Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
1FBE2C0F-3849-4E0E-A906-8D88F95B086F.jpeg

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mh. Edward Lowassa leo amefika katika kata ya Makiba akiambatana na Mbunge wa Arumeru Mh. Joshua Nassari, Mbunge wa Simanjiro Mh. James Milya na baadhi ya viongozi wa chama wa kanda ya Kaskazini ili kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo Bi. Joyce Rutha.

Hii ni sehemu ya aliyoongea:

Edward Lowassa: Leo Nimeona kwenye mitandao ya kijami kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi CCM, siwezi kurudi CCM hayo ni maneno ya Kipuuzi na Ndoto za mchana

Edward Lowassa: Nikajiuliza hata Patrobass Katambi? Nikagundua ooohh Kumbe ni Msukuma... Ndio Maana

Edward Lowassa: Ninaiomba Serikali ya CCM iache mara moja kutuongoza kwa ukabila taifa letu halikujengwa katika misingi hiyo

Edward Lowassa: Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza. Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.
 
Edward Lowassa: Leo Nimeona kwenye mitandao ya kijami kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi ccm siwezi kurudi ccm hayo ni maneno ya Kipuuzi na Ndoto za mchana

Edward Lowassa: Nikajiuliza hata Patrobass Katambi? Nikagundua ooohh Kumbe ni Msukuma... Ndio Maana

Edward Lowassa: Ninaiomba Serikali ya ccm iache mara moja kutuongoza kwa ukabila taifa letu halikujengwa katika misingi hiyo
Eti! huyu mzee sijui ana matatizo gani yeye ndio kawaida yake kuwagawa watu ooh mara zamu ya kkkt kuongoza nchi leo tena kazuka na la ukabila tumuogope kama ukoma huyu mzee
 
Wanawaiba wapinzani kwa ahadi za vyeo ili mradi ahakikishe anaudhoofisha upinzani. Kumbe hajui kwamba mtu mwenye msimamo thabiti hawezi kudanganywa kwa vyeo kama ilivyo kwa akina Kitila.
 
Dikteta anatongoza wapinzani kwa ahadi za vyeo ili mradi ahakikishe anaudhoofisha upinzani. Kumbe hajui kwamba mtu mwenye msimamo thabiti hawezi kudanganywa kwa vyeo kama ilivyo kwa akina Kitila.
Ni sahihi kwa Edward kuongelea ukabila na KUWATUHUMU wasukuma ilhali mtendaji wa chama ni msukuma?!
 
Edward Lowassa: Leo Nimeona kwenye mitandao ya kijami kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi ccm siwezi kurudi ccm hayo ni maneno ya Kipuuzi na Ndoto za mchana

Edward Lowassa: Nikajiuliza hata Patrobass Katambi? Nikagundua ooohh Kumbe ni Msukuma... Ndio Maana

Edward Lowassa: Ninaiomba Serikali ya ccm iache mara moja kutuongoza kwa ukabila taifa letu halikujengwa katika misingi hiyo
Edward Ngoyai Lowassa sio Rahisi aandike maneno hayo ya hiyo paragraph ya Pili.
 
Eti! kumbe ni msukuma huyu mzee sijui anamatatizo gani yeye ndio kawaida yake kuwagawa watu ooh mara zamu ya kkkt kuongoza nchi leo tena kazuka na la ukabila tumuogope kama ukoma huyu mzee
Kaenda Kenya kaingilia siasa za Kenya..matokeo yake kawagawa watu..anashindwa kujua hata hao wapinzani wa Kenyatta wapo wanaomkubali yeye lowasa..
 
Serikali ya sasa imetawaliwa na ukabila sana, sijui hata tunakoelekea.
Labda nikutonye kitu usichojua kuhusu chadema sehemu zote ambazo chadema imeshinda tanzania bara imeshinda kwa kuwa maeneo hayo yana moja walutheri wengi na pili wachaga wengi.Mikoa ya kaskazini ni ngome ya walutheri na wachaga wengi.Dar es salaam ngome yao iko wilaya ya kinondoni na ubungo.kikabila na kidini chadema iko juu
 
Katika kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, ni muhimu kuwa na vyama vilivyojijenga maeneo yote ya nchi.

Kuna tatizo la fikra kwa wengi kwamba maeneo yale ambayo upinzani umeimarika CCM haipo, hizo ni fikra potofu.

Ili kuhakikisha umoja na ustawi wa taifa, kuna haja ya kuwepo sera ya kuendeleza vyama vya siasa vienee maeneo yote ya nchi kuwajengea wananchi fikra chanya kisiasa.
 
Edward Lowassa: Leo Nimeona kwenye mitandao ya kijami kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi ccm siwezi kurudi ccm hayo ni maneno ya Kipuuzi na Ndoto za mchana

Edward Lowassa: Nikajiuliza hata Patrobass Katambi? Nikagundua ooohh Kumbe ni Msukuma... Ndio Maana

Edward Lowassa: Ninaiomba Serikali ya ccm iache mara moja kutuongoza kwa ukabila taifa letu halikujengwa katika misingi hiyo

Mwanahabari Huru, kama umesahau, sikiliza video clip hii utupe maoni yako, ukirejea ulichokileta hapo juu.

Back
Top Bottom