Edward Ngoyai Lowassa awe mgombea pekee urais 2015

galiya

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
302
131
KWAKUA Mh Lowasa ameonyesha ana hamu kubwa sana ya kua Rais wa nchi hii kwani pamoja na Mwalimu Nyerere kutishia kurudisha kadi yake No. 1 ya CCM mwaka 1995,iwapo Lowasa angeteuliwa kua Rais kwani akiwa kijana mdogo tu wa miaka 42 alikua na utajiri mkubwa mno uliopatikana isivyo halali, Lowasa ameendelea na jitihada hizo waziwazi na kwa kasi kubwa sana

NA

KWAKUA Mh Lowasa katika kuhakikisha PIGA UA GARAGAZA lazma anatinga Magogoni mwaka 2015, ameanza kutumia fedha nyingi mno ambazo hatimaye zimemwezesha kujaza watu wake kwenye jumuia za CCM ili kumrahisishia kubeba bendera ya chama chake 2015

NA

KWAKUA Mh Lowasa amekua akizunguka nchi nzima kuendesha mambo ya fund raising za kuwezesha ujenzi wa shule, makanisa na misikiti ikiwa ni njia nyingine ya kujiweka karibu na wananchi wengi iwezekanavyo

NA

KWAKUA licha ya afya yake kua mgogoro hadi anaenda mara kwa mara Ujerumani ambako daima anadai ni macho tu ndio yanamsumbua ingawa kuna wambea wanadai eti ana stroke upande wake wa kushoto(sijui hawa wambea wameambiwa na DR wake!), lakini Lowasa ameonyesha kupangamikakati lukuki ya kumfikisha Magogoni kwa nguvu moja na ari moja

NA

KWAKUA WANAJAMIIFORUM karibu 99% wameonyesha wanamkubali Lowasa kuliko hata Dr Slaa,Zito au Lipumba kua RAIS WA TZ 2015

HIVYOBASI badala ya CCM kupoteza hela nyingi za kuandaa vikao vya kumchagua mgombea Urais na badala ya vyama vyote vya upinzani makini kama Chadema na vingine Mburura kama CUF kupoteza hela na kumweka mgombea wao na pia badala ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kutumia pesa nyingi bila sababu wakati watanzania KARIBU WOTE wanamtaka Lowasa awe Rais wao NAPENDEKEZA Mh Lowasa APITE BILA KUPINGWA

Great Thinkers, imekaaje hii?
 
Asante sana kwa maoni mazuri, na uzuri katiba yetu ya sasa inaruhusu uhuru wa mawazo. Hata hivyo ni vizuri kusikiliza mawazo kutoka pande mbali mbali ili ujiridhishe kuwa pendekezo lako linaungwa mkono. May God bless you!!!
 
hatuna rais mwingine ajaye zaidi ya lowasa,tunahitaji rais mwenye udhubutu jamani,membe aende huko na unafiki wake
 
Back
Top Bottom