Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,294
24,118
Tundu Lissu na rekodi yake ya kisiasa, ati sasa naye anautaka Urais.
...............

APR
17

EDWIN MTEI ASIKITISHWA NA ALAANI KITENDO CHA TUNDU LISSU KUMTUKANA BABA WA TAIFA, MWL. NYERERE

Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei,

Founder Chairman of CHADEMA.
 
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani (akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka na viongozi wa chini. Wakampamba .

Hint: katiba ya 1977

Udiwani,unapingika kortini
Ubunge,unapingika

Uraisi,hapana. Akitangazwa,imeisha hiyo.
Yeye alikuwa raisi. If you know you know
 
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani(akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka Na viongozi wa chini. Wakampamba .

Acha wivu
Ji overrate na wewe kama ni rahisi hivyo!
 
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani(akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka Na viongozi wa chini. Wakampamba .

Hint: katiba ya 1977

Udiwani,unapingika kortini
Ubunge,unapingika

Uraisi,hapana. Akitangazwa,imeisha hiyo.
Yeye alikuwa raisi. If you know you know
Still Mwalimu Nyerere, even in death, he is a major force.
Anaheshimiwa sana kwa kuweka misingi ya utaifa.
Mtukane kijinga at your own risk
 
Tundu Lissu simuoni kama anafaa uraisi(hisia zangu). Ila Nyerere is overrated
Kuna watu humu tusingekuwa nao kutokana na sehemu wanazotoka. Leo mungekuwa wapagazi na wafanyakazi wasaidizi. Elimu ilikuwa sehemu fulani tu za nchi, Mwalimu aliondoa hilo.

Watu wengi hawaeliwi msingi huu mkubwa wa kujenga utaifa.
 
Binafsi sijawahi kumwelewa kiviile mzee wetu Nyerere,Kuna maamuzi mengi ya kiboya aliyafanya na kuficha ukweli, hakuwa muwazi na alikuwa mbinafsi sana, aliona yeye ndo Yuko sahihi tu na watanzania wote no maboya. Ni Kama kagame anavyoiongoza Rwanda
 
Kuna watu humu tusingekuwa nao kutokana na sehemu wanazotoka.
Leo mungekuwa wapagazi na wafanyakazi wasaidizi.
Elimu ilikuwa sehemu fulani tu za nchi, Mwalimu aliondoa hilo.
Watu wengi hawaeliwi msingi huu mkubwa wa kujenga utaifa.
Kama nchi gani?
 
Unazungumziaje kipengele cha ubunge/udiwani kupingika,uraisi kutokupingika(ambacho kiliwekwa wakati wake)?
 
Nyie vijana mliozaliwa 2000s ni bora mkae kimya tu
Nyerere is overrated. Kwa umasikini huu wa kutupwa. Kuipeleka nchi vitani(akimpigania Obote arudi madarakani baada ya kupinduliwa Na IDD Amini). Nyerere alitengeneza kuogopeka Na viongozi wa chini. Wakampamba .

Hint: katiba ya 1977

Udiwani,unapingika kortini
Ubunge,unapingika

Uraisi,hapana. Akitangazwa,imeisha hiyo.
Yeye alikuwa raisi. If you know you know
 
Tusiishi katika ukomo wa kifikira kuendana na historia ya nchi yetu. Ndiyo! Mwl. Nyerere ni Muasisi na Baba wa Taifa letu, na alikuwa kiongozi mashuhuri kwa wakati wake, ambaye alilitetea sana utu wa watu nchini, barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Lakini hiyo siyo sababu ya kumfanya akose wakosoaji wa misimamo yake. Kama binadamu awaye yeyote yule, alikuwa na madhaifu yake. Na jambo hili linathibitika kupitia kauli yake mwenyewe kabla mauti hayamkuta. Alikuwa "remorseful" kwa baadhi ya maamuzi yake kama kiongozi, hasa kwa yale yaliyoleta matokeo hasi.

Kwa hiyo Tundu Lissu naye ni kiongozi mwenye sifa zake ktk taifa lake. Na pia mwenye maono yake ya kulipeleka taifa letu ktk "next frontier" kupitia mapungufu ya kihistoria ambayo anaamini kwa dhati yalitokana na Baba wa Taifa. Tuzipime "constructive criticisms" zake. Wala tusizibeze kwa kauli za jumla jumla tu.

Tuje na hoja mujarabu hapa jukwaani na kuainisha wapi amekosea. Sio hoja za juu za kutumiwa na mabeberu. Kama hizo "claims" ni za kweli, wakosoaji wa TL waainishe ni lini, wapi na kwa vipi anahusika.
 
Back
Top Bottom