Mwembebasha
JF-Expert Member
- Dec 27, 2013
- 1,425
- 405
Mafisadi wajiandaa kuchafua Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake: Taarifa tulizozipata zisizotiliwa shaka ,Ni kwamba Genge la Mafisadi likiongozwa na baadhi ya wahariri na kijana mmoja Mwenye asili ya Kisomali anayetoka kanda ya Ziwa,limejipanga kwa vita ya kuanza kuwachafua, baadhi ya viongozi wa chama na waasisi wa Taifa hili ikiwemo Familia ya mwalimu Nyerere.
Mkakati huo ni mahususi kwa ajili ya kuhakikisha kila anayejiandaa kuchukua fomu kupambana na mgombea wao anachafuliwa kama alivyochafuka Mzee wao anayetaka Urais kwa udi na uvumba.Baadhi ya vijana hao wamepanga kuendesha mkakati huo kupitia Mitandaoni na baadhi ya Wahariri,akiwemo Mhariri aliyeshambuliwa miaka miwili iliyopita na kwenda kutibiwa Afrika kusini.
Wataanza kuendesha mkakati huo kuanzia Jumatatu hii kwa kutumia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na mafisadi hao. Hasira hizo zimekuja baada ya JK kutamka CCM haitompitisha mgombea yeyote mwenye doa,hii ni hatari sana!
Nawasilisha,
UKANA SHILUNGO.
kaazi imeanza. huyo kijana wa kisomali bila shaka ni Hussein Bashe na huyo mhariri ni Absalom Kibanda