Ee mwenye enzi Mungu nikumbuke tena katika upweke wangu

uwarid81

Member
Oct 15, 2017
25
31
Ndungu zangu wanajamvi Poleni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa,

Mimi ni mgeni humu naomba mnipokee wanajamvi.

Kama title inavyojieleza hapo juu,

Mimi naitwa UWARIDI ni MKRISTO.Nimezaliwa 1981, ni mjane nina watoto 3. Mume wangu alifariki miaka 6 iliyopita.

Nimepitia changamoto nyingi sana za kulea familia peke yangu kwa kipindi chote cha upweke, kwani kutokana na maisha ambayo tulikuwa tumejiwekea sikuona kama kwa wakati huo ningeweza kupata a right person ambaye angeweza kulibeba jukum la baba kikamilifu kwa watoto wasio wake!Pili sikupenda kabisa kuwa disappoint watoto kuwaletea.

Baba mwingine mapema haswa ukizingatia mapenzi makubwa sana aliyokuwa nayo mume wangu kwa familia yake. Bila shaka humu kuna wanandoa na hapa nazungumzia ndoa bora zilizotawaliwa na upendo wa dhati heshima uvumilivu jinsi ambavyo ni vigumu kuzoea maisha ya upweke.

Angalao naweza kusema nilikubali kuusononesha moyo wangu kwa kipindi chote hicho ili watoto wangu wasogee kidogo. Na sasa umefikia wakati ambao kwangu naona ni sahihi kumuhitaji ubavu wangu.

MAISHA: Maisha yangu ni ya kati ya kuweza kujimudu, lakini haimaanishi kama sitohitaji msaada wa mwenza wangu hapana. Nahitaji mume ambaye atayatambua majukumu yake lakini pia aniruhusu kuendelea na shughuli zangu za ujasiriamali kwani mbali na majukumu ya kawaida niliyonayo ADA tu za wanangu kwa mihula yote kwa mwaka ni 9.6milion. Lakini ukiachana na hilo mimi binafsi siwezi kukaa bila shughuli yoyote ya kuniingizia kipato kwani nimeona umuhimu wa hilo.

AINA YA MUME NINAEMTAKA; kwakweli sita base sana kwenye kabila ila napenda ni base sana kwenye tabia! Asiwe mlevi, awe na hofu ya MUNGU, awe anaitambua thamani ya mke bora, awe anayatambua na kuyahisi machungu ya kusalitiwa. Ndoa bora inajengwa na upendo wa dhati uaminifu, hizi silaha mbili zitazalisha kuheshimiana kuvumiliana katika shida ba raha, kuthaminiana.

KABILA; Mimi ni Mchaga.

IMANI; Mimi ni mkristo hivyo ningependa mkristo, lakini kama atakuwa muislam basi nitaomba ndoa ya bomani kila mmoja abaki na dini yake.

NB; kwa mujibu wa maadili yangu siruhusiwi kuolewa nikaishi na mume mwingine kwenye mji nilioachiwa na marehemu mume wangu.

Naomba kuwasilisha asante sana.
 
Pole dada,nikupongeze kwanza kwa kumuenzi mumeo kwa ulilowafanyia watoto,wanawake wengi kizazi hiki mume akifa hajazikwa anawaza kuolewa...Mungu akupe hitaji la moyo wako akakuletee mtu mwema mtakaeweza kuishi kama ulivyoandika hapo juu,usisahau kusali ktk hilo!
Amen, asante sana mpendwa wangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom