Ee Mungu uliyehai, huwezi kusikia vilio vya waTz? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ee Mungu uliyehai, huwezi kusikia vilio vya waTz?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Julius Kaisari, Jan 19, 2011.

 1. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Mungu mtakatifu, mwenye mamlaka yote, uliyeumba vitu vyote,vinavyoonekana na visivyooneka,.. Tazama Tanzania yako uliyoibariki,tangu siku za mwanzo za uhuru wake,kwa kuipa kiongozi aliyekuheshimu na kukuogopa wewe Mungu. Nchi yako imevamiwa na kutu,viwavi,dumadu,nzige,wevi,matapeli,mafisadi,na watu wasiokuheshimu wala kukuogopa. Nakuomba kwajili ya urithi na mali ya watz wote,inayochotwa na wajanja kuwahi, RA,JK,EL, NM,EC,IM, na wengine wote waovu, uilinde na uwapatilize uovu kuanzia kizazi chao cha kwanza hadi cha nne.. Wote tuseme.... Amen
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mungu hafanyi kazi ya kusaidia asiyejisaidia.
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Mungu si mwanadamu,pia mawazo yake si kama yako..kinachohujumiwa ni mali ya watoto wa tanzania wote.. Kwani wewe hiyo hewa na jua na mvua umevistahili kwa kujisaidia uvipate? Hiyo ni dhihaka.
   
 4. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Bila shaka kauli kama "tuingie mtaani tuwatimue RA,EL, &co" ndo ungpenda kuisikia. Pole!. Mungu anaweza kulainisha moyo wa jambazi,mdhulumu,mwivi,mwongo, wakawa watu wema. Nadharia nyingi zimeonesha harsh actions huwa hazisaidii kuwarudi waovu.. Mfano,kunyonga wauaji hakujawahi kuonesha kuwa ni suluhu ya watu kuua. Bali labda kuwafunga miaka mingi na hao kuja kutoa ushuhuda kwa walionje kuhusu maisha ya jail,nk. Ambapo ni Mungu mwenyewe anaingia kulainisha mioyo na kuwafanya kujutia uovu...okay bro/sister?
   
 5. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa udhati huu wa maombi yako, siku si nyingi utashangaa Mungu anavyosikiliza kilio cha wengi na kutoa jibu lisilozuilika hata kwa jeshi zima la nchi. UkweliKitugani, nyamaza usilie sana, ukilia utatuliza wengi Watanzania.

  Ila dawa iko jikoni usihofu.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mungu tayari ameshawasaidia wanaadamu na hao watoto Wa Tanzania kwa kuwapa maarifa.

  Kama maombi pekee yangesaidia unaenda kazini kufanya nini? Kaa nyumbani uombe chakula
   
 7. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli dada, jibu ni dawa aina ya 'Tunisia' kwa magonjwa ya Ufisadi uliokithiri, uchakachuaji na mauaji ya Watanzania kwa kiburi cha ngedere kwa akina mama mashambani.
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Acheni kumpa mungu kazi za kihuni. Wezi mnawaweka madarakani wenyewe halafu mnataka mungu awaondoe? Wabunge mnawachagua wenyewe washindwa kuwajibisha serikali halafu mnataka mungu awawajibishe? Mungu ana kazi nyingi, Haiti, Somalia, Palestina, n.k.

  Kwani huko Tunisia ni mungu ameondoa serikali madarakani?
   
 9. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,935
  Likes Received: 672
  Trophy Points: 280
  ukwelikitugani.... nimependa sana ulivyo na uchungu na nchi hii.... je una uchungu kwa maslahi ya nani..? wengi wana uchungu lakini wakiwekwa kwenye nyadhifa nyeti hawakumbuki tena kama kuna wevi, mafisadi , matapeli, viwavi na nzige
   
 10. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu,unajua mimi kwa nafasi niliyonayo ofcn kwangu imebidi niitafute haki,na kutoa haki kwa kuwajibika. Najua iko siku nitakuwa mtu muhimu zaid kwa taifa hili. Lakini tofauti na wachangiaji hapo juu,nashukuru kwa kuungana nami. Unajua kitu tunachosahau waliowengi ni nafasi ya Mungu ktk matatizo haya,na nchi yetu.. Kimsingi tunapaswa kuendelea na mapambano kama sehemu ya wajibu wetu, remind you,hizi purukushani zetu tunaoitwa vyama vya upinzani its simply our responsblty. Lakini Mungu naye ana nafasi yake. If u r Christian believer,utakumbuka ajabu na ishara na miujiza mingi Mungu alowatendea watu waliodhulumiwa.
   
 11. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mungu anataka kutufundisha jambo muhimu watanzania. Ameacha mafisadi watamalaki ili tujue madhara yake na hatimaye tuweze kubaini maadui wa nchi yetu na tuchukue hatua madhubuti.
   
 12. BigTime

  BigTime Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  E bhana hii fua imetulia sana, Mungu alishasikia kilio chetu hata kabla hatujaanza kulia ila katuruhusu tuombe kwa maneno asikie, na this time kilio hiki kimekuwa kila sehemu. Nchi ya neema na ahadi imegeuka kuwa jangwa kuu hata tone la maji hakuna, tunabaki kula upepo wenye vumbi jepesi. Hawa watu wanaoitwa mafisadi wamezidi kumnyonya na kumla ng'ombe huyu Tanzania, hawaonei uchungu ndama wanaotegemea maziwa ya ng'ombe huyu, wanamyonya hadi kwato na kumbakiza mbavu nje....Ee Mola wetu sikia hiki kilio cha waja wako...Amen
   
 13. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka kwa uzito wa hoja yako, nimenyong'onyea kabisa na hata kufikiria kuondoa kauli hapo juu.
  Dawa hapa ni kutumia mtindo wa Tunisia nchi nzima bila kuchelewa hata wiki.
   
 14. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  mkuu hata yaliyoteka tunisia ni sehemu ya wajibu wao. Mungu ananafasi yake kumuumbua mwovu.. Kama si neema unaweza ukatunisia na bado ukaambulia vipigo na kuwa kilema!. Mungu tupe ujasiri tuendelee kupigania hii nchi yako ulotupa mwenyewe. Legeza na nyong'onyeza nguvu za wevi kina rostam,kikwete,chenge,mkono,lowasa (tena huyu kwa unafiki wake siku akija madhabahuni pako mpige dafurao,upofu iwe funzo kwa mafisadi wote.)
   
 15. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wewe na vitukuu vyako vyote mtakufa kabla mungu hajafanya hayo mnayomtaka afanye. ulikwishaambiwa sauti ya watu ni sauti ya mungu. mkiweka wezi madarakani mungu anasema hewala hivyo ndivyo walivyopendezwa kufanya. hata hivyo anawaonesha kwamba mliowachagua ni wezi, nyie mnasubiri yeye sasa awaondoe?? Kwani huko tunisia watu hawakufa na kuwa vilema? alikudanganya nani kwamba madabdiliko ya mfumo wa kisiasa huteremshwa kutoka mbinguni? soma historia ya kanisa na jamii za kale, tafadhali.

  hata wana wa israele walipigana na kufa na waliopigana sio waliongia kumiliki israeli. na hawa walikuwa na direct contact na mungu siyo wewe unayewasiliana naye kwa hisia na kudhani kwamba eti atakusikiliza na kutekeleza unachotaka. wao walikuwa na mazungumzo na mungu, direct, lakini walilazimika kupigana na waliuawa na walikuwa vilema. so please expand your view of thinking.
   
 16. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo ninayoyaogopa! Kwenye post post moja leo nimesema idadi ya watu wanaoamua kuokoka kutafuta majibu ya maswali na suluhisho la shida zao inaongezeka siku hadi siku! Watu wanatafuta majibu ya shida zao. Jf nako wanaotakiwa kufikiri kwa kina na kutoa suluhu ya matatizo ya nchi hii wamekuwa wachungaji na mshekhe!

  Tumeamua suluhisho ni kumuachia Mungu.

  Kuna bwana mmoja alikuwa na kesi ya kubaka. Kwa madai yake alikuwa amebambikiziwa. Baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao akaambiwa ajitee. Huku akibubujikwa na machozi akamwambia hakimu 'namuachia Mungu'. Kweli, hukumu ilipotoka akachezea miaka 30 jela!!

  Wapo watakaosema Mungu anatoa fundisho hapo. Fundisho gani? Usiniachie kesi yako nikutolee utetezi. Utafungwa!

  Hao wezi wanaenda kanisani na misikitini. Wanatoa michango na waumini wanawaombea 'Mungu akuongezee hapo ulipotoa baba'.....RA anachangia kwaya na kwa wakristo Mungu ni Mungu wa sifa na kwa kuimbiwa sala inafika haraka!! Sasa sijui hapo inakuwaje!

  Gurudumu na PakaJimmy mnisaidie!
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Alberto, natumaini hauanzishi mjadala wa dini, kwa maana ya kwamba watu badala ya kujadili mantiki ya ulichosema wataanza kukushambulia wakidhani unakufuru imani zao.

  wanaambiwa na viongozi wao wa dini kwamba kila kitu mwachie mungu. viongozi wa dini za kisasa nao wanatumia falsafa kama za waganga wa kienyeji. Kwamba wale wote wenye matatizo ya ndoa, mapenzi, kupata kazi, kutopanda cheo kazini, kuota ndoto mbaya....

  ukiwa na jamii ambayo inapumbazwa kwa misingi ya kishirikina, iwe ni sangoma au yesu, mantiki huondoka. na kama ulivyosema mwenyewe kwamba watanzania wengi wameingia kwenye hizo imani, hivyo hawaoni sababu ya kufikiri na kutekeleza bali kuomba na kumwachia mungu. na kama nilivyosema hapo juu, siyo kazi ya mungu.

  hata askofu kakobe, wakati ana mgogoro na tanesco, alijikuta anavunja mafundisho yake mwenyewe. alipoulizwa kwa nini usimwachie usiangushe maombe na kumwachia mungu awashuhulikie tanesco alijibu, mungu ana kazi nyingi na kazi ya kutetea himaya ya kanisa siyo kazi ya mungu bali ya waumini wa mungu.
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurudumu, umethibitisha imani yangu katika umakini wako! Umesema vyema. Jukumu la kuleta mabadiliko liko mikononi mwetu. Tunachohitaji ni kumuomba Mungu atupe ujasiri wa kuthubutu na hekima ya kutenda!
   
 19. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Mi namuona Mungu kwenye yote yanayoendelea hapa Tanzania,huwezi chukua hatua wala kuungana na wanaopinga dhambi na dhuluma kama hujafahamu kwanini wanafanya hivyo???Mungu anatufahamisha yale yanayoendelea ambayo yangeweza kuwa siri,ili wenye macho waone na wenye masikio wasikie and vice versa,baada ya kufahamu ukweli,atatupa nguvu ya kupambana na hayo magumu kama ni ufisadi,ufitini etc etc....Usitarajie kumuona Mungu mambo yanapokuwa shwari,Mungu yupo kwenye safari hata pale yanapokuwa machungu na ya kukatisha tamaa.
   
 20. m

  mkambu New Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kuwa Mungu huanzia pale ambapo mwanadamu huishia kufikiri, kutenda. naamini Mungu anaweza
   
Loading...