Edward Lowassa na Dr Wilbrod Slaa: Kosa la propaganda za CCM za Ukanda na Udini.

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,619
2,000
Wanajamvi

Watu hawa wawili wenye nguvu ktk siasa hapa nchini wanatoka ukanda wa Manyara kaskazini mwa Tanzania.

Jimbo la Karatu anapotokea Dr Slaa na Monduli anapotokea Lowassa yamepakana na yapo mbali na himaya za kichaga zilipo mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa vyovyote vile ukizungumzia mbio za urais wa nchi hii usipoyataja haya majina ya watu hawa wa KASKAZINI utakuwa sio mtanzania wa kawaida kwani inaaminika kuwa kila mmoja wao anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na vyama vya CHADEMA na CCM ktk uwakilishi wa ngazi ya Urais hapa nchini.

MAJINA HAYA MAWILI yanabebwa na propaganda chafu ya chama cha mapinduzi ya UKANDA na Udini hasa kwa Dr Slaa ambaye wachambuzi huru wa kisiasa wanadai kuwa PROPAGANDA YA UKABILA imemuweka juu kisiasa.

Propaganda ya Ukanda imeendelea kukididimiza chama cha mapinduzi hapa nchini hasa kwa kulenga ubaguzi hatua ambayo wanaokereka nayo wanaeleza kuwa ama DR SLAA ama LOWASSA ambayo ni miamba ya kaskazini.


ITAENDELEA..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom