Edward Lowassa ni mtu mwenye maono, uthubutu na misimamo, anafaa kuwa Rais ajaye wa Tanzania, Mungu akutangulie, akulinde na akupiganie

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,589
4,599
Awali ya yote napenda kukiri kwamba sijatumwa wala kutumika na yeyote kuandika juu ya hii mada, ni maoni na mtazamo wangu binafsi na pengine ni mtazamo wa wengine wengi wanaomtazama Lowassa kama ninavyomtazama mimi.

Katika ulimwengu wa siasa, jambo dogo linaweza kujadiliwa kwa marefu na mapana kufikia hitimisho. Binafsi ninaamini baada ya Rais Magufuli kukubalika, kupendwa na kuheshimika ndani na nje ya CCM kwa sasa, anayefuata ni Mzee Lowassa.

Nini kinachombeba Lowassa?
Kila jambo linalotokea katika ulimwengu huu lina sababu zake lakini naamini za wengi kuendelea kumpenda na kumuheshimu Lowassa ni historia yake.

Lowassa ana historia ya upambanaji mkubwa dhidi ya udhalimu na unyonyaji, historia ambaye ni kumbukumbu iliyoacha alama katika uongozi wake alipokuwa katika nafasi mbalimbali kama waziri na hatimaye waziri mkuu. Mchango wa Lowassa kwa taifa hili si wa kubezwa ni wa kukumbukwa na kuenziwa na hili nafikiri ndio sababu ya watu kumpenda na kumuheshimu sana.

Historia ya uchapakazi, tangu akiwa waziri na hatimaye waziri mkuu Lowassa amekuwa mstari wa mbele kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa. Wawili hawa, Rais Magufuli na Mzee Lowassa wana historia zinazofanana katika uchapakazi na kuchukia uzembe. Sifa hii ya uchapakazi imesaidia taifa hili kufanikisha mambo mengi na machache ya kukumbukwa wakati wa uongozi wa mzee Lowassa kama waziri mkuu ni ujenzi wa shule za kata na chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kwa muda mfupi.

Lowassa ni mtu mwenye maono kama alivyo Rais Magufuli, sera kuu ya Rais Magufuli kwenye kampeni za 2015 ilikuwa ni Tanzania ya viwanda kwa lengo la kuiwezesha nchi kuwa na uhuru wa kiuchumi na kuwa uwezo wa kujitemea na sera kuu ya Lowassa kwa wakati huo ilikuwa ni Elimu kwa lengo wa kuwawezesha watu kuwa na uhuru wa fikra. Wote wana maono makubwa sana na wote wanaamini katika Tanzania huru na uhuru wa kiuchumi na kifikra.

Kwanini Lowassa anafaa?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ‘mnapochagua mtu chagueni mtu aliyebeba matarajio ya wananchi hasa matarajio yakow ewe mpigakura’. Ninaamini kwamba kiongozi yeyote mwenye maono, uthubutu na misimamo kabeba matarajio yetu sisi wananchi anafaa baada ya Rais Magufuli.

Lowassa anayaishi maneno ya Mwalimu juu ya kudumisha amani. Katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru Lowassa amenukuliwa akimnukuu Mwalimu na alisema “ akitokea mtu jeuri na fedhuli na akawaambia mna nini watanzania? Mjibu hivi’ mwambie tuna amani”. Tumeadhimisha miaka 58 ya uhuru wetu kutokana kwa kuwepo kwa amani, na yeyote anayejali na kuheshimu amani kutoka moyoni anafaa kuwa Rais ajaye

Mwalimu nyerere aliwahi kutaja sifa za mgombea urais kupitia CCM, sifa hizo ni: anatakiwa kuwa mtu anayechukia rushwa ,udini na ukabila kwa dhati ya moyo wake na pia anatakiwa kuwa mtu anayejali maskini na wanyonge kwa kuwa nchi yetu ni ya masikini. Binafsi ninaamini Mzee Lowassa anazo sifa hizo.

Hitimisho
CCM ndipo matarajio, Imani na matumaini ya watanzania ilipo chini ya uongozi thabiti ya mwenyekiti wake Dkt. Magufuli, tunaiombe na kumuombea busara na hekima zaidi ya kuongoza nchi yetu. Pia, mzee Lowassa tunakuombea Mungu akutangulie, akulinde na akusimamie.
 
Mmeona jiwe hana mvuto na ameanza kuogopa hicho cheo baada ya kukuza deni la taifa na sasa anaogopa yajayo, mnatafuta mtu wa kumpa mkidhani anakubalika na wote. Huyo mzee sio mwanasiasa bali ni tapeli la siasa lililoukwaa utajiri kupitia siasa.
 
sioni sehemu yoyote ambayo jamaa anafaa.
lakini alishasema akishindwa urais basi ataenda kuchunga ng'ombe huu ndio muda wake wa kuchunga.
lakini jamaa hahaminiki kabisa ni mroho wa madaraka sana huyo mmasai kwa ujumla hafai na zama zake zimepita hana nafasi kabsa katika siasa za sasa zinazokataa ufisadi.
 
KARLO MWILAPWA,
I beg to differ. Edo hafai hata kwa chembe kuwa Raisi wa JMT maana hana msimamo. Kitendo cha kudefect akaenda kwa adui halafu akarudi kwa kisingizio cha kurudi nyumbani kinampunguzia sana heshima. Edo maisha yake ni CCM na vyote alivyonavyo ni CCM. Alitakiwa kuwa loyal kwa chama chake hata kama kaumizwa roho namna gani. OK alivyodefect angekaa na huo uamuzi labda tungemfikiria. Kitendo cha kurudi kinaonyesha hana maamuzi thabiti. Alitakiwa kubaki CCM.
 
Mmeona jiwe hana mvuto na ameanza kuogopa hicho cheo baada ya kukuza deni la taifa na sasa anaogopa yajayo, mnatafuta mtu wa kumpa mkidhani anakubalika na wote. Huyo mzee sio mwanasiasa bali ni tapeli la siasa lililoukwaa utajiri kupitia siasa.
Aliyepo sasa atakaa miaka 10 na 2020 tutathibisha maneno unayosema kuwa hana mvuto baada ya kushinda kwa zaidi 90%. Hapa tunaangalia Rais wa 2025
 
Aliyepo sasa atakaa miaka 10 na 2020 tutathibisha maneno unayosema kuwa hana mvuto baada ya kushinda kwa zaidi 90%. Hapa tunaangalia Rais wa 2025

Hana uwezo wa kushinda kwa 90% kwa kura halali, bali anaweza kutangazwa mshindi kwa asilimia hata zaidi ya hizo, kwakuwa kiongozi yoyote dictator hutumia madaraka yake kujitangaza mshindi katika uchaguzi.
 
[QUOTE="KARLO MWILAPWA, Watanzania kwa unafiki ni balaa, Lowassa huyu huyu mlìyemkata jina, akaenda Upinzani mkamwita kila aina ya majina mpaka Marehemu eti leo ana maono watanzania ,ndio maana Mwanaharakati Huru Musiba alisema kuwa CCM ni lazima uwe na PHD ya Unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hana uwezo wa kushinda kwa 90% kwa kura halali, bali anaweza kutangazwa mshindi kwa asilimia hata zaidi ya hizo, kwakuwa kiongozi yoyote dictator hutumia madaraka yake kujitangaza mshindi katika uchaguzi.
Huo mchezo CCM hatuna ,hiyo ni michezo ya Maalim seif ya kujitangaza anapoona kashindwa.
 
Mwalimu Mwilapwa!ninachokiona hapa ni kuwa!kwanza unamtabiria kifo mzee wa watu!huo ni uchuro!!nasema hivyo kwasabb kwa kipindi cha miaka minne ambayo ametawala jpm tumeona vifo vya wanasiasa wakongwe nchini(mungai,mzee kingunge,masaburi na wengine wengi),matajiri na wafanya biashara kina Mufruki,mengi na ruge!na wengine wengi watafuata!!SASA NAONA ZAMU YA KUMTANGULIZA EL IMEFIKA!SIELEWI KAWAFANYA NINI HADI MMALIZE!!KUMBUKA PIA APSON MWANGONDA MMEMALIZA KIMYA KIMYA!!!!!Mwacheni mzee wa watu!!!
 
Aliulizwa Kapilimba wakati bado yupo TISS kuhusu kuletwa kwa lowassa 2020 ili awe Rais alichojibu ni kwamba lowassa hawezi kushinda labda waibe kura. alienda mbali na kuwataja watu wenye ushawishi wa kushinda kuwa ni Lissu na Zitto au January Makamba na Membe. wote mliona walivyo na wanavyoshugulikiwa. so inawezekana ili wazo Magufuli bado analo.
 
Back
Top Bottom