EFD je bei yake ni sawa

jjeremiah

Member
Jul 30, 2010
43
13
Wana jf wenzangu napata utata mkubwa kuhusu bei iliyo pangwa kwa ununuzi wa hizi ELECTRONIC FISCAL DEVICE ambapo yenye bei nafuu kabisa ni Tzs 1,860,000/- lakini ukiangalia chombo chenyewe hakifanani na thamani hiyo ya pesa maana ni sawa na calculator ya kawaida iliyoongezewa ka printer kadogo na memory card ya GB 2 kingine ni WAP ambayo ni teknolojia ya kawaida ambayo hata simu za Tzs 30,000/- huwa nazo. Utata huwo naupata pale ninapoangalia vyombo vingine kama vile laptop ambapo yenye thamani ya wastani wa Tzs 1,200,000/- inakuwa na vitu vingi sana na vya kuweza kufanya kazi sawa na hiyo EFD au hata zaidi sasa hii kwanini iwe ghali kiasi hicho, naomba maoni yenu.
 
Mkuu inaelekea una jambo ulitaka kutuambia lakini umeamua kuzunguka kwa kutaka mtu mwingine ajitolee kumfunga paka kengele.. sema tu mkuu ..... uwanja wako huu ......... A S crown-1:
 
Bei za vitu vingi Tanzania feki aidha kutokana na ushuru mkubwa au tu hakuna wa kufuatilia bei za bidhaa. Naona wakubwa pia hutia mfukoni the difference. Infact, ni nafuu kuishi London kuliko Dar- kulingana na bei za umeme nk.
 
Na kuna specific point of sales only... haziuzwi ovyo ovyo... Mradi una wenyewe! do you remember speed governers? redfaces:
 
Back
Top Bottom