EFC BANK YAANZISHA HUDUMA MPYA YA MTANDAO WA BIASHARA "EFC BUSINESS NETWORK" KWA WATEJA WAKE.

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83

Benki ya EFC Tanzania Microfinance Bank ltd leo imezindua huduma mpya kwa wateja wake ya mtandao wa kibiashara wenye lengo la kuboresha mawasiliano kati ya wateja na benki itakayosaidia kurahisisha utoaji huduma hasa katika shuguli zao za ukopeshaji, ambapo Benki hiyo inaamini mawasailiano mazuri na mteja ni jambo muhimu katika kipindi hichi ambapo benki inakua kwa kasi.Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo maeneo ya Victoria Barabara mpya ya Bagamoyo Jijini Dar es slaam Mkurugenzi mtendaji Bwana Bas Nierop amesema EFC sasa ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha inaongeza matawi yake Dar es salaam na Mikoani ili kuweza kuwasogezea wananchi huduma za kibenki na mikopo kwa ukaribu zaidi.
Aidha bwana Nierop ameongeza kuwa miaka sita sasa imepita tangu EFC ianze kutoa huduma zake kama taasisi ya mikopo na imekuwa ikijiendesha vizuri kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wake kiasi kwamba wameiona ipo haja ya kutanua wigo wa kibiashara na kuwa Benki kamili yenye uwezo wa kutoa mikopo kwa wajasiliamali na kuwahudumia kibenki zaidi, ambapo wataweza kutoa na kuhifadhi fedha kwa usalama zaidi nakunufaika
na huduma hiyo.
Nae Mkurugenzi wa kitengo cha mikopo Bwana Robert Pascal amesema katika kuboresha huduma zao Benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kukutana na wateja wake mara kwa mara ili kuweza kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wateja wao na kuona namna bora ya kuboresha huduma zao kwa wateja wao.Pia bwana Pascal kawasisitiza wateja kua waaminifu ili kujenga mahusiano mazuri na benki.
Meneja masoko wa Benki hiyo Bi Waheeda Mohamed amewataka wakazi wa Dar es salaam kuchangamkia fursa ya kujiunga na benki yao kwani sasa benki hiyo imeweza kupiga hatua na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo kwa masharti nafuu ambayo hata Mwananchi wa kwaida anaweza kumudu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom