Ee Mwenyezi Mungu naomba uniponye ikishindikana kupata dawa hapa jf

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Ilikuwa tarehe 10.11.2012 nikahisi maumivu ndani ya pua kwa ndani kabisa yaani kama allergy hivi. Kesho yake nikahisi baridi, kichwa kuuma, mafua na nikipenga kamasi ni za kung`ang`ania baada ya siku kama 4 nikaanza kuhisi harufu puani nayo ikazidi ikaendelea na tundu la kushoto la pua kutoa kamasi zenye usaha na unanuka sana nikaenda kwa daktari akachunguza pua yangu akaniandikia dawa za Ampiclox na paracetamol nikatumia bila kuona badiliko na kufikia sasa hivi nikiinamisha kichwa harufu inatoka kali sana nashindwa hata kuongea na watu na mawazo yangu yameenda mbali sana mpaka kufikiria kuwa labda ubongo umeharibika. Naombeni msaada jamani.
 
Pole ndugu, KIRI ZAB53:5b,
pia nenda hospitali kubwa usiende dispensary,
wataalamu wanakuja
 
Nenda hospital mapema ukafanyiwe check up kabisa,hospitali kubwa kama ulivyo elekezwa. Na BCR.
 
Pole inaweza kuwa sinus..nenda hospital utapona wala usiwe na wasiwasi

Sent from my GT-N7100 using Tapatalk 2
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom