Edward Lowassa: Bora kuwa na Rais kama Kagame ili tuendelee

Kumbe upo kazini! Unataka kutuhadaa huku we umepewa hela kumsafisha haaa leo umetukosa mwambie hatuendi chooni leo...hatuhitaji kuona toilet paper
 
Safi lowassa tunatumaini utayatekeleza hayo utakapoapishwa kuwa prezidaaa wa Tz 2015
 
Daah yani huyu jamaa kila siku anampiga vijembe jk
 
wakati akiongea, nilimsikia akimsifia kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama pm, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....nadhani tunahitaji rais kama lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.

he is not the right person
 
Anaposema bora Kagame ni kwamba hana hisia yoyote kwamba MKUKI KWA NGURUWE MCHUNGU. Unaposema bora kuwa kama Kagame ni kwamba hutaki huo uhuru wa kusema bora Kagame
 
Lowassa ni mpuuzi. Hatuwezi kuendelea kwa kuigiza watu wengine tena madikteta. Heri kuwa Nyerere ili tuendelee kuliko Kagame ambaye ni dikiteta anayenuka na mwizi kama Lowassa. Tanzania hatuhitaji tena kiongozi asiyejiamini. Kwanini rais wa Tanzania asiwe Lowassa au Father of All badala ya Kagame? Ni upuuzi kwa mtu mwenye kivuli kujigeuza kivuli cha mwingine wakati anacho kivuli. Shame on Lowassa mwizi anayepokea pesa ya kustaafu wakati alitimliwa.

father of all,saizi naweza amini kuwa unakazi maluum humu ndani ya kumpigia membe kampeni,yani kama unashndwa kukubaliana na hoja ya kagame kuwa kiongozi bora kisa tu kaongea lowasa,ebu jamani tuweni helenics,hata kwetu kiongoz wa mfano ni kagame africa mh.mbowe anasemaga rwanda kama mfano wa kuigwa,tatizo lenu munataka aje dhaifu kama huyu aliopo eti membe,membe kuwa rais bora jk aendlee,ni dhaifu muno na muno,we need slaa,lowasa,magufuli,mbowe wenye element za uongozi kama kiongozi na sii kujichekesha chekesha.
 
E.L. hafai hata kama amefanya kazi nyingi za umma. Hata mimi nafaa kwa vile nilifanya kazi za maendeleo kijijini kwetu? Yale ni majukumu 2.
 
siku ile mwaka 2005 mkutano mkuu wa ccm uliompitisha kikwete kuwa mgombea wa urais nililia machozi kwa sababu nilijua kwamba tunaelekea kupata rais dhaifu of all time. nililia kwa sababu nilikumbuka maneno ya mwalimu kwamba siku ccm watakapomtaja mgombea wao wa urais huenda ndio watakuwa wamemtaja rais. baadhi ya rafiki zangu walinishangaa niliposema kikwete hafai. hatimaye watanzania walimchagua msanii huyu kwa kishindo kuwa rais. the rest is history. jamani tuache ushabiki ktk suala sensitive km hili.
 
Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora Lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na Rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au Lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama PM, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....nadhani tunahitaji rais kama Lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.

Tatizo la lowassa ni afya yake ukiacha utajiri wake ambao hauna maelezo ya jinsi ulivyotatikana,kwani ukiacha urithi ng'ombe alizoachiwa na baba yake hakuachiwa hata baiskeli ya miguu mitatu..ni hayo tu ndio yaliyofanya watanzania wamtapike

Huyu ndio Lowassa mtaka urais kwa nguvu...soma documents zifuatazo then upime kama bado anakufaa?!!


paperclip.png
Attached Files


 
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo:

"Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma". Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali".

Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.



Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli).
Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?"

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?"

Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.

Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!

Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa "Natural Justice" hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?

Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) " kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena "For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!

There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious" Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.

Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.

Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.

Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.

Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.

Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?

Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo?
Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.

There is also a compelling case that is in Tanzania's self interest.
Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.

Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?

Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.

It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can't, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.
 
Haiba ya MTU inaweza kuwa RIGHT or WRONG!

Haiba ya Rais should and must be RIGHT!

WRONG Character can be either weak or strong ...but all being weak characters.
Can be Wrong strong or wrong weakness!! Can have weak dictator, Can have strong Dictator ..But all of these are Weak characters.

RIGHT is humanity coupled with FIRMNESS of NOBILITY, KINDNESS AND CREDIBILITY which knows no nonsenses!!

Right Character for presidency IS TOTAL HONEST, LOYALTY, equipped with unwavering humane strength not found in any of corruptions, confusions, meanness and all negative Traits!

ITS a RIGHT STRONG AND AT THE SAME TIME INNOCENT POWER FOR THE GOODNESS OF THE COUNTRY!!

It has no need for giving in to nonsense, of being people pleaser, of being weak and wimpy for the gain of simple popularity ...

The right character, nobility and credibility is what The President of Republic of Tanzania should JUST BE!

Comrade Lowasa good with this? ...go on you tell us!!!
 
Ni kweli, Kagame ni mchapa kazi, anachukua maamuzi magumu na kuyatekeleza, anajali maisha ya wananchi wa kawaida, but I don't think Lowassa has any ground to compare or to be compared with him. Nilikuwa Rwanda kwa miezi sita and saw what Kagame does. Viongozi wengi wa kiafrika, including Lowassa himself have little guts to do what the man does. Wizi wa Lowassa pia unamwondolea credibility kabisa ya kutawala nchi hii. Let him go to hell!
 
Wakati akiongea, nilimsikia akimsifia Kagame, kuwa bora tuwe kaksi kama kagame ili tuendelee, tusiwe legelege, dhaifu dhaifu..tuwe na kiongozi mwenye kuchukua maamuzi magumu kama yana manufaa kwa taifa.....kwa upande fulani...najua jamaa lina kashfa ya richmond,....lakini pamoja na ufisadi wake, nadhani ni bora Lowasa mara mia kuliko rais dhaifu....kuwa na Rais ambaye kidogo ni dictator kama kagame au Lowasa kipindi chake cha miaka miwili kama PM, ni bora mara mia kwasababu tukikumbuka kwa ile 2 years alichachafya wavivu wengi sana na wengine waliacha kazi on da spoti....nadhani tunahitaji rais kama Lowasa.....mfano wa kagame...tukijachagua rais dhaifu tena, tutachezewa ngoma za kikwere na hatutafaidi chochote....zaidi ya migawanyo katika nchi na umasikini.

Haya ni maneno ya kukata tamaa. Unasema ni fisadi lakini unamfananisha na Kagame kama yeye anavyojipambanua. But this is the same guy in the same rotten government system. Tumesikia ahadi zao hewa , tumesikia uove wao wote, na tumeskia mazuiri yao ambayo bila shaka ni kama tone la maji baharini. Tumekuwa nae na tunamfahamu.

Hebu jiulize , ukipewa fursa ya kuoa au kuolewa upya , utamchagua mkeo/mumeo wa zamani au utashawishika kutafuta mpya ambaye unafikri ataendana na matakwa yako?. Halafu si huyo mpya atakuheshimu zaidi ya yule wa kwanza ili ajinusuru na yaliyomkuta wa kwanza? Samahani kwa kutumia mfano huu sina maana nyingine zaidi ya kusema kwa lugha rahisi kwamba Watanzania wanahitaji compelte changes na sio viraka viraka. LOWASA ni kiraka.
 
binafsi namlilia sana lowasa alikuwa kiongozi makini sana wakati akiwa pm, amekuja huyu jamaa wa kulialia hana lolote analolifanya
 
Sijui kwa nini watu
wanamsifu Nyerere kiasi hicho.He had his good and dark sides.Kwa mfano
kwa kiasi fulani alifanikiwa kuleta umoja wa Watanzania ingawa sijui kwa
nia gani.Inawezekana ni katika mkakati ule ule wa serikali moja ya
kishetani ya dunia,which is a bad side.Pia alifanikiwa sana katika kutoa
elimu kwa watanzania bure,again sijui kwa nia gani,one can argue on
negative sides of this endevour.Mbaya sana ni kwamba Nyerere
ali-mismanage uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha juu sana,kwa hili
sitakuja kumsamehe.No, tuliteseka sana,hasa baada ya vita ya kumng'oa
Iddi Amin.

Do you mean angemwachia Idd Amin aichukue Kagera?matokeo ya vita yalileta anguko la uchumi japo kuwa pamoja na sera yake ya ujamaa!
 
Back
Top Bottom