Edward Lowassa: Vijana wanaichukia CCM

Yeye mcheza senema za Bongo movie huyo simuoni wala smsikiii akila migahawani au akipanda Daladala hahah Lo mimvi shame on yu
Ni mawazo ya kimaskini na hivyo ndivyo ccm wametujenga Watanzania. Ili nchi iweze kupiga hata tunahitaji kwanza kujikomboa kutoka kwenye ujinga huu(jambo ninaloliona gumu). Hakuna taifa duniani lililoendekeza unafiki na uduni wa mawazo likaendelea. Na hakuna taifa duniani limeendelezwa na maskini.
Tanzania inahitaji watu wa aina ya Lowasa ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi, najua watu wataona hiki ni kituko lakini tunabakia kituko zaidi kwa kukumbatia fikra mgando. Always mwenye hela ndiyo huwa na fikra pana juu ya hela. Maskini amejaa choyo, kihoro, kisokorokwinyo, unafiki umbea na masengenyo. Ndiyo maana taifa letu limejaa masengenyo, unafiki na umimi. Hakuna mpango wa kuifanya nchi kuwa sehemu ya matumizi ya akili na taaluma.
Kitendo cha ccm kubakia na itikadi ya ujamaa na kujitegemea wakati tuko kwenye mfumo wa soko huria, ni unafiki wa kujilimbikizia umaskini wa akili. Rais wa nchi kusema yeye ni Rais wa maskini ni kuliangamiza taifa. Na leo tunaona kama tunanyoosha mambo, lakini hakuna lililopinda linalohitaji kunyooshwa. Ni kauli za kufubaza akili za wananchi.
 
Wana JF,

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameweka wazi kuwa vijana wengi ktk hii nchi wanaichukia CCM kwa sababu ya Ukosefu wa ajira. Katika hili la ajira mzee Lowassa amejaribu kutoa utofauti uliopo kati ya watoto wa wakulima na wanao jiita watoto wa wakubwa amesema watoto hao wa wakubwa wamepata kazi sehemu nzuri. Wamepata kazi TRA au BoT na ndani ya miezi sita utamwona anaendesha gari zuri na ana nyumba yake ya kifahari.

Wakati huo mtoto wa mkulima au yule ambaye amezaliwa katika familia ambayo sio bora, pamoja na kisomo chake ataendelea kusaga lami hadi kiatu alichotoka nacho chuoni kinakuwa upande.

Hivyo WAZIRI MKUU PINDA ameombwa alitafutie ufumbuzi suala hilo.

HAYA VIJANA WA JF KAZI HIZO ZINAKUJA NI NYIE KUWA AGRESSIVE JUU YA HILO DONT HESITATE TO MAKE APPLICATION IF IT IS OUT

MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAA
Huyu Mzee naona anaanza kupagawa.Kwani yy watoto wake ktk kundi la wakuluma au vigogo?

Hebu anaewajua wapo wapi na wanafanya nini amuumbue huyu mzee.
 
Ana makampuni mengi awape ajira na mikopo vijana asitunze pesa ili aje anunulie vijana makofia matshirt na kukodi helikopta kumi wakati wa kampeni za 2020.
Ni wakati muafaka mheshimiwa Lowassa aonyeshe anaweza kuwafanyia nini watanzania.
 
Back
Top Bottom