Edward Ngoyai Lowasa aka LAIGHWANAN aende IKULU au KEKO?


G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
Ndugu Watanzania wenzangu, kama mnavyojua mwaka 2015 tutapata Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu (kwa mujibu wa taratibu zetu) ndiye atakayeiongoza nchi yetu 2015-2025 hivyo hatutakiwi kufanya kosa kwani kosa dogo tu tujue tumeumia na majuto ni mjukuu. Watu wengi wameishaonyesha nia ya nafasi hii ya Urais na mmoja wao ni Mh Edward Lowasa.

Kwangu mimi naona huyu bwana hafai kabisa kwenda Ikulu bali yeye anafaa kwenda Keko!!. Maovu na mabaya yake yoote yameishaanikwa wazi humu JF kwa takriban mwaka mzima sasa hivyo sitapenda kuyarudia kwani hata Watanzania wa vijijini wanayafahamu fika. Hata hivyo ovu lake kubwa ambalo hata yeye privately anakiri kuwa nalo na ambalo limeganda kwenye mwili wake na ambalo anahitaji special Jiki kujisafishia ili liondoke ni suala la Rushwa.

Kwa mtazamo wangu THABITI NA USIOTETEREKA siku ambayo Rais wa awamu ya Tano anaapishwa na Jaji Mkuu, Lo-rushwa (sio Lowasa) anatakiwa awe anaingizwa mlango wa Keko kwa kifungo cha maisha (tena hata hiyo adhabu sio kali sana maana watu kama yeye kule China ni Kunyongwa tu). Msiulize eti atakua amehukumiwa na mahakama gani. Kwa Lo-rushwa, hakuna cha PCCB, POLISI wala MAHAKAMA inayoweza kuona ndani. Si mnakumbuka jinsi PCCB walivyomsafisha kwenye Richmondul? Ndio maana alipokua Ujeruman akiuguza afya yake -alisema eti Hosea amefanya kazi nzuri anastahili pongezi wakati watanzania woote wanajua Hosea nae yumo genge la wala rushwa na hana nia thabiti ya kupambana na rushwa.Chaguzi za Dodoma ambako Lo-rushwa na genge lake walidhalilisha utu wa wanadamu wenzao kwa kugwa Lo-rushwa kwenye vyoo vinavyonuka tsh 40,000 na 70,000 zinaonyesha uovu wa mtu huyu na jinsi PCCB ilivyoshindwa kuwanasa watu wake kwa makusudi kwakua Hosea nae ni "WALEWALE" Mahakama pekee ya kumtia hatiani Lo-rushwa ni Wananchi wa Tanzania na sheria pekee itakayotumika ni UZALENDO.

Lo-rushwa ahukumiwe kula MBOKO 100. Siku hiyo anaingia Keko ale mboko 50 ila chondechonde wakati wa kumtandika mboko hizo mtandikaji(nashauri ateuliwe Morani mmoja aliyeshiba) aangalie upande wakushoto wa mwili wa Laighwanan asije akamtonesha matatizo yake mengine. pia nashauri mkewe ie Regina awepo kushuhudia maana wakati mmewe anakwapua mihela yeye alikua akichekelea na kununua vidan, mawax na vikuku vya kuwakoga wanawake wenzake!!!. Hivi uchu gani huu wa kuwaumiza binadamu wenzio we Lo-rushwa ? Lo-rushwa akiwa Ofisi ya PM wakati wa mafuriko ya kusini yeye akakwapua hela za mafuriko wakati wananchi wanateseka hawana hata pa kukaa! Watoto wetu wanakosa viwanja vya kuchezea na hatimae hata timu ya Taifa inakosa vipaji kwakua tu wakati akiwa Waziri wa Ardhi Lo-rushwa aliviuza viwanja vyote kwa wahindi! Ama kwa hakika Lo-rushwa atakua ni KUNI ya kuchomea waovu wote mbele ya Mungu, Uroho gani huu????

Najua kuna wapambe wake wengi hawatapendezwa na uzi huu, bali mimi kama mtanzania kwa kuandika hii thread natimiza wajibu wangu kama viongozi wetu ambao wamekua wakituhimiza kwamba tumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo. Mwalimu alisema anachukia sana rushwa na dawa ya mla rushwa ni fimbo siku ya kuingia gerezani na siku ya kutoka akamwonyeshe mkewe!

Mtu huyu Lo-rushwa mwenye uchu mkubwa wa mali tukimpa nchi kwa hiyo miaka kumi na hasa ukitilia maanani ugunduzi wa gesi na mafuta, je nchi hii itasalimika? Au mnaompenda mnadhani akiwa Rais ndo atabadilika na kua mtu mwema na kuwapendeni Wadanganyika? WIZI na RUSHWA NI HULKA!Kitendo cha hivi karibuni kule Dodoma kutumia MAHARAMIA YA KISOMALI kama Bashe kutaka kumngoa Mwenyekiti wetu kwa njia za Umafia kinatakiwa kulaaniwa na kila mpenda amani na ndio "the last nail in his coffin", maana hata baadhi ya wapambe wake wamechukizwa sana na kitendo hicho.

Mwalimu katika hotuba yake ya tarehe 12.6. 1982 mbele ya NEC alisema "Rushwa ni Kansa mbaya sana. Haitoshi tu wewe kutokua mla rushwa bali ni lazma wewe kama Kiongozi au mwananchi wa kawaida kuonyesha umechukua hatua gani kupambana na rushwa au hata tu kukemea. Kitendo cha mataifa mengi kumkemea Nduli Idd Amini alipotuvamia kilionyesha wao wanajua kwamba Amin alikua na makosa na ilionyesha wanachukizwa na hali hiyo. Hivyo ndugu zangu, kila mtu kwa nafasi yake apambane vilivyo na rushwa". Mwalimu, huu uzi ni katika KUKUENZI KWA VITENDO!

Great Thinkers, je Lo-rushwa aende Ikulu au Keko?
 
kawakama

kawakama

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
1,302
Points
1,225
kawakama

kawakama

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
1,302 1,225
wewe unaonekana una chuki binafsi tu na RAIS WETU EL
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
KAWAKAMA

Mkuu jibu swali kwa kutoa hoja . Swali rahisi tu aende keko au ikulu? Ni hilo tu kaka
 
A

adobe

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
1,957
Points
2,000
A

adobe

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
1,957 2,000
Hakuna wa kumpiku lowasa kiutendaji.huyu bwana si dhaifu kama alivyo jk ni mtu wa maamuzi.kuna usemi usemao bora mwizi kuliko tondo.so am suporting lowasa for presidence.keko nenda wewe na roho yako mbaya
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
29,154
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
29,154 2,000
Naunga mkono aende Keko ila pia uhakikishe anakwenda na wenye mizigo yao ambao alijitolea kuwabebea!.
 
bucho

bucho

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Messages
4,824
Points
2,000
bucho

bucho

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2010
4,824 2,000
inaelekea wewe umetumwa sio bure .
 
K

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2008
Messages
887
Points
225
K

Kwame Nkrumah

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2008
887 225
Halafu kua makini, kampeni kama hizi zinaweza ku-backfire vibaya sana.
Romney alikua anatangaza atashinda kwa sababu alifikiri minorities na vijana hawatajitokeza kupiga kura.
Lakini kumbe kauli hiyo iliwa motivate watu kujitokeza kwa wingi kuliko 2008.
Punguza kasi Mkuu, be aware of the unintended consequences, mashambulizi binafsi dhidi ya Lowasa yanamuongezea umaarufu.
i welcome that,anytime.
 
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Messages
908
Points
500
Age
39
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2011
908 500
Chuki binafsi kwa mheshimiwa EL kajipange uje na hoja zinazo eleweka siyo kutokwa na povu bila hoja za msingi..
alikutuma mwambie umshindwa acha kuropoka kama kasuku..
 
J

jerry-B

Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
25
Points
0
Age
30
J

jerry-B

Member
Joined Apr 6, 2012
25 0
Lo-rushwa a.k.a Lo-fisadi anastahili kwenda keko maisha yke yte yaliyobaki,kma ni mtu mwenye maamuz magumu na muadilifu auelezee uma tuhuma zinazomkabili asa ishu ya Richmonduli aliyodai kasingiziwa
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
PASCO

Nafurahi kua ukiwa mtetezi mkubwa wa lowasa umekiri kua kiukweli anafaa kwenda keko. Ila Mkuu sijakuelewa uliposema aende na aliowabebea mizigo yao. Je ni akina nani hao? Tiririka maana tunachohitaji watanzania WAZALENDO ni kua mtu tutakaempeleka Magogoni lazma awe ni mtu safi
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
NONONO BARAKA

Mi nimetoa hoja zangu. KWAKUA umeziona ni mbovu ebu tupe zako nzuri sio unafura kwa hasira na kutokwa povu!
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
JERRY-B

Kula 5, nakubaliana na wewe 100%
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
KWAME NKRUMAH

Kwanza naomba kutoa rai ubadilishe jina. Vijana wa nchi hii mliozaliwa miaka ya 90 mnapenda kujipachina majina huku hamjui maana yake. Huko aliko Nkrumah akigundua kua kuna mtu anatumia jina lake huku akitetea MAFISADI walai laana utakayoipata ni mbaya sana
 
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
1,257
Points
0
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
1,257 0
Mkuu, ahsante sana. Lkn EL siyo Lighwanan. yule ni Mmeru pure. Kawaokota tu wamasai. Ndiyo maana anapingwa sana na wamasai wasomi.
 
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
1,257
Points
0
Mawenzi

Mawenzi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
1,257 0
Mkuu, ahsante sana. Lkn EL siyo Lighwanan. yule ni Mmeru pure. Kawaokota tu wamasai. Ndiyo maana anapingwa sana na wamasai wasomi.
 
G

galiya

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
302
Points
0
Age
43
G

galiya

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
302 0
MAWENZI

Lowasa ni MMASAI au MMERU? Mbona kwenye CV ameandika yeye ni MMASAI? Kama kweli ni Mmeru lakini anadai ye MMASAI nini lengo la kufanya hivyo?
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
39,310
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
39,310 2,000
Hakuna wa kumpiku lowasa kiutendaji.huyu bwana si dhaifu kama alivyo jk ni mtu wa maamuzi.kuna usemi usemao bora mwizi kuliko tondo.so am suporting lowasa for presidence.keko nenda wewe na roho yako mbaya
Sasa akaonyeshe utendaji wake huko KEKO kwenye kulima na kupasua mawe.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Messages
908
Points
500
Age
39
naninibaraka

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2011
908 500
NONONO BARAKA

Mi nimetoa hoja zangu. KWAKUA umeziona ni mbovu ebu tupe zako nzuri sio unafura kwa hasira na kutokwa povu!
Kwanza nikurekebishe id yangu ni naninibaraka na siyo nononobaraka,la pili JF ni sehemu ambayo members hutoa maoni yao freely lkn isiwe kigezo cha kupakana matope kutokana na misukumo ya mtu,join date yako tu kama JF MEMBER ina describe the type of a person ur,la msingi jenga hoja za msingi hata aliyekutuma afurahie alichokutuma na siyo kutokwa na povu hovyo...si mtetei lowassa wala simjui lkn the whole ccm is corrupt,even aliyekutuma ni corrupt kwa taarifa,siku si nyingi utamjua aliekutuma vizur
 

Forum statistics

Threads 1,294,754
Members 498,027
Posts 31,187,074
Top