Edward Lowassa: Tatizo ni uwaziri mkuu (tafadhari isome hii)

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete anagombea Urais ilijulikana wazi kuwa kama angepata Urais basi Lowassa Ngoyai Edward angekuwa Wazir Mkuu- "YAKATIMIA"

Au kama Prof Mark Mwandosya angepata Urais basi Dr Harrison Mwakyembe angeukwaa Uwazir mkuu- "HAYAKUTIMIA"

Ili kutihibitisha hili- Wakati Dr Harrison anakabidhiwa jukumu la kuifatilia sakata lile mpaka tupo njia panda (Richmond) alimwambia Lowasa ajitetee- na Mkuu huyu wakati anajitetea alisema " TATIZO NI HUU UWAZIRI MKUU"

Hii ni kumaanisha kuwa ilikuwa ni Vita ya Madaraka ya Utendaji mkuu kabisa wa serikali na Lowasa alijiona anaonewa WIVU.

UHALISIA......
Kumekuwa na dhana kwa baadhi ya watu kuwa Lowasa ndie suluhisho la MATATIZO ya WATZ na ni mtu mwenye MAAMUZI MAGUMU
KULIKO KIONGOZI YEYOTE!!

DR MWAKYEMBE kakabidhiwa Rungu (UWAZIRI KAMILI) anaonyesha uwezo wake wa utendaji kazi kwa kufanya kile kilichokuwa kinafichwa kwa kuwekwa chini ya fulani.

JE HATUJIONI KUWA SASA NI MUDA MUAFAKA WA KUAMINI NCHI HII INAVIONGOZI WENGI MAHIRI NA WENYE MAAMUZI YENYE TIJA KWA TAIFA NA madailiko hayaletwi na mtu mmoja tu ni SISI SOTE NDIO TUTAIBADLISHA TZ pia yatupasa tubadilishe ule msimamo MGANDO uliopo na FIKRA zetu zilizopo kwenyekijichupa cha MUCOLYNE kuwa Suluhisho ni huyo jamaa - Lowasa..........!!?
 
Tatizo ccm imewapaka kinyesi wengi hata wazuri wanaonekana wana harufu ya kinyesi
 
  • Thanks
Reactions: UKI
Sijawai kuona mtu anayeumwa akapewa sumu heti nidawa. Huyo ni FISADI hatuwezi kumpa mgonjwa wetu katu
 
Aliyekuambia suruhisho ni Lowasa ni nani? usitake kututoa kwenye mstari, suruhisho letu ni kuiondoa CCM Madarakani period. pumba zako peleka lumumba au chamwino
 
Dr H Mwakyembe unaweza kumweka katika kundi la mawaziri wachapa kazi tatizo muda wake wa kuishi hapa dunia unawezakuwa umekaribia sana.Mungu akimsaidia akampatia walau miaka mitano si vibaya sana.
 
utakua umetumwa sio bure hivi EL huwa anawalipa shiling ngapi tena kwenye kumnadi?

Soma thread vizuri, inaelekea hujamuelewa kabisa Mwea. Mleta mada anawapinga watu wanomtetea EL kuwa ni mchapa kazi na mwenye maamuzi magumu. Ametoa mfano wa Mwakyembe kuwa nae ni jembe na si lazima awe huyo EL pekee.
 
gamba gamba tu jamani,hata ulichemshe haliivi.hao wote hawana jipya labda wavue magamba yao
 
Back
Top Bottom