Edward Lowassa: Tujitokeze kwa wingi Sept 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu

Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,628
2,720
Leo nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Sisi,
Miezi michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.

CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.

Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi tuendelee kuwa wamoja hivi hivi, tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna nguvu kubwa kama ya Umma.
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.

KUHUSU UKUTA .

Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo ,Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .

Wasuluhishi wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. Mtu mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .

POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutaoambana nao mmoja mmoja, hatutahangaika na jeshi tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . Ni bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.

Tabia za baadhi ya viongozi ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki za kidemokrasia .

Tujitokeze kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu . Tuna chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni.

facebook wall..

14021594_1152820424784545_1744431915309270186_n.jpg

14080032_1152820404784547_1503435098246334171_n.jpg

14141709_1152820418117879_7427980042456843053_n.jpg
 
Natabiri kutokea yaliyotokea Pemba mwaka 2001.. Lowassa kama una uchungu na nchi kakae mbele usikimbie kama Maalim seif alivyo wakimbia wapemba wakipukutika kama kuku.. Naamini baada ya Sept 1 mkiambiwa mimi sijaribiwi mtakuwa mnaelewa maana yake.. Ngojeni muone mziki.
 
eheheh kama episode fulani hivi,alafu ndio yale mambo "kama una ubavu?,vuka mstari"
 
Leo nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Sisi,
Miezi michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.

CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.

Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi tuendelee kuwa wamoja hivi hivi, tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna nguvu kubwa kama ya Umma.
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.

KUHUSU UKUTA .

Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo ,Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .

Wasuluhishi wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. Mtu mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .

POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutaoambana nao mmoja mmoja, hatutahangaika na jeshi tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . Ni bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.

Tabia za baadhi ya viongozi ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki za kidemokrasia .

Tujitokeze kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu . Tuna chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni.

facebook wall..

View attachment 386975
View attachment 386976
View attachment 386977
1472046119914.jpg
1472046135736.jpg
 
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi

Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Leo wamekubali
 
Huyu mzee hatari sana, kumbe hajui kipindi cha kuchukua fomu hali haikuwa namna hii, anatutia moyo kama alivyosema, pigeni kura muondeke, zoezi la kuhesabu niachieni mimi! Leo, yakowapi? Eti tutawalinda, mna dhana gani ya kuwalinda watz? Icc ni matokeo ya watu kupukutika acheni ujinga, hurumieni watanzania wenzetu! Mwenye nguvu mpishe!
 
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi

Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Leo wamekubali
Hapa ndio kuna umuhimu kwa Jeshi letu kuachana na siasa
 
Back
Top Bottom