Edward Lowassa: Bora kuwa na Rais kama Kagame ili tuendelee

Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama Kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....Kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora Lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na Rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au Lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama PM, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....Nadhani tunahitaji rais kama Lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.
Hii bora huyu kuliko huyu haisaidii, watanzania tupo 50milion ndani yake wapo watu wazuri wa kuongoza nchi achana na hii bora bora yako hapa
 
Wiki hili naona watu wamelipwa hapa JF wanachotaka Lowassa agombee Urais wapinzani hasa CDM wamuweke Dr Slaa au yeyote na ukweli atapita kiulaini na kumuacha mbali Lowassa.
wengine hamumfahamu E.L. wanataka kumfananisha na Pinda yaani bora kumfananisha na Kagame kwa sababu wale tuliokuwa PMO baada ya SUMAYE ndio mngetuuliza yaliyotukuta, mpaka mpishi wa Ikulu ya PM (mama MG) alifukuzwa akawekwa wa kwake bado ma Bodyguard waliwekwa wapya na wakatengeneza vyumba vyao mpaka na bathtube mpya vifaa hivyo havijalipwa hadi leo.
Mngewauliza wafanyakazi wa Ofisi hizo sio kujisemea tu, km ni mbinu subirini Mkutano Mkuu ndio mtajua watu wamejipanga vipi na Uchaguzi wa 2015
 
Tusirudie makosa tena, tuweke vigezo vya mtu amefanya nini.

Lowasa namkubali, ndani ya miaka miwili alifanya kazi kubwa na kuisimamia.

1. Aliweza kufuatilia mkataba uliotuzuia kutumia maji ya ziwa Victoria uliowekwa mwaka ...... na ukatenguliwa. leo
watu wa Shinyanga wanatumia maji bwerere.
2. Aliweza kusimamia uanzishwaji wa shule za kata,natumaini angewezesha hata walimu kuwepo ktk shule hizo.
3.

Ungekuwa umefanya vema kama ungeainisha pia mabaya aliyowahi kuyafanya ili tuone yapi yanampa advantage ya kumfikiria kuwa kiongozi mzuri au la
 
Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama Kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....

Kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora Lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na Rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au Lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama PM, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....

Nadhani tunahitaji rais kama Lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.
Wewe mleta mada unamjua Kagame au unamsikia, kwanza huyo Lowasa hajui Kagame ninani ndio maana anakurupuka tuu!!! Kwa Mhe Paulo Kagame Rwanda Lowasa asingepata muda wa kupiga kelele akiwa huru, yeye atakuwa mtu wa kwanza kwenda jela kama alivyosema Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa!!! Kwa Rwanda Lowasa sio raia huru ni mfungwa au ameisha fia jela, wacha kutetea ufisadi wewe mwambie angoje zamu yake ya kwenda lupango!!!! Kujikosha aanze kurudisha fedha zetu huko Uswizz, na majumba ya London Trafagher squere, Leicester aanze kuyauza arudishe fedha zetu zikomboe wamasai wanao teseka kwenye lindi la umaskini anaowadanganya kila kukicha!!!

Mkuu hali ndo hii.
Sitambuliki kwa sababu nilifanya katika ngazi ya kijiji lakiniingekuwa position kama yake ingekuwa 3 times E.L. Tafuta watu wenye muono mpya. Ataingia kwa ajili ya visasi na kusulubu wengine.

CCM atafute mtu ambaye watu hawazanii ili kuleta hamasa mpya si hawa wasio na kitu kipya.
Mkuu umelogewa CCM nini nje ya CCM kuna watu bora kabisa wasio na kashifa za wizi na ufisadi, CCM ni chaka la wezi hukuna zaidi tuachane nao!!!!

sidhani kama kulishawai onekana rais dictator tz kama nyerere,...si uliona tulivyokuwa tumefumbwa midomo....chadema wangekuwa huru kama hivi leo kama nyerere angekuwa rais au kipindi kile wangefanya hivi? tulikuwa tumefumbwa midomo tukawa mambumbumbu sukuma twende na hakuna maendeleo wala nini...akili ya nyerere peke yake ndo ilikuwa inaongoza nchi, ndio maana kwasababu kwenye akili yake aliamini ujamaa basi na akili za wabongo zikaelekea kwenye ujamaa tukabaki tumepoa na masikini hadi leo.....yaani hapa tulipofikia ni matokeo ya kuongozwa na akili ya mtu mmoja ambaye hapati challenge yeyote ile.

Yeye aanachokiamini ndicho mnachokifuata hakuna wa kumpinga hata kama anakosea....sasa sijui kipi utamsifia nyerere kama si amani peke yake? kama ni maendeleo.....hata wenzie walioanza naye kutafuta uhuru nchi zao zimeendelea kuliko tz.....jaribu kutathmini miaka ile miwili Lowasa aliyofanya kazi kama angefanya vile hadi leo hii tungekuwa katika hatua gani?...pia, kama tunasema ameiba, ameiba nini? prove it....pia hakufukuzwa aliachia ngazi...hahaha....zamani ukiangalia kwenye post zangu zote nilikuwa nampinga hadi kumtukana Lowasa, lakini imefika kipindi nimeona yeye ndo anayetufaa kuliko kuwa na dhaifu...imajini...kama kikwete anapoondoka akamuweka rais awe Asha rose mingiro...aliyepoa kam maji ya kwenye mtungu?...

labda amuweke mama tibaijuka....kidogo inakuja....kwa wengine wote wanaccm waliobaki, no one to match Lowasa...hakuna mtu anayeweza kuiongoza hii nchi kama lowasa ndani ya ccm..labda atoe chadema na si ssm....ccm yupo lowasa peke yake...wengine wote masifuri.
Mkuu vipi umelogewa CCM nini watu wako wote ni CCM kwani wao wamenunu Watanzania kama watumwa hatuwezi kujiamulia mustakabali wetu???? Tanzania inahitaji kiongozi dynamic well prepared, full of zeal to unblock or salvage our state from this demon CCM and its rhetoric members the like of Lowasa!!! Huyo jamaa ni mwizi saana tutoke kwenyi ufisadi tuingie sijui kwa lugha gani kuelezea uozo au uvundo wa mafisadi!!!Mkuu achana na CCM tupate the new cream kuokoa nchi yetu bwana!!!

Mkuu umelogewa CCM nini nje ya CCM kuna watu bora kabisa wasio na kashifa za wizi na ufisadi, CCM ni chaka la wezi hukuna zaidi tuachane nao!!!!

haa haaaaaaa!!!!!!!!!!!!! Mkuuu siko hivyo na sina chembe ya uccm. Me naheshimu maoni ya watu wote na natakiwa kutoa elimu kwa yeyote juu ya msimamo wangu kinagaubaga katika kila mada.

Kwa ujumla ccm na mazalia yake lazima watokomezwe.

Nashukru.
 
UPUUZI UPUUZI UPUUZI
hivi leo ndotunaona chadema wanafaa? kwanini basi hatukuwachagua? badala yake tukawarudisha mafisadi madarakani. mnajidai kuisifia chadema mkifika kwenye masanduku yakupigia kura mnaichagua CCM huo ni unafki na uzandiki. shame on you all
 
Mimi nakaa mbali sana kutoka nilikojiandikisha kupiga kura, kitendo cha EL kuchukua fomu ya urais kitanifanya niandae nauli ya kurudi kwetu kupiga kura ya kumkataa kwani kutopiga kura kutasababisha fisadi mkuu na baba wa mafisadi aingie ikulu.
 
Kaniki itabaki kuwa kaniki tu haitakati hata uoshe na jiki, Lowasa ni Kaniki Hatakati
 
mkuu uko sawa kabisa ila soma historia vizuri,hata nchi kama SOVIET UNION(USSR)iliongozwa na JOSEPH STALIN tena alikuwa mbaya kuliko hata NYERERE,mfano mwingine CHINA iliongozwa kidikteta sana hata mauaji ya wanasiasa yalikuwa makubwa sana ila leo hii CHINA is among the world greatest super powers,tofauti nihii mkuu nchizilizotawaliwa zote zilikuwa hazina wasomi wa kutosha kuweza kufanya maamuzi mazuri kwa taifa,pili kipindi kile pia NYERERE na viongozi wengi walikuwa wanahofia COLD-WAR intervention since SPIES toka WESTERN STATES WALIWATUMIA wazawa wa nchi mbalimabali kuleta political instabilities na kufanya sabotage ndo maana CHINA pamoja na nchi nyingi zilifanya rapid reforms after the end of the cold-war since suspicion ilipungua.Lowassa kuongoe hivyohajakosea kabisa ila is he a person we can really bet our lives on?kumbuka nchi kama hii wasomo walikuwa ni wachache na in democracy everybody makes decisions for the state ila areyou willing to sell your rights to the illiterates just because they are many?basically that won't be democracy but hipocrisy.KAGAME is a patriot to his people only,worse enough he is terrible vessel WESTERN INFLUENCE in AFRICA. POST AFRICAN leaders were the policy makers at least they restricted some western interference within their statesm but most of our current leaders are pro-western and hypocrits,LOWASSA is a good leader but his deeds and greedy stained his political charisma,so we should be carefwe site examples and KAGAME SHOULDN'T BE OUR ROLE MODEL since he hates AFRICANS particulary the congolese.
 
Wiki hili naona watu wamelipwa hapa JF wanachotaka Lowassa agombee Urais wapinzani hasa CDM wamuweke Dr Slaa au yeyote na ukweli atapita kiulaini na kumuacha mbali Lowassa.
wengine hamumfahamu E.L. wanataka kumfananisha na Pinda yaani bora kumfananisha na Kagame kwa sababu wale tuliokuwa PMO baada ya SUMAYE ndio mngetuuliza yaliyotukuta, mpaka mpishi wa Ikulu ya PM (mama MG) alifukuzwa akawekwa wa kwake bado ma Bodyguard waliwekwa wapya na wakatengeneza vyumba vyao mpaka na bathtube mpya vifaa hivyo havijalipwa hadi leo.
Mngewauliza wafanyakazi wa Ofisi hizo sio kujisemea tu, km ni mbinu subirini Mkutano Mkuu ndio mtajua watu wamejipanga vipi na Uchaguzi wa 2015
Ikulu ya PM!? Ikulu ya PM ndio iko wapi mkuu?
 
Lowasa ana hoja ya msingi kuhusu kufnya maamuzi hasa magumu especially kwa faida ya taifa, ili ndilo tatizo la serikali yetu haitaki kuamua ili hisionekane mbaya machoni kwa watu kuna mambo yanaachwa yajiendee tuu...mipango mingine inahitaji kuamua tuu, mfano tuliamua kuwa na shule za kata kwenye kila kata na tumeweza bila kujali kasoro zake, sasa ndo tungedili na kasoro zake then tuamie project ningine hata ikibidi kubana mikanda....tatizo ni udhaifu wa serikali ndo message aliyoitoa Lowasa kwa kutumia reference ya KAGAME.
 
Hivi Lowasa anajiona amekwisha kwepa kushtakiwa kutokana na kashfa zake, iwapo nchi hii itapata rahisi kama kagame atapona lazima wote walioiba na kulisababishia hasara taifa lazima wafungwe(Lowasa, Chenge, maige, Karamagi) na wengineo
 
sidhani kama kulishawai onekana rais dictator tz kama nyerere,...si uliona tulivyokuwa tumefumbwa midomo....chadema wangekuwa huru kama hivi leo kama nyerere angekuwa rais au kipindi kile wangefanya hivi? tulikuwa tumefumbwa midomo tukawa mambumbumbu sukuma twende na hakuna maendeleo wala nini...akili ya nyerere peke yake ndo ilikuwa inaongoza nchi, ndio maana kwasababu kwenye akili yake aliamini ujamaa basi na akili za wabongo zikaelekea kwenye ujamaa tukabaki tumepoa na masikini hadi leo.....yaani hapa tulipofikia ni matokeo ya kuongozwa na akili ya mtu mmoja ambaye hapati challenge yeyote ile.

Yeye aanachokiamini ndicho mnachokifuata hakuna wa kumpinga hata kama anakosea....sasa sijui kipi utamsifia nyerere kama si amani peke yake? kama ni maendeleo.....hata wenzie walioanza naye kutafuta uhuru nchi zao zimeendelea kuliko tz.....jaribu kutathmini miaka ile miwili Lowasa aliyofanya kazi kama angefanya vile hadi leo hii tungekuwa katika hatua gani?...pia, kama tunasema ameiba, ameiba nini? prove it....pia hakufukuzwa aliachia ngazi...hahaha....zamani ukiangalia kwenye post zangu zote nilikuwa nampinga hadi kumtukana Lowasa, lakini imefika kipindi nimeona yeye ndo anayetufaa kuliko kuwa na dhaifu...imajini...kama kikwete anapoondoka akamuweka rais awe Asha rose mingiro...aliyepoa kam maji ya kwenye mtungu?...

labda amuweke mama tibaijuka....kidogo inakuja....kwa wengine wote wanaccm waliobaki, no one to match Lowasa...hakuna mtu anayeweza kuiongoza hii nchi kama lowasa ndani ya ccm..labda atoe chadema na si ssm....ccm yupo lowasa peke yake...wengine wote masifuri.
Mkuu Lowasa kesha kunasa nini? mbona huko kuna akina magufuli na akina mwakyembe. lakini nao wakitaka kuendelea kutoa mchango kwa taifa hili lazima wahamie M4C. Vinginevyo wajiandae kutupisha.
 
CCM iliharibika yote baada ya kutelekeza azimio la Arusha. Wote kwa pamoja walikubaliana kuiba kila kilicho mbele yao bila kujali impact kwa taifa ndio maana unaona kila mmoja wao analalama kama wanaendeshwa na robot! Wabunge, mawaziri mpaka PM analalama hii yote nikwasababu wanajua kuwa walikubaliana kuiba na sasa kila mmoja anatekeleza makubaliano yao. Kuanzia kwenye nishat, madini mpaka wanyama pori nikuiba kwa kadri nafasi inavyopatikani.
 
Binafsi huku serikalini kwa sasa tunahitaji mtu mweye akili kama lowassa. kipindi chake ukisikia anakuja jamaa watu wanajituma hakuna mfano, sasa hivi serikalini kama shamba la bibi vile.
 
Hivi Lowasa anajiona amekwisha kwepa kushtakiwa kutokana na kashfa zake, iwapo nchi hii itapata rahisi kama kagame atapona lazima wote walioiba na kulisababishia hasara taifa lazima wafungwe(Lowasa, Chenge, maige, Karamagi) na wengineo
Mwizi nambari wanu ni kijana anayejiita ezekiel maige. Nashangaa ameachwa anarandaranda mitaani wakati amejilimbikizia mali kibao ikiwa ni pamoja na majumba ya kifahari na malori ya kusafirisha mizigo kwenda nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom