Eid-Mubarak

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,817
eid_mubarak-761530.jpg

Eid-Mubarak

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar,

Laa ilaaha illallahu Wallahu Akbar, Kabira Allahu Akbar, Wa lillahil Hamd

Wishing you and your family a Happy and peaceful Iydul- Adhwhaa!!!

May Allah accept your good deeds.
Forgive our transgressions and ease the suffering of all people around the Globe...

Eid Mubarak!!!
 
Tunamuomba Allah azikubali amali zetu, azikubali funga zetu, azikubali sala zetu, atuzidishie imani na mapenzi ya dini yetu, atusamehe makosa yetu tuyajuwayo na tusiyoyajuwa.

Tunamuomba Allah awape nusra waislam popote duniani, awape nusra waislam wadhaliliwao, wadhulimiwao na wateswao. awape wao ushindi na sisi kwa jumla.Ushindi utakaowatia watu katika dini yake makundi kwa makundi.

Tunamuomba Allah atuunganishe na sio tutengane, atupe mapenzi baina yetu na sio tuchukiane na atuepushe, atuepushe na unafiki na wanafiki pia.

Yaa Rabb tia kwenye nyoyo zetu imani iliyo ya kweli ifanane na vitendo vyetu na iyowane na fikra zetu.

Yaa Rabb twakuomba utuongoze katika njia iliyonyooka, njia ya wale uliyowaneemesha na sio ya wale uliyowaghadhibikia au ya waliyopotea.

Tunakuomba Yaa Rabb utujaaliye uwezo wa kufanya uliyotuamrisha na kuyawacha uliyotukataza, tujaaliye tuwe ni wenye kuamrishana mema na kukatazana mabaya.

Twakuomba Yaa Rabb uviongoe vizazi vyetu, uzipambe nyoyo zao kwa imani na namapenzi ya dini ya Kiislam, uwape ujuzi wa kupambanua baina ya haki na batil na uwaondoshee khofu dhidi ya maadui wa Uislam.

Yaa Allah wasemeh na warehemu wazazi wetu waliyo hai na waliyotushatutangulia.

Yaa Allah tukubalie dua zetu...AMIN

TUNAWATAKIA KILA LA KHERI

EID MUBAARAK
 
BAKWATA badilikeni dhima ya waislam wote Tz iko mikononi mwenu. Kote duniani watu wameswali Idd kwa kuungana na wenzao walioko Makkah ktk hijja halafu nyie bakwata mnawatangazia waislam wa Tanzania kuwa kesho ndio Idd kwa kuungana na akina nani? Hao watu wa bakwata walioenda hija nao hawajaswali na wenzao leo huko makkah wanasubiri kesho?. Kimantiki haileti maana yoyote. Idd hii ni ya mahujaji iweje nyie msiungane na waliko hija? Kijiografia pia inakataa Tanzania na Saudi Arabia hazipishani hata sekunde moja ktk hesabu ya wakati,iweje tupishane siku nzima ktk kuswali idd? Ni mambo ya wazi sana ambayo Bakwata haitaki kuufahamisha umma wa watz. Hata nyie watanzania pia ninyi badilikeni akili za kuambiwa na bakwata changanyeni na zenu mtajikuta mnaswali idd pamoja na waislam wote duniani.
 
Kesho ni siku ambayo tunaungana na waumini wa dini ya kiislamu:peace: kusherekea sikukuu ya idd el haji :pray2:
Nawatakieni Idd njema Watanzania na wanachama wote wa JF
:amen:
 
BAKWATA badilikeni dhima ya waislam wote Tz iko mikononi mwenu. Kote duniani watu wameswali Idd kwa kuungana na wenzao walioko Makkah ktk hijja halafu nyie bakwata mnawatangazia waislam wa Tanzania kuwa kesho ndio Idd kwa kuungana na akina nani? Hao watu wa bakwata walioenda hija nao hawajaswali na wenzao leo huko makkah wanasubiri kesho?. Kimantiki haileti maana yoyote. Idd hii ni ya mahujaji iweje nyie msiungane na waliko hija? Kijiografia pia inakataa Tanzania na Saudi Arabia hazipishani hata sekunde moja ktk hesabu ya wakati,iweje tupishane siku nzima ktk kuswali idd? Ni mambo ya wazi sana ambayo Bakwata haitaki kuufahamisha umma wa watz. Hata nyie watanzania pia ninyi badilikeni akili za kuambiwa na bakwata changanyeni na zenu mtajikuta mnaswali idd pamoja na waislam wote duniani.
Ni kweli kwa mujibu wa hapa inaonyesha sikukuu ni leo
Muslim holidays - Wikipedia, the free encyclopedia
lakini hapa inaonyesha sikukuu ni kesho
Eid al-Adha - Wikipedia, the free encyclopedia
hii sikukuu wanaiita Eid al Adha(idd el haji)
ila kuna mahesabu wanafanya jinsi ya kuwa sikukuu itakuwa lini
http://en.wikipedia.org/wiki/Islamic_calendar
nenda chini ktk convert Hijri to Gregorian year or Gregorian to Hijri year
Gregorian ni kama leo 16 novemba 2010,Hijri ni calender ya kiislam eg leo mwezi Dhū 'l-Hijja 1431 mwezi wa mwisho hadi tarehe 07 desemba 2010 ndio mwaka mpya wa kiislam 1432,kuna hesabu wanafanya eg zimebaki siku ngapi kumaliza mwaka wanaupeleka ktk Hijri calender inakuwa inaendana au makadirio na siku fulani,sasa ndio inagongana ikifutwa ya Saudi Arabia inaonyesha sikukuu ni leo leo kimakadirio ya karibu hapo sasa mahesabu na dunia inaangaliwa sehemu kubwa eg zimetofautiana saa/siku wanaamua wengi wape au mwenye sauti inaamuliwa na wengi sikukuu kesho,kwahiyo tusiwalaumu sana BAKWATA japo sawa una point Saudi Arabia tupo nao sawa,ni sawa mahesabu ya makadirio ukiwa ktk nchi zilizoendelea au hata ktk malls eg Mlimani City nikitolea mfano nchi yetu mkate labda natolea mfano ni USD 0.99 kwenye pale point of sale labda ktk nchi hiyo senti moja haitumiki atakadiria bei ni USD 0.95 ili akurudishie change senti 5 kama ulitoa USD 1,au nchi zingine/sehemu zingine/maduka mengine yeye atakukadiria ni USD 1 change hairudi,kwahiyo ndio kama mabo haya yanapotokea hivyo usilaumu sana haiwezi kuenda sawa kabisa nikiazima kamusi wanasema exactly.
 
BAKWATA badilikeni dhima ya waislam wote Tz iko mikononi mwenu. Kote duniani watu wameswali Idd kwa kuungana na wenzao walioko Makkah ktk hijja halafu nyie bakwata mnawatangazia waislam wa Tanzania kuwa kesho ndio Idd kwa kuungana na akina nani? Hao watu wa bakwata walioenda hija nao hawajaswali na wenzao leo huko makkah wanasubiri kesho?. Kimantiki haileti maana yoyote. Idd hii ni ya mahujaji iweje nyie msiungane na waliko hija? Kijiografia pia inakataa Tanzania na Saudi Arabia hazipishani hata sekunde moja ktk hesabu ya wakati,iweje tupishane siku nzima ktk kuswali idd? Ni mambo ya wazi sana ambayo Bakwata haitaki kuufahamisha umma wa watz. Hata nyie watanzania pia ninyi badilikeni akili za kuambiwa na bakwata changanyeni na zenu mtajikuta mnaswali idd pamoja na waislam wote duniani.

daaah sie tusha swali leo wakuu!
 
Mufti Xpaster........... nalfaidhina ...........Eid Mubarak to you too !! Mola akujalieni yote mliomwomba..........
 
Back
Top Bottom