Eeh Mungu kwa tabia hii ya wanaume kutembea na vichaa tuadhibiwe zaidi

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,197
2,024
Ninandika huku nina majonzi mazito nyoyoni kutokana na tabia ambayo tunayo sisi wanamume. Mwanaume ni kiongozi katika familia na jamii zetu hakuna mwenye kupinga katika hili. Lakini kwa tabia hizi tunazoziendeleza zinatuweka katika daraja la chini kabisa.

Ijumaa karimu bandugu. Kuna haka katabia ambako kameenea katika maeneo mbalimbali katika mikoa yetu. Najua umewahi kuona vichaa hawa wa jinsia ya kike wakiwa na ujauzito.

Inasikitisha sana kuona mwanamke asiye na utimamu wa akili (kichaa) akiingiliwa kimwili hadi kuwa mjamzito bila ridhaa yake. Tena kuna baadhi yao wamezaa hadi watoto watatu na zaidi wakiwa katika ukichaa huo. Yaani inafika kipindi wengine wanachomwa sindano za kuzuia mimba.

Wanaofanya tabià si wengine ila sisi wanamume, tumekumbwa na nini sisi mbona kuna wanawake wengi tu.
Hii tabia ni ya kukemewa sana.
 
Ninandika huku nina majonzi mazito nyoyoni kutokana na tabia ambayo tunayo sisi wanamume.
Mwanaume ni kiongozi katika familia na jamii zetu hakuna mwenye kupinga katika hili.Lakini kwa tabia hizi tunazoziendeleza zinatuweka katika daraja la chini kabisa.

Ijumaa karimu bandugu.Kuna haka katabia ambako kameenea katika maeneo mbalimbali katika mikoa yetu.Najuwa umewahi kuona vichaa hawa wa jinsia ya kike wakiwa na ujauzito.Inasikitisha sana kuona mwanamke asiye na utimamu wa akili(kichaa) akiingiliwa kimwili hadi kuwa mjamzito bila ridhaa yake.Tena kuna baadhi yao wamezaa hadi watoto watatu na zaidi wakiwa katika ukichaa huo.Yaani inafika kipindi wengine wanachomwa sindano za kuzuia mimba.Wanaofanya tabià si wengine ila sisi wanamume,tumekumbwa na nini sisi mbona kuna wanawake wengi tu.Hii tabia ni ya kukemewa sana.
Hiki ulichoandika ni unyanyapaa Kwa mlemavu wa akili. Licha ya kuwa ni walemavu ila bado wana haki ya kuzaa.
 
Pole yao.

Ila pana watu wenye akili tena hadi vibosile/ mikoani wanawaita wenye ukwasi huwa wanafanya hayo mambo. Japo, hapa imani za mshana jr zinahusishwa na vitendo hivyo though, sina uhakika maana ni mambo ya imani.

Japo, pana wengine wanapata kutoka kwa walemavu wa akili wenzao.
 
Sikatai kama wanakubali kwa hiari yao lakini cha kushangaza wengi wanabakwa tu kitu ambacho ni unyanyasaji mkubwa dhidi yao
 
wanazaaga na vichaa wenzao.
mtu mwenye akili timamu hawezi zaa/baka na kichaa.
kichaa si lazima kuokota makopo.
Kuna mmoja miaka ya 90 alizaa na DMO. Alikuwa busy kuzunguka kwenye korido za hospital (jina kapuni). Mtoto kazaliwa ni kopo na mfuniko... ikabidi DMO aridhie matunzo ya mama na watoto... hakumaliza mwezi tangu scandal ile alihama
 
Mkuu hata vichaa wenyewe huwa wanapigana mabao! Mwaka mmoja hivi nikiwa Morogoro, vichaa me na ke wakakutana kwenye kidaraja pale karibu na round about ya Masika, ghafla tukaona wanaangushana na kupigana mbupu pale. Walipomaliza wakakimbilia kwenye kijito kujimwagia maji. Sasa hapo kichaa ke hawezi kubeba mimba?
 
Sikatai kama wanakubali kwa hiari yao lakini cha kushangaza wengi wanabakwa tu kitu ambacho ni unyanyasaji mkubwa dhidi yao
Mtu mwenye ulemavu wa akili hana kisheria uwezo wa kuridhia jambo lolote! Ila hiyo haimnyimi haki ya kuzaa.
 
Pole yao.

Ila pana watu wenye akili tena hadi vibosile/ mikoani wanawaita wenye ukwasi huwa wanafanya hayo mambo. Japo, hapa imani za mshana jr zinahusishwa na vitendo hivyo though, sina uhakika maana ni mambo ya imani.

Japo, pana wengine wanapata kutoka kwa walemavu wa akili wenzao.
Ni kweli kabisa pia hata wenye akili timamu wanahusika kwa vitendo hivi
 
Mkuu hata vichaa wenyewe huwa wanapigana mabao! Mwaka mmoja hivi nikiwa Morogoro, vichaa me na ke wakakutana kwenye kidaraja pale karibu na round about ya Masika, ghafla tukaona wanaangushana na kupigana mbupu pale. Walipomaliza wakakimbilia kwenye kijito kujimwagia maji. Sasa hapo kichaa ke hawezi kubeba mimba?
Hiyo ni one in thousand,wengi wao wanapewa na wenye akili timamu
 
Siyo ufisi ila level ya uelewa tu! Kuna mkunga mmoja alishtakiwa kwa udhalilishaji alipotamka maneno aliyohisi ni ya kumfariji mwanamke "kiwete" aliyefikishwa hospitalini kujifungua. Yule mkunga alitamka kuwa "jamani jamani, ni mwanaume gani huyu aliyemfanyia unyama huu huyu mlemavu!" Ndo akanunua kesi hivyo tayari.
 
Hata kama wana haki ya kuzaa huoni kama mnawapa mzigo mkubwa yy kutunza hao watoto katika hatari??? Mvua yake jua lake na mtoto jamani hebu acheni
 
Ninandika huku nina majonzi mazito nyoyoni kutokana na tabia ambayo tunayo sisi wanamume.
Mwanaume ni kiongozi katika familia na jamii zetu hakuna mwenye kupinga katika hili.Lakini kwa tabia hizi tunazoziendeleza zinatuweka katika daraja la chini kabisa.

Ijumaa karimu bandugu.Kuna haka katabia ambako kameenea katika maeneo mbalimbali katika mikoa yetu.Najuwa umewahi kuona vichaa hawa wa jinsia ya kike wakiwa na ujauzito.Inasikitisha sana kuona mwanamke asiye na utimamu wa akili(kichaa) akiingiliwa kimwili hadi kuwa mjamzito bila ridhaa yake.Tena kuna baadhi yao wamezaa hadi watoto watatu na zaidi wakiwa katika ukichaa huo.Yaani inafika kipindi wengine wanachomwa sindano za kuzuia mimba.Wanaofanya tabià si wengine ila sisi wanamume,tumekumbwa na nini sisi mbona kuna wanawake wengi tu.Hii tabia ni ya kukemewa sana.
Wana haki ya kupata mapenzi,
 
Back
Top Bottom