Egypt planning war on Uganda

ByaseL

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
2,225
1,225
Uganda Observer

A Ugandan diplomat has warned that Egypt may be planning to attack Uganda.
Uganda’s High Commissioner to Tanzania, Ibrahim Mukiibi, told fellow ambassadors during a closed-door retreat at Serena Lake Victoria Resort on Saturday, that Egypt might wage war against Uganda and other regional governments in a bid to control the River Nile waters.
Mukiibi, a former ambassador to Egypt, added that the North African country is also inspired by the need to stop Southern Sudan from breaking away from the Sudan.

“Egypt is planning to build nuclear energy and we are threatened by their efforts to engage in war. We should tell the US about this because these people are planning a war with Uganda,” Mukiibi said.

Mukiibi also rallied ambassadors to consider the protection of the Nile waters and the January referendum in Sudan as significant security challenges facing Uganda.

“We must know that Egypt is against this referendum. And as a man of experience, I must tell you that all members of the Arab League are behind Egypt. So, we must watch out,” he added.
On learning that this reporter was in attendance, Foreign Affairs minister Sam Kutesa asked Mukiibi to stop his submission and ordered the reporter out of the conference, arguing that the meeting was intended to be closed to the press.

However, Mukiibi’s remarks have come shortly after a meeting between President Museveni and the Egyptian delegation on December 6 where the Nile water issue was discussed extensively by the two governments.

During the meeting, Museveni told the Cairo delegation led by Egypt’s electricity and energy minister, Dr Hassan Younis, that there will be no political problem with the sharing of the River Nile waters.
In May this year (May 19, 2010) we reported in a story States stockpile arms as row over Nile waters rages, that two senior Egyptian government officials – the minister of Legal and Parliamentary Affairs, Moufid Shehab, and the minister of Water Resources and Irrigation, Mohammed Allam – had urged their country to do anything –including going to war – to safeguard what they call their country’s historic right to the largest share of the Nile waters.
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Hilo wala sitolishangaa, kwani wakati Uganda hawaelewani na Sudan Egypt iliwapa waganda vifaru ili waishambulie Sudan. Jiulize mkataba ulikuwa ni nini? hali ile ilisababisha maafa makubwa kusini mwa Sudan na kaskazini mwa Uganda na kupelekea mkataba wa amani. (ushirikiano wa kuipiga Sudan ulihusisha pia Ethiopia na Elitrea - kwa wafuatiliaji wa mambo wanakumbuka kilichotokea ni kipi) Kama hoja kweli ni maji ya Nile kwanini wasianze na EL ambaye alitamka wazi maji tutayatumia wala hakuna cha Egypt wala nani.. KWELI HERI MKOLONI MZUNGU KULIKO MWAFRIKA (HATA MU-EGYPT NI MWAFRIKA) Tabia zile zile... aaarg
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
KWELI HERI MKOLONI MZUNGU KULIKO MWAFRIKA (HATA MU-EGYPT NI MWAFRIKA) Tabia zile zile...
This is a widely held notion and it has exposed thick brains africans possess! Oh Lord The Almighty, emancipate these minds free!
 

Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Kazi kwenu waganda msipokaa chonjoo mtapigika lakini hiyo ni vita rahisi sana na hatathubutu. Kifo chao ni kufunga maji???
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
10,467
2,000
Bila hata ya kufikiria kupigana na hao Jamaa hebu tujiulize, tuna mito mingapi ambayo inaweza kutupatia maji ya kututosha?
Kama tunayo ya kutosha; basi tuna haja gani kukoromeana na Misri ambao tegemeo lao ni huo mto Nile pekee?
nadhani kimantiki tunaweza kuwa hatuwatendei haki hawa watu, ila wakitishia kutupiga watakuwa wamekosea..
Manake wakijaribu tu hata kutupa jiwe, naingia jeshini kuitetea nchi yangu aisee...

Akikupiga ngumi ya jicho, wewe mpige ya sikio....
 

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Kuna haja ya kuelewa nini kinaendelea kwani mikataba ambayo Waingereza walisaini na Misri pamoja na Sudan mwaka 1929 na 1959 ndiyo ambayo inadai kutoa upendeleo kwa Misri. Sisi Tanzania tuliikataa mikataba hiyo mwaka 1962 kwani katika kile kinachotambulika kama Kanuni ya Nyerere ya Urithi wa Taifa (Nyerere Doctrine on State Succession) ni kwamba taifa huru halibanwi na mikataba iliyosainiwa na Mkoloni kwa niaba yake bali kama linachagua kuitambua mikataba hiyo. Kwa hiyo Tanganyika tulipopata uhuru tulikataa kuitambua mikataba mingi ukiwemo ule ambao ulikuwa unazipa Rwanda na Burundi haki ya kutumia na kusafirisha mizigo yao katika barabara, reli na bandari zetu bure. Ikumbukwe Tanganyika, Rwanda na Burundi zilikuwa nchi moja chini ya utawala wa Mjerumani hadi mwaka 1919 ambapo ziligawanywa katika nchi tatu. Wabelgiji walidai kuwa nchi hizo mbili ambazo ziliwekwa katik usimamizi wao ziwe na haki ya kutumia bandari, reli na barabara kwani zilishiriki kwa namna moja katika kuzijenga na vilevile vitu hivyo vilikuwa ni muhimu kwa uchumi wao. Mwalimu alikataa na hivyo Rwanda na Burundi walilazimika kulipia kwa huduma hizo.

Vivyo hivyo kwa mkataba wa Maji ya mto Nile. Ni muhimu kuelewa kuwa 85% ya maji yanayotiririka na kufika Misri hayatoki upande wa Mto Nile Nyeupe bali Nile ya Bluu. Mto wa Nile Bluu uko Ethiopia. Lakini mkataba ule unaibana Ethiopia isitumie maji yale na Misri imekuwa ikitishia kupigana vita na nchi yoyote ile itakayohatarisha usalama na uhakika wake wa kupata maji hayo. Ikumbukwe kuwe Ethiopia na Misri zilikwisha pigana vita kuanzia mwaka 1875 hadi 1877. Misri ilichapwa.

Kwa sehemu kubwa kama Ethiopia ingetumia kikamilifu maji ya Mto Nile isingekuwa na matatizo ya chakula ambayo yamesababisha mamilioni ya watu wake kufa na njaa na kulazimika kuchangiwa pesa duniani kupitia matamasha ya muziki kama Band Aid. Hivyo sisi Watanzania tuna kila sababu ya kutumia maji ya Mto huo ili kuweza kuboresha maisha ya watu wetu. Cha msingi ni kuwa ni lazima tuhakikishe kuwa tunatunza mazingira ya bonde zima la Ziwa Lweru(Victoria) au kama ambavyo ningependa siku moja liitwe Ziwa Nyerere. Kwa bahati mbaya bonde lake linatunzwa vibaya na hivyo kuchagiza kuharibika kwa mazingira yake. Sehemu nyingi zinazonguka Ziwa Lweru hazina maji ya bomba na wala haziyatumii kwa kilimo cha umwagiliaji. Kupeleka maji Kahama imeonekana ni kitu cha ajabu wakati ni kwamba hata watu wa Tabora, Singida na Dodoma ukiachilia mbali wale wa mikoa yote inayozunguka Ziwa hilo walitakiwa wawe na maji saa zote 24. Tukitaka kufanya hivyo tunatajiwa mikataba hewa ya 1929 na 1959.

Misri ni lazima ijifunze kuishi vizuri na nchi zetu na kushirikiana nazo katika kutunza vyanzo vya maji vinavyotoa maji yanayotiririka na kuingia katika Mto Nile. Ushirikiano na nchi zetu na Ethiopia utaihakikishia uhakika wa maji kwani kama nchi hizo zikishindwa kutunza vyanzo hivyo na Mto huo nazo zitakuwa zimejiharibia. Lakini njama ambazo WikiLeaks imezionyesha juu ya Misri kutaka hata kuzuia kura ya uamuzi ya Watu wa Sudani Kusini zinatisha nasi ni lazima tuzipinge.

Egypt requested delay for Sudan referendum, according to new WikiLeaks cable | Ethiopiaforums.com
 

Kinyambiss

JF-Expert Member
Dec 2, 2007
1,374
1,225
If these people attack Uganda we could take our uranium and give it to uganda to dump in the nile and EFF them all to hell.
 

Nyumbu-

JF-Expert Member
May 26, 2009
987
500
Let them try.
We will poison their water : they use nuclear, we use bilogic.
The winner is the winner, no matter what method is used.....
 

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,545
2,000
hawawezi kufanya hilo kosa. never. mbona watapigika. pili, nyie wenye mawazo ya kutupa sumu kwenye mto/lake, hiyo ni roho chafu toka kwa shetani, watu wengi watakufa na Mungu hapendi watu wengi hivyo wafe...hatuwezi kufaidika chochote kama wamisro wote watapata shida ya maji yenye sumu...wewe uliyeongea hivi naomba dadilisha kauli....roho chafu sana hio unamhitaji Mungu akuokoe.
 

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,763
1,500
hawawezi kufanya hilo kosa. never. mbona watapigika. pili, nyie wenye mawazo ya kutupa sumu kwenye mto/lake, hiyo ni roho chafu toka kwa shetani, watu wengi watakufa na Mungu hapendi watu wengi hivyo wafe...hatuwezi kufaidika chochote kama wamisro wote watapata shida ya maji yenye sumu...wewe uliyeongea hivi naomba dadilisha kauli....roho chafu sana hio unamhitaji Mungu akuokoe.


Kemea na roho chafu ya mafarao....................kutaka kuipiga nchi kwa kuwa maji yanatoka huko!
 

vassil

Senior Member
Apr 13, 2008
122
195
yaani lowassa asingekuwa mwizi angekuwa kiongozi mzuri alisimama kidete kwenye hili swala
 

bucho

JF-Expert Member
Jul 13, 2010
4,966
2,000
kweli edu alikuwa anafanya maamuzi ya kijasiri . tutakukumbuka sana EL
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
hawawezi kufanya hilo kosa. never. mbona watapigika. pili, nyie wenye mawazo ya kutupa sumu kwenye mto/lake, hiyo ni roho chafu toka kwa shetani, watu wengi watakufa na Mungu hapendi watu wengi hivyo wafe...hatuwezi kufaidika chochote kama wamisro wote watapata shida ya maji yenye sumu...wewe uliyeongea hivi naomba dadilisha kauli....roho chafu sana hio unamhitaji Mungu akuokoe.

Wewe unamuongelea Mungu gani, wa Musa, Daudi na Israel kwa ujumla? Kama ni huyo basi kawaongoza waisrael kuangamiza maelfu ya watu wasiokuwa na hatia. Na hata hao wamisiri maelfu walikufa walipojaribu kuwazuia waisrael wasiondoke Misri. Wewe sema tu kwamba azingatie suala la ubinadamu. Lakini kwa hiyo habari ya Mungu, mimi sidhani kama Mungu hapendi watu wauane. Akina Sauli waliua maelfu kwa maelfu na mwisho wa siku akawabariki na kuwasamehe dhambi zote. Mungu ni complex sana linapokuja suala la vita.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom