Edward Lowassa: Vijana wanaichukia CCM

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wana JF,

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameweka wazi kuwa vijana wengi ktk hii nchi wanaichukia CCM kwa sababu ya Ukosefu wa ajira. Katika hili la ajira mzee Lowassa amejaribu kutoa utofauti uliopo kati ya watoto wa wakulima na wanao jiita watoto wa wakubwa amesema watoto hao wa wakubwa wamepata kazi sehemu nzuri. Wamepata kazi TRA au BoT na ndani ya miezi sita utamwona anaendesha gari zuri na ana nyumba yake ya kifahari.

Wakati huo mtoto wa mkulima au yule ambaye amezaliwa katika familia ambayo sio bora, pamoja na kisomo chake ataendelea kusaga lami hadi kiatu alichotoka nacho chuoni kinakuwa upande.

Hivyo WAZIRI MKUU PINDA ameombwa alitafutie ufumbuzi suala hilo.

HAYA VIJANA WA JF KAZI HIZO ZINAKUJA NI NYIE KUWA AGRESSIVE JUU YA HILO DONT HESITATE TO MAKE APPLICATION IF IT IS OUT

MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAA
 
Mtoe fisadi huyo hana lolote la maana mnafiki na anakimbilia kiti tuu!
 
kijana mwenye akili nzuri hawezi kulaghaiwa kwa maneno ya kina lowasa
ni upuuzi mtupu kwa mwenye ufahamu
 
Acha uchirika, wewe ni mwongo, hivi lowasa ni mtu wa kusema watoto wa wakubwa wako TRA na BOT, wakati ndo wako wanae na wa marafiki zake.Usitujaribu peleka umbea wako huko.
 
ndio anajua leo!!!! yeye amekua kwenye system kwa miaka tele aliwasaidiaje vijana? je yeye watoto wake nao wanasaga lami????

WIZI MTUPU!

au ndo kujisafisha...................
 
Huyo Lowasa anajikomba tu kwa serikali ili wampe kauwaziri katika wizara fulani,hana lolote la kukemea wala kushauri maana bado yupo katika mkondo ule ule wa wenye nacho.

Ukweli unabakipale pale kuwa vijana hawaichukii CCM bali wanataka mabadiliko,na kwa kuwa mabadiliko hawayapati CCM huyatafuta mahali pengine wanapoona yapo.
 
chanzo GWIJI LA HABARI TANZANIA,HABARI LEO,KWA MALA YA KWANZA WAANDIKA HABARI YENYE MLENGO WA KUSHOTO

MAPINDUZIIIIIII DAIMAAAAAA
 
I even wonder why he dared to utter such nonsense, au ndio anajishtake mwenyewe na wenzake ambao watoto wao ndio wanaofaidi nchi hii japo akili zao ni bogus kulinganisha na akili za watoto wa wayonge ambao they have to struggle to reach where they are academically lakini hakuna ajira maana ajira chache zinapewa watoto wa wakubwa na wahisani wao; labda uhonge ndio ufanikiwe. EL angekaa tu kimya kuliko kujiaabisha zaidi kujaribu kuongea ongea mambo yanayoleta hisia za kukasirisha watu
 
Lowasa ana majibu ya Vijana Kuchukia CCM..........asituchore! atuambie leo ni hela ngapi zimetumika kwa kampeni za CCM; tisheti, vitenge, kufia, magari ya kifahari, rushwa, kuhamisha watu na mabasi kwenda kwenye mikutano ya kampeni? Hizi hela zote zingefanya mambo mangapi ya kuwasaidia watanzania hususan vijana? na hizi hela ccm walizipata wapi? Nawashangaa sana watanzania; juzi tu kampeni watu wamevaa tisheti na kofia za ccm wakisema hakuna kama wao leo uchaguzi umeisha wanasema maisha ni maguma..........eti pertol na bidhaa zingine zimepanda sana!! hivi vitu vimepandishwa na serikali ipi na kwaninin? Pia ni nani aliyewapigia kura? watanzania wenzagu tufike mahali tubadilike tuwe kitu kimoja......kuna haja ya kohoji mafuta yanapopanda na ikibidi kuandamana nchi nzima! angalia wenzetu Kenya bei ya mafuta imepanda kidogo tu.......chama cha wafanyakazi kimetoa tamko mafuta yawe bei ileile vinginevyo wataandamana nchi nzima. Mungu tusaidie watanzania wale ambao wamelazwa usingizi na ccm waamke!
 
Huyo Lowasa anajikomba tu kwa serikali ili wampe kauwaziri katika wizara fulani,hana lolote la kukemea wala kushauri maana bado yupo katika mkondo ule ule wa wenye nacho.

Ukweli unabakipale pale kuwa vijana hawaichukii CCM bali wanataka mabadiliko,na kwa kuwa mabadiliko hawayapati CCM huyatafuta mahali pengine wanapoona yapo.

Kweli mkuu kwani hata mie naona matamshi yale kama yanalenga kujijengea njia ya kupewa wizara ya Kazi na maendeleo ya vijana
 
. Lowasa amesema kile kilicho moyoni mwake,lakini je ana dhamira ya kutenda aliyoongea?
Tuache kumuandama lowasa kwa kuali yake hiyo? Na baadala yake tuangalie kama kuna ukweli wa kauli yake na kama upo je njia sahihi ya kupambana na halia hiyo ni ipi?
Off topic:
hivi lowasa kabla ya kashfa ya richmond, alikuwa mtu wa namna gani?
 
Na kama ni kweli Lowasa ameyasema hayo, basi kampeni zake za uraisi zimeanza rasmi.
 
wana jf,

waziri mkuu mstaafu, edward lowassa ameweka wazi kuwa vijana wengi ktk hii nchi wanaichukia ccm kwa sababu ya ukosefu wa ajira. Katika hili la ajira mzee lowassa amejaribu kutoa utofauti uliopo kati ya watoto wa wakulima na wanao jiita watoto wa wakubwa amesema watoto hao wa wakubwa wamepata kazi sehemu nzuri. Wamepata kazi tra au bot na ndani ya miezi sita utamwona anaendesha gari zuri na ana nyumba yake ya kifahari.

Wakati huo mtoto wa mkulima au yule ambaye amezaliwa katika familia ambayo sio bora, pamoja na kisomo chake ataendelea kusaga lami hadi kiatu alichotoka nacho chuoni kinakuwa upande.

Hivyo waziri mkuu pinda ameombwa alitafutie ufumbuzi suala hilo.

Haya vijana wa jf kazi hizo zinakuja ni nyie kuwa agressive juu ya hilo dont hesitate to make application if it is out

mapinduziiiii daimaaaaaa

pumbafu!!!!!!!!!!
Alipayuka maneno haya katika gazeti lao la mtanzania ijumaa ya wiki iliyopita.

Mwambie kwanza arudishe zile zote alizoliibia taifa hili ili zisaidie kutengeneza ajira za vijana badala ya kuozea katika mabenki ya kigeni zikitengeneza ajira za wazungu.

Ninyi kusika maneno mshashangilia?
 
Wana JF,

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameweka wazi kuwa vijana wengi ktk hii nchi wanaichukia CCM kwa sababu ya Ukosefu wa ajira. Katika hili la ajira mzee Lowassa amejaribu kutoa utofauti uliopo kati ya watoto wa wakulima na wanao jiita watoto wa wakubwa amesema watoto hao wa wakubwa wamepata kazi sehemu nzuri. Wamepata kazi TRA au BoT na ndani ya miezi sita utamwona anaendesha gari zuri na ana nyumba yake ya kifahari.

Wakati huo mtoto wa mkulima au yule ambaye amezaliwa katika familia ambayo sio bora, pamoja na kisomo chake ataendelea kusaga lami hadi kiatu alichotoka nacho chuoni kinakuwa upande.

Hivyo WAZIRI MKUU PINDA ameombwa alitafutie ufumbuzi suala hilo.

HAYA VIJANA WA JF KAZI HIZO ZINAKUJA NI NYIE KUWA AGRESSIVE JUU YA HILO DONT HESITATE TO MAKE APPLICATION IF IT IS OUT

MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAA
Usimpe sifa ambayo hana. Nani alikwambia Lowasa alistaafu? Ni Waziri Mkuu aliyewajibishwa na ufisadi wake period!
 
Ni kweli hawaipendi, ila kakosea sababu; Vijana hawapendi pombe za kienyeji, hawavai t-shirt za chagua CCM barabarani.
Pia huuliza kwanza, kabla ya kushangilia hovyohovyo!!
 
Kwani yameanza leo...alipata nafasi akafanya nini kuliondoa hilo tatizo..?
 
Back
Top Bottom