Edwin Mtei: Rais Magufuli asiige kila kitu kutoka kwa Nyerere

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aanze kasi ya kushughulikia kero mbalimbali za wananchi, kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusu aina ya
ufanyaji kazi wake.

Rais Magufuli alianza kasi hiyo kwa kuzitembelea idara mbalimbali za Serikali zikiwamo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pia ameshafika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kushuhudia namna huduma zinavyotolewa. Wananchi wameonekana kufurahishwa na kasi hiyo.

Kitendo cha kufuta sherehe za uhuru zinazofanyika kila Desemba 9 kila mwaka na kasha kuagiza mabilioni ya fedha yaliyotengwa kwa ajili ya sherehe hizi yaelekezwe katika mahitaji muhimu, kimewagusa Watanzania kiasi kwamba baadhi yao wameufananisha uongozi wa Dk Magufuli na ule wa Rais wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere.

Miongoni mwa watu walioguswa na hatua za Rais Magufuli ni aliyewahi kuwa gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania (BoT) na mwasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mtei anasema anamatumaini makubwa na kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Swali: Unamtazamaje Rais Magufuli?
Jibu: Ni mtu mwenye shauku na maendeleo, ni mzuri kama atasimamia na kuishi maneno yake. Ni mtu ambaye atasimamia maendeleo yetu na ninaamini atasimamia ukuaji wa uchumi wetu. Pamoja na kuridhishwa na kasi ya Rais Magufuli, naamini kwamba kwa sehemu kubwa anatekeleza sera na ilani ya Chadema. Kile anachofanya kwa sasa kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwenye ilani na sera zetu na tutashirikiana naye katika kuisadia hii nchi yetu.

Swali: Je, ungepata nafasi ya kumshauri Rais Magufuli ungemwambia nini.
Jibu: (anavuta pumzi) Kwanza ningempongeza kwa kupata ushindi katika hali ngumu sana, lakini ningemshauri maliasili za taifa hili zitumike kwa ajili ya Watanzania wote na wananchi washirikishwe katika kuendeleza nchi yao. Ningemwambia ahakikishe Watanzania wanashirikishwa katika umiliki wa ardhi na kuwekeza. Wao ndiyo wawe wahusika wakuu katika kusimamia rasilimali zao na siyo vinginevyo hata wageni wakiingia nchini wawe kama wabia tu. Nashauri kwamba wageni wanaotaka kuwekeza katika sekta ya madini, wauze hisa zao kwa Serikali ambayo itakuwa ikimiliki hisa nyingi zaidi. Kwa kufanya hivyo, maliasili za Taifa zitatumiwa na wazawa wenyewe. Ningemshauri Rais Magufuli ahakikishe Watanzania wananufaika na rasiliamali zao ambazo walipewa na Mwenyezi Mungu kwa kusudi la kuwakomboa na umaskini.

Swali: Unadhani Rais Magufuli anairejesha Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere?
Jibu: Kwanza unajua mimi napinga siku zote Azimio la Arusha kwa kuwa naamini liliturejesha katika umaskini, hivyo nisingependa Rais Magufuli airejeshe nchi yetu katika enzi za Mwalimu Nyerere. Rais Magufuli anaweza kuchukua mambo machache kutoka kwa Mwalimu Nyerere ikiwamo ufufuaji wa viwanda vilivyokufa. Ningependa airejeshe Tanzania kwa watu wake kufaidi matunda ya rasilimali zao kama wananchi wawe na ajira, mashamba na uchumi wa kuwatajirisha wote na siyo watu wachache.

Swali: Je, ni nini unaona kimebadilika tangu enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa.
Jibu: Mambo mengi yamebadilika sana kama uchumi umepaa na watu wanafaidika kupitia uchumi huo, lakini tatizo lililopo hapa ni kwamba wanaofaidi ni wachache kuliko wale wengi ambao ni maskini wa kutupwa. Tanzania haina mfumo wa kuwabana matajiri kuhakikisha wanawasaidia maskini kuinua uchumi wao ili nchi ipige hatua kwenye maendeleo, lazima iweke mfumo huo.

Swali: Je una maoni gani kuhusu baraza jipya la mawaziri?
Jibu: (Anatabasamu) Kwanza hili siyo baraza dogo hata kidogo, laiti kama angekuwa na mawaziri 18 hadi 24 hapo tungesema baraza ni dogo. Hili nililiona wakati nikiwa gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) na mshauri wa Rais katika masuala ya uchumi, Mwalimu Nyerere alikuwa na baraza dogo.
Naamini Rais Magufuli kabla ya kuteua baraza hilo alizingatia watu waadilifu na wenye uzoefu na siyo walafi. Rais Magufuli analenga kuleta mabadiliko nchini kwa lengo la kuwafanya Watanzania wafaidi matunda ya rasilimali zao kama gesi, mafuta na madini, basi baraza hilo halina budi kuendana na kasi yake.

Mawaziri hawana namna ni lazima waendane na kasi yake au waondoke. Ni lazima hili baraza lihakikishe linafanya kama aliyewateua anavyotaka kuwatumikia Watanzania wote.

Chanzo: Mwananchi
 
Lowassa anazidi kuwa yatima wa fikra za kisiasa ndani ya CHADEMA!

Wakati Lowassa anadai ni mshindi wa kura za Urais wa Tanzania, Mzee Mtei ambaye ndiye mwenye CHADEMA anautambua ushindi wa Rais Magufuli na kutoa pongezi.

Fikra za Mzee Mtei kisiasa huwa ndizo fikra za Freeman Mbowe!

Politically, Lowassa is fading away every day!

Jinamizi la kifo cha kisiasa kwa wagombea Urais wa Tanzania ambao walishindwa uchaguzi limeanza kumwandama pole pole!
 
Mzee mtei nyamaza bado tunakumbuka wewe na mkono mlivyochoma benki kuu mkaiba mamilioni ya pesa. Nyerere aliwastahi sana mlitakiwa kunyongwa
 
Dah. Lowasa inabidi ajitafakari uhusiano wake na mbowe maana kama hadi babu mtei anasema hivi ujue game limebadilika sana
 
Mzee mtei nyamaza bado tunakumbuka wewe na mkono mlivyochoma benki kuu mkaiba mamilioni ya pesa. Nyerere aliwastahi sana mlitakiwa kunyongwa

Mzee hataki ya Nyerere ila tuendelee tulivyo leo alafu anasema watanzania wengi wamekuwa maskini alafu anasema tukirudi kwa Nyerere umaskini utazidi ...kiufupi hajui tatizo ni nini kwa sshivi huyu mzee
 
Mzee mtei nyamaza bado tunakumbuka wewe na mkono mlivyochoma benki kuu mkaiba mamilioni ya pesa. Nyerere aliwastahi sana mlitakiwa kunyongwa

..Mtei aliondoka serikalini mwaka 1979.

..Benki kuu iliungua moto mwaka 1984.

..siyo rahisi kwa mtu ambaye yuko nje ya system[MOF & BOT] kwa wakati ule kuweza kuchoma moto benki kuu.

NB:

cc MsemajiUkweli, Edwin Mtei
 
Last edited by a moderator:
Dah. Lowasa inabidi ajitafakari uhusiano wake na mbowe maana kama hadi babu mtei anasema hivi ujue game limebadilika sana
Lowassa anapigwa teke na wenye CHADEMA!

Biashara na wenye CHADEMA imeisha baada ya kushindwa kwenye uchaguzi Mkuu.
 
Safi sana Edwin Mtei, nimefurahishwa sana na mahojiano yako na imeonesha kwa kiasi kikubwa kuwa wewe Edwin Mtei huna wivu wa husda bali una wivu wa maendeleo kitu ambacho ndicho kinachotakiwa kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kwa mara nyingine tena, safi sana Edwin Mtei
 
..Mtei aliondoka serikalini mwaka 1979.

..Benki kuu iliungua moto mwaka 1984.

..siyo rahisi kwa mtu ambaye yuko nje ya system[MOF & BOT] kwa wakati ule kuweza kuchoma moto benki kuu.

NB:

cc MsemajiUkweli, Edwin Mtei
Hata mimi huwa ninashangaa kuhusu hizi tuhuma.

Hata hivyo tuhuma bila vielelezo ni jadi katika siasa za nchi yetu.
 
Mzee hataki ya Nyerere ila tuendelee tulivyo leo alafu anasema watanzania wengi wamekuwa maskini alafu anasema tukirudi kwa Nyerere umaskini utazidi ...kiufupi hajui tatizo ni nini kwa sshivi huyu mzee
Nadhani ana maana siyo yote ya utawala wa Mwl. Nyerere kwa sasa ni mazuri katika mazingira ya sasa, kitu ambacho hata mimi ninakubaliana naye.
 
Safi sana Edwin Mtei, nimefurahishwa sana na mahojiano yako na imeonesha kwa kiasi kikubwa kuwa wewe Edwin Mtei huna wivu wa husda bali una wivu wa maendeleo kitu ambacho ndicho kinachotakiwa kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kwa mara nyingine tena, safi sana Edwin Mtei
Ni kweli, Mzee Mtei ametoa majibu ambayo ni balanced bila kujali tofauti za kiitikadi.
 
Unalichukia Azimio LA Arusha wakati huohuo unataka rais ahakikishe rasilimali zinakuwa chini ya wananchi.
Rasilimali kuwa chini ya wananchi kivipi??
How? For god's sake!
 
Mzee mtei nyamaza bado tunakumbuka wewe na mkono mlivyochoma benki kuu mkaiba mamilioni ya pesa. Nyerere aliwastahi sana mlitakiwa kunyongwa
Pamoja na maovu ya mzee Mtei, kama kweli, bado kuna kitu Dr. Magufuli anaweza kuchukua kwenye ushauri huu! UPINZANI WA KISIASA SIO UADUI!
 
..Mtei aliondoka serikalini mwaka 1979.

..Benki kuu iliungua moto mwaka 1984.

..siyo rahisi kwa mtu ambaye yuko nje ya system[MOF & BOT] kwa wakati ule kuweza kuchoma moto benki kuu.

NB:

cc MsemajiUkweli, Edwin Mtei

Joka,
Mimi sijui lisemwalo ni kweli au la, bali huu ndio muono wangu,

  1. Edwin Mtei Kuondoka u-Gavana 1979 haina maana kuwa yeye hawezekani kuwa aliichoma BoT. Edwin Mtei kama Gavana wa muda mrefu, bado alikuwa na watu wake ndani ya benki.
  2. Pesa aliyo-nayo Mtei, ina-walakini kama ile ya Lowassa. Zote hazina maelezo walikozipata.
  3. Licha ya hizi tuhuma kuwepo kila wakati, Mtei hajalikanusha hili hata siku moja, bali kakaa kimya, kitu kinachofanya hizi tuhuma zishike mizizi
  4. Onus iko kwa Mtei na wengine wote walio na pesa zisizoelezeka wawaHabarishe wananchi jinsi walivyojitengenezea huo utajiri.
 
Lowassa anazidi kuwa yatima wa fikra za kisiasa ndani ya CHADEMA!

Wakati Lowassa anadai ni mshindi wa kura za Urais wa Tanzania, Mzee Mtei ambaye ndiye mwenye CHADEMA anautambua ushindi wa Rais Magufuli na kutoa pongezi.

Fikra za Mzee Mtei kisiasa huwa ndizo fikra za Freeman Mbowe!

Politically, Lowassa is fading away every day!

Jinamizi la kifo cha kisiasa kwa wagombea Urais wa Tanzania ambao walishindwa uchaguzi limeanza kumwandama pole pole!

Mtei anasema "Nampongeza kwa ushindi alioupata kati hali ngumu" nini tafsiri?
 
Unalichukia Azimio LA Arusha wakati huohuo unataka rais ahakikishe rasilimali zinakuwa chini ya wananchi.
Rasilimali kuwa chini ya wananchi kivipi??
How? For god's sake!

Hata mimi sielewi ....labda aje humu mzee wetu kufafanua zaidi ...

CC Edwin Mtei
 
Last edited by a moderator:
Unalichukia Azimio LA Arusha wakati huohuo unataka rais ahakikishe rasilimali zinakuwa chini ya wananchi.
Rasilimali kuwa chini ya wananchi kivipi??
How? For god's sake!
Nadhani Mzee Mtei ana maana ya kuchukua vile ambavyo vinaweza kuingia kwenye sera ya soko huria. Kwa maana nyingine, dira yake ya kiuchumi iwe katika siasa za mlengo wa kati.
 
Kubwajinga,

..Mzee Mtei hakuondoka BOT kwa kashfa yoyote ile.

..Hata katika uwaziri wa fedha hakuondoka kwa kashfa pia.

..Baada ya kuondoka Mwalimu Nyerere alipendekeza jina la Mtei kwenda kufanya kazi IMF desk la Afrika.

..Kwa msingi huo utaona Mwalimu na Mtei hawakuwa na mahusiano yoyote mabaya hata baada ya kutofautiana kimsimamo/kikazi wakati Mtei alipokuwa Waziri wa Fedha.

..kutokana na sababu hizo hapo juu sioni motive yoyote ile ya Mzee Mtei kufanya hujuma dhidi ya bot au taasisi yoyote ile hapa Tanzania.

..Mzee Mtei alipokuwa IMF aliendelea kufanya kazi na viongozi mbalimbali hapa Tanzania kutokana na majukumu yake kama Mkurugenzi wa IMF Africa desk.

..Mwisho, Mzee Mtei alipostaafu IMF alirudi Tanzania na moja ya kazi alizofanya ni kuongoza Tume ya marekebisho ya sheria zetu za kodi na ushuru. Raisi Mzee Ali Hassan Mwinyi ndiye aliyemteua kuongoza tume hiyo. Ripoti ya "TUME YA MTEI" ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa mamlaka ya ukusanyaji mapato TRA.

..Mtei angechoma moto Benki Kuu, basi Mzee Mwinyi asingemwamini na kumteua kuwa Mwenyekiti wa Tume muhimu kama ile iliyoangalia sheria na muundo wa idara zetu za kodi na ushuru wakati ule.

..Mimi nadhani Mzee Mtei hajakosea kuyaacha madai haya kama yalivyo. Ni madai yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

cc Mdanganywa, MsemajiUkweli
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom