EFM Sports HQ : Ni kipindi cha michezo au bango la matangazo ya biashara?

Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,063
2,983
Kipindi cha michezo cha Efm kile cha asubuhi kimejaa porojo na matangazo mengi mengi hasa ya kamali.

Kipindi kinaanza saa 3 :00 lakini habari ya kwanza inaanza kusikika baada ya DK 20 huku wakitangaza matangazo tuuu na kupiga masingeli.

Hivi kwanini matangazo yasiwe machache kwakuwa kuna vipindi vingine?

Huyu Kitenge anaruka kutoka nje ya nchi inamaanisha nini kwetu sisi wasikilizaji?

NI HAYO TUU
 
kipindi cha michezo cha Efm kile cha asubuhi kimejaa porojo na matangazo mengi mengi hasa ya kamali. kipindi kinaanza saa 3 :00 lakini habari ya kwanza inaanza kusikika baada ya DK 20 huku wakitangaza matangazo tuuu na kupiga masingeli.
ivi kwanini matangazo yasiwe machache kwakuwa kuna vipindi vingine?
huyu kitenge anaruka kutoka nje ya nchi inamaanisha nini kwetu sisi wasikilizaji?
NI HAYO TUU
Kwahyo mkuu hata manjonjo ya bwakila nayo huyataki au
 
Shukran kama umeliona hilo mkuu walikuja vizuri sana lakini siku zinavoenda ndio wasikilizaji watapungua matangazo hatukatai yasiwepo lakini yawe interval ya mda fulani kipindi kinaanza saa tatu lakini habari ya kwanza saa tatu na nusu hii sidhani kama iko sawa halafu michezo ya kimataifa inaanza 11:50pm kipindi kinaisha 12:00 pm hapo kuna uchambuzi kweli au kuharakisha habari nadhani wanahitaji kurekebisha hili
Mda ni kitu muhimu sana ukipanga vizuri wasikilizaji hawawezi kuchoka kipindi cha redio yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kipindi kiwe mara tatu kwa wiki, ili wakusanye habari, inaonyesha muda mwingine wanakosa habari za kutosha, hivyo kucheza matangazo huku yskijurudia rudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kweli matangazo yamezidi lakini bila hayo matangazo sidhani kama hadi leo kungekuwa na efm
 
Sports HQ wabakiharibu, kuna kipindi nilikuwa mdau wao segment inayoanzia saa tano, ambayo ni habari za kimataifa.

Siku hizi kadri time inavyoenda wanazidi kula muda tu, contents husika zinachukua chini ya 18 minutes.

Inabidi wajitafakari, matangazo hatukatai, ila vipindi vya michezo vinahitaji contents zaidi.

Sports Extra ya Clouds wanajitahidi sana kupunguza matangazo ukilinganisha na vipindi vingi vya Clouds.
 
Hao nimesha achana nao kitambo. Habari za michezo naingia zangu application za michezo ya kimataifa.

Local News za michezo naingia azam app.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kipindi pekee Bongo nachosikiliza kwa sasa cha michezo ni Clouds, tena nafungulia kuanzia 3.45 hivi kwa ajili ya international news, ila huwa wanachemkaga sana basi tu.

Kuna dogo mmoja anaitwa Kotinyo, akiendelea vizuri atakuja kuwa analyst mzuri sana.
 
Back
Top Bottom