SuperImpressor
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,504
- 646
Ilikuwa tarehe 10.11.2012 nikahisi maumivu ndani ya pua kwa ndani kabisa yaani kama allergy hivi. Kesho yake nikahisi baridi, kichwa kuuma, mafua na nikipenga kamasi ni za kung`ang`ania baada ya siku kama 4 nikaanza kuhisi harufu puani nayo ikazidi ikaendelea na tundu la kushoto la pua kutoa kamasi zenye usaha na unanuka sana nikaenda kwa daktari akachunguza pua yangu akaniandikia dawa za Ampiclox na paracetamol nikatumia bila kuona badiliko na kufikia sasa hivi nikiinamisha kichwa harufu inatoka kali sana nashindwa hata kuongea na watu na mawazo yangu yameenda mbali sana mpaka kufikiria kuwa labda ubongo umeharibika. Naombeni msaada jamani.