Sitta na Richmond kuhusu wale waliojiuzulu kulipa deni: Suala la Richmond, Dowans na kujivua gamba atatoa majibu baadaye!!
My observations:
  1. EL ameonekana mwenye wasi wasi sana…his mouth was dry all the time, indicating that he was very stressed!
  2. Kuna simu karibu na vipaza sauti, imeita karibia mara 4…Na kuna sms kadhaa zimesikika zikiingia kwenye simu ambayo ilikuwa karibu naye!
 
Bado sijaelewa umuhimu wa kauli ya Lowasa kuwa yeye na Kikwete hawakukutana barabarani!. Who cares if they met in a football pitch or in Savile Row? One thing is for sure, their meeting has now become a 'weapon of mass destruction' for this country.
 
It is minutes past am only seeing models with dresses for kitchen party dresses.
It has started thanks....eti ukimya ni busara aliyoipata kutoka kwa Mungu...Crap he is talking nonsense. Eti kunakufinyana na kuonyana ndani ya chama wandugu nahama it is nauseatic.
 
Namtazama Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa katika TBC 1 kipindi cha marejeo alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibu.

Kwa mtazamo wa haraka ni kama mtu aliyepoteza bashasha na mvuto....sura yake ni kama anasumbuliwa na tatizo fulani la kiafya kama si kisaikolojia.. Japo si vizuri kumtabiria mwenzio mabaya, lakini kwa mwonekano wa haiba yake, sijui kama inawezwekana akaweza kusimama kidete kuwania kiti cha Urais mwaka, 2015 kama wengi wanavyotabiri.



-----------------

Tuesday, 18 October 2011 21:38
0digg
lowassa-top.jpg
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa​
MILLYA ACHAFUA HALI YA HEWA CCM, ASEMA MAISHA YAKE YAKO HATARINI
Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa leo anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari katika mkutano ambao utazungumzia mambo makuu matatu likiwamo suala la Kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambalo lilisababisha ajiuzulu wadhifa huo, Februari 2007. Mkutano huo wa Lowassa unafanyika siku moja tangu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Millya atoe matamshi makali akiwatuhumu aliowaita watoto wa vigogo kwamba wanavuruga umoja huo huku akilalamika kwamba: "Maisha yake yapo hatarini." Habari zilizopatikana jana kupitia kwa watu walio karibu na Lowassa zinasema, katika mkutano huo, Mbunge huyo wa Monduli (CCM), pia atazungumzia taarifa zinazomhusu ambazo zimekuwa zikichapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Suala jingine ambalo linatarajiwa kuzungumzwa na kiongozi huyo ni kuhusu mgogoro ndani ya CCM mkoani Arusha, ambao unatokana na mgawanyiko miongoni mwa makada na viongozi wa chama hicho. "Pia anasema kwamba ataanzia pale alipoishia, siku ile alipozungumza bungeni kuhusu Serikali kufanya uamuzi mgumu lakini hakutakuwa na kumshambulia mtu," alisema mmoja wa watu hao na kuongeza:

"Anasema (Lowassa) kwamba lazima aweke kumbukumbu sahihi kwa baadhi ya mambo ambayo yametamkwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na viongozi wengine kwani amebaini kuwa uongo ukisemwa sana na kwa muda mrefu hugeuka kuwa ukweli."
Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuitisha mkutano wa vyombo vya habari tangu alipojiuzulu kuzungumzia sakata la Richmond ambalo halikuwahi kupata hitimisho la kisiasa wala kisheria.

Lowassa pamoja na mawaziri wawili waliowahi kuwa na dhamana katika Wizara ya Nishati na Madini kwa vipindi tofauti, Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha walijiuzulu nyadhifa zao kwa kuwajibika, baada ya matokeo ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge la Tisa, iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Ujenzi.

Uchunguzi huo ulihusu kampuni tata ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, ambayo ilishindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba baina yake na Tanesco, hivyo kuhamishia majukumu yake kwa kampuni Dowans.

Mkutano wa Millya
Mkutano wa Lowassa unafanyika katika kipindi ambacho CCM kinakabiliwa na misukosuko ambayo imedhihirisha kuwapo kwa mpasuko mkubwa huku kukiwa na tofauti za wazi miongoni mwa makada na viongozi wake ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakirushiana maneno nje ya vikao rasmi vya chama.
Jana, Millya naye aliingia katika malumbano hayo pale alipowaambia waandishi wa habari kwamba: "Watoto wa viongozi wa CCM na Serikali wamejitwika madaraka ya wazazi wao kinyume cha sheria za nchi."

"Ninaomba kuwaonya watoto wa vigogo wenye tabia ya kuingilia mambo ya UVCCM na uendeshaji wa nchi kwamba hatutaruhusu na hatutavumilia watumie mamlaka tuliyowapa wazazi wao ili kutuvurugia jumuiya yetu," alisema Millya na kuongeza:

"Haki hufuatana na wajibu lakini amani huletwa na haki. Niwaombe viongozi wetu wasikubali kutumia mamlaka kunyima watu haki zao kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha amani na utulivu wa muda mrefu wa nchi yetu." Millya alitoa kauli hizo akitokea polisi kuhojiwa kutokana na matamshi yake ya Oktoba 10, mwaka huu katika mkutano wa hadhara kwamba polisi walizuia maandamano ya UVCCM kutekeleza shinikizo la mtoto wa kigogo mmoja.
Akizungumzia kuhojiwa huko, Millya alisema: "Ni muhimu sana mfahamu kwamba sijayumba na sitayumba kwani tuna safari ndefu ya kujenga demokrasia ya kweli na Uhuru wa kweli wa mawazo na maoni."

"Uhuru wa utashi wa kisiasa, Uhuru wa kusimamia misingi na kanuni za chama chetu, jumuiya yetu (UVCCM) bila woga, wala kuyumbishwa na mtu yeyote hata akijaribu kutumia vyombo vya dola au taasisi binafsi ili nitoke kwenye hoja ya msingi ya kuhakikisha Tanzania huru inawezekana."
Alisema mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini wanahujumiwa na kikundi kidogo cha watu wenye uchu wa madaraka na wenye lengo la kulinda maslahi yao binafsi ya sasa na ya baadaye.

Alitoa mfano wa tamko lililotolewa na Baraza la UVCCM Mkoa wa Pwani kwamba Rais wa 2015, kamwe hawezi kutokea Kanda ya Kaskazini kuwa ni uthibitisho kwamba vijana hao walitumiwa.

"Mbali na kwamba hili ni tusi kwa watu wa kaskazini wenye haki yao kikatiba kuwania nafasi ya uongozi wa juu wa nchi yetu, ni tusi pia kwa wapiga kura wa Tanzania wanaoamini katika demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa," alisema.
Alisema cha kushangaza mpake leo hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimewahi kutoa tamko la kukanusha taarifa hiyo iliyounganishwa na taasisi moja ya juu serikalini.

Millya alisema kwa hali falsafa ya kujivua gamba yenye waasisi wake, ni mbinu madhubuti na endelevu za kuwapunguza nguvu baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM ili kuwazuia kugombea urais 2015.Alidai kuwa hivi sasa maisha yake yapo hatarini kutokana na kutumiwa ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi na kwamba ametoa taarifa polisi kuhusu suala hilo.

Kama walivyofanya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangoro na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa, Millya naye alimtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwamba ndiye chanzo cha mitafaruku yote ndani ya CCM.

Hata hivyo, Nape alipoulizwa kwa simu Jumamosi iliyopita kuhusu shutuma nyingi kuelekezwa kwake alisema: "Sijui kwa nini haya mageuzi ya kujivua gamba yanapotajwa yanahusishwa na urais, hili si sahihi hata kidogo." Nape alikuwa akijibu tuhuma Ole Nangoro ambaye alimshambulia hadharani, akikosoa utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba inayosimamiwa na Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

Kujivua gamba Falsafa ya kujivua gamba ni moja ya maazimio 24 yaliyopitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ikiwataka watuhumiwa wa ufisadi kupima kisha kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Rostam Aziz alishajivua nyadhifa zake ambazo ni ujumbe wa NEC na ubunge wa Igunga ambalo CCM ilifanikiwa kulirejesha kupitia kwa Dk Dalaly Kafumu katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema taarifa ya utekelezaji wa maazimio 24 ya NEC likiwamo la kujivua gamba, inaandaliwa ili iwasilishwe kwenye kikao cha NEC ambacho kinaweza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi ujao, kikitanguliwa na Kamati Kuu (CC). Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dar na Peter Saramba, Arusha
 
Huwa najiuliza pasipo kupata jibu hivi huyu kapteni mstaafu wa JWTZ Bw Edward Ngoyai Lowassa ni nani? kwanini haachi kutajwa midomoni mwa watu? yaani akizungumza neno moja linageuka mjadala wa nchi nzima, ana nini huyu Lowassa? au tuseme yeye ni Jacob Zuma wa Tanzania? kwamba eti licha ya kashfa zote hizi bado urais unamngoja? SIELEWI SIELEWI KABISA!
 
Kukosekana kwa gamba lolote kuchangia aliyoyasema E Lkukosoa au kuunga mkono kunatoa picha gani?

MAZUNGUMZO YOYOTE YA lOWASSA BILA KUZUNGUMZIA KUJIVUA GAMBA AUDHANA YA KUJIVUA GAMBA ,RICHMUND,DOWANS NI USANII NA UPUUZI MTUPU.MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI HAKUNA JIPYA.BLAHABLAH.MUNGU INUSURU TANZANIA KUTOKA KWA MAFISADI.HAPA EBU NGOJA TUKUSAIDIE,KATIKA UFUNGUZI WA WAKO KATIKA MAZUNGUMZONA WAANDISHI WA HABARI UNGELIANZA NA KAULI IFUATAYO"Mimi na mh.Rais hatukukutana mitaani tunajuana kwa kina na mapana kama mimi fisadi basi na Rais JK ni fisadi kama mimi na swala la Richmund na Dowans liko nje ya uwezo wangu aneweza kulitolea ufafanunuzi ni Mh.Rais JK, hivyo hukumu yangu kama fisadi pia ni hukumu stahiki kwa Mh.Rais JK.Tuhukumuni sote sawa"
 
EL amekosea kimsingi!Namna pekee ya kufunga midomo wachafuzi wake kama anavyodai ilikuwa ni kuwaeleza kile anachokijua kuhusu RICHMOND,DOWANS na mengine yanayofanana na hayo maana hayo ndio agenda za wachafuzi wake.Anapokwepa kuzungumzia hayo na huku akitaka kufunga watu midomo ni kazi bure!Watu hawatamwacha EL hadi pale atakapozungumzia hayo madubwasha na kweli wa TZ wamuelewe.
 
Back
Top Bottom