Edward Lowassa na mzee Mwinyi wakutana kwenye msiba kwa Sheikh mkuu, Kinana na Gharib Bilal pia wahudhuria

Msiba ulikuwa mtaa ufipa Jana karibu na makao makuu ya chadema


Ova
 
View attachment 592029
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwenye awamu ya nne, Edward Lowassa walipohudhuria msiba wa kaka yake Mufti mkuu wa Tanzania, Sheikh Saad Zuber.

View attachment 592038

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa, pamoja na aliyekuwa makamu wa Rais kwenye serikali ya awamu ya nne, Mohammed Bilal pamoja na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakiwa nyumbani kwa Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakary Zubeiry bin Ally, Kinondoni, Dar es Salaam, kushiriki msiba wa kaka yake Mufti Zubeir, aitwae Sheikh Saad Zuber, uliotokea jana jioni.​

Hivi Mzee Lowassa huko CHADEMA aliko hafanyi ' Kazi Maalum ' kama ile aliyokuwa akiifanya Profesa Mruma katika Makinikia na Madini yetu?

Nitashukuru sana nikijibuwa nanyi ' Wajuvi ' wa Kutukuka wa haya mambo.
 
Lowasa sasa busara ndio zinaanza kumwingia.Huko nyuma alikuwa sifuri.Toka mwanzo alitakiwa awe karibu na sheikh mkuu wa Bakwata na kardinali Pengo sababu hao watu wawili ndio wenye wapiga kura wengi wa dini zao wanaowaongoza waliomo vikao vya uteuzi na kura ndani ya vikao vya CCM VYA KUCHUJA majina NA NDIO WENYE wapiga kura wengi nchini.Lowasa hakujali akaamua kwenda kuungana na mujahidina akina sheikh Katimba ambao kutwa kazi yao kutukana BAKWATA!!! Pia akaenda kuungana na ASKOFU Gwajima ambaye kutwa kazi yake kutukana kardinali Pengo!!!! HIVYO kwa muungano huo kweli alitarajia CCM WANGEMPITISHA kugombea uraisi na angeweza kushinda uraisi? Angekuwa na busara kipindi kile alitakiwa awe karibu na huyo mzee wa bakwata na pengo.Lakini lowasa hajawahi kaa karibu na kiongozi mkuu wa BAKWATA wala PENGO alikuwa kazi yake kuruka ruka na akina GWAJIMA na akina Sheikh katimba AMBAO HAWANA watu kwenye vyombo vya maamuzi!!!

Anyway naona busara zinamrudia taratibu.Ila kukaa karibu na BAKWATA hakuwafurahishi akina sheikh Katimba na akina SEIF SHARIFF HAMAD wenye imani za kijahidina.
Kwa hiyo ndio sababu ya kumkata jina lake? tulikuwa hatujui
 
Kinana kwengine anaonekana, ila Ofisini haonekani, haiti press kama Katibu wa Chama kutoa ufafanusi wa mambo mbalimbali na kuonesha sapoti ya Chama kwa serikali. Hajawahi kupokea wageni wa Chama, wanapokelewa na Naibu wake au Polepole. Yeye ni Katibu Mkuu wa Chama kwa nini anakuwa hivyo? Polepole ndio amekuwa kama Katibu.
Mashinji hajaonekana Nairobi kumjulia hali kamanda Lisu hadi leo.
 
Back
Top Bottom