Eike Batista: Tajiri number 7 Duniani aliyefilisika na kubaki 0

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
234
218
Eike Batista ni tajiri wa kibrazili na ambaye alikuwa mtu tajiri kuliko wote nchini Brazil na number 7 kwa utajiri Duniani. Alimiliki Dollar Billion 35, ila sasa anadaiwa Dollar billion 1.4. Polisi wamekamata magari yake yote ya thamani.

Binafsi anasema kufilisika kwake ni kwa sababu alipeleka biashara zake kwenye soko la hisa. Wachambuzi wa mambo wanadai alifilisika kwa sababu ya anguko la bei za bidhaa zake..
 
Once Kuna mtu aliniambia UTAJIRI unakwisha lakini UMASKINI hauishi ni kwamba ni rahisi sana kuvuka kutoka kwenye UTAJIRI na kwenda moja kwa moja kwenye UMASKINI lakini ni vigumu sana kutoka kwenye UMASKINI na kuangukia kwenye UTAJIRI utaambiwa kuna hili na lile
 
Tembo hata akonde vp hawezi kua Kama sungura , hata hivyo maadam kilichoisha Ni Mali Tena kutokana na ushindani huku Akili yake ikiwa Timamu , Tegemea kurudia utajiri Muda wowote.
 
Utajiri unaisha Sana pale Mtu anapokesea masharti alopewa na mganga wake , Chanel za pesa yake akizikosea ,muda na hitaji la business ukiisha bila yeye kufanya ubunifu kuenda na muda husika
 
Kivipi mkuu. Hebu fafanua tafadhali.
Hivi mkuu.., mtu mwenye deni la 1.4bn dollar akaomba deni hilo aliongeze japo kwa 5% ili aje alipe zote baadae maana yake atakuwa amejipatia shs. 140 bn za kitanzania. hivi akizungusha hizo kwa muda wa miaka kadhaa si atakuwa zaidi ya huyo mwenye 100bn? by that time hao wanaomdai hiyo 1.4bn $ watakuwa wamesha right off hilo deni maana hata kumtaifishia vipesa alivyonavyo kwao watakuwa wanaona ni kama pesa ya dagaa tu. huwezi ukawa unamdai muuza karanga million 100 halafu ukamnyang'anya sinia la karanga ili kupunguza deni.
 
Maji hufuata mkondo,.. penye utajiri unaingia utajiri. Atapata tena .. money is an idea
 
Maisha ni kupanda na kushuka.

Kufilisika kupo.

Unaweza kuwa na mipango, mikakati, kichwa, utulivu, makini, kutokuwa na matumizi ya ulazima nk.

Na bado ukafilisika
 
Sasa umesema utajiri wake ni 35bn USD na benk anadaiwa 1.4bn dollar itakuwaje afilisike kwa deni dogo km hilo?
 
Amefilisika kwa muda gani?
Na wakati anaanza kufilisika hakuna watu wali mshauli abadilishe mfumo wa biashara
Na kwanini amefirisika kizembe namna hiyo?
Hizo pesa ni nyingi sana
 
Back
Top Bottom