Edward Lowassa ashiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge Mstaafu, Beatrice Shelukindo

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1.jpg

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji walioshiriki maziko ya mbunge wa zamani, Beatrice Shelukindo (58) yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wake katika kata ya Olorien Jijini Arusha jana.

Viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyotanguliwa na ibada ni pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.

Pia maziko hayo yalihudhuriwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Tanga na Arusha, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali.

Ibada ilifanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro ambako Askofu mstaafu, Simon Makundi, alisema Beatrice hakuwa fisadi na alitoa mchango mkubwa kwa familia, dini, taifa na Afrika Mashariki.

“Jiulize wewe una mchango gani hata katika familia yako, dini yako, taifa hili na hata kwa Afrika Mashariki?” Alihoji Makundi.

Aliwataka mamia ya waombolezaji wakipewa nafasi, heshima na vyeo serikalini au katika kampuni yo yote kuitunza heshima hiyo kwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa na hofu ya Mungu.

Beatrice aliyezaliwa mwaka 1958 amefariki akiwa na umri wa miaka 58, jambo ambalo askofu mstaafu alisema hiyo ni neema ya Mungu.

Alisisitiza kuwa Beatrice alifanya kazi za utumishi serikalini na ubunge kwa uadilifu mkubwa na kupata heshima na serikali, dini na jamii na ndiyo maana aliweza kuhitimisha heshima hiyo hadi mwisho. Askofu Makundi alisema alipata bahati ya kuzungumza naye kabla ya mauti.
 
HABARI kuu hapa ni Maziko ya Beatrice (RIP) au mahidhurio ya Lowassa?

Unaonesha unamuota sana huyu Mzee. Au kama walivyo CCM wengi, mnatafuta kiki kupitia kwake!
 
HABARI kuu hapa ni Maziko ya Beatrice (RIP) au mahidhurio ya Lowassa?

Unaonesha unamuota sana huyu Mzee. Au kama walivyo CCM wengi, mnatafuta kiki kupitia kwake!
Kosa langu nini? Nimeichukua kama ilivyo kutoka kwenye social networks, labda hizo social networks ndo zinamuota. Kwangu mimi Lowassa ni sawa na punje ya ulezi.
 
Mungu amrehemu huko alipo. Hivi alikuwa mke wa William Shelukindo aliyewahi kuwa mbunge na mwenyekiti Kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini?
 
Mungu amrehemu huko alipo. Hivi alikuwa mke wa William Shelukindo aliyewahi kuwa mbunge na mwenyekiti Kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini?
Amina, ndiyo alikuwa mke wa mzee Willium Shelukindo. Pia likuwa Team Lowassa mzuri sana, ni miongoni mwa watu 500 waliobisha hodi Monduli kwa Lowassa kumuomba agombee urais. Laigwanani amempoteza mtu muhimu sana.
 
Amina, ndiyo alikuwa mke wa mzee Willium Shelukindo. Pia likuwa Team Lowassa mzuri sana, ni miongoni mwa watu 500 waliobisha hodi Monduli kwa Lowassa kumuomba agombee urais. Laigwanani amempoteza mtu muhimu sana. QUOTE]Mbona Willium Shelukindo alikuwa hamtaki Lowassa na ni mmoja wa wabunge machachari walioshinikiza kamati ya bunge ya uchunguzi wa RITCHMOND iundwe yeye akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini? Inakuwaje watofautiane na mkewe kipenzi?
 
Amina, ndiyo alikuwa mke wa mzee Willium Shelukindo. Pia likuwa Team Lowassa mzuri sana, ni miongoni mwa watu 500 waliobisha hodi Monduli kwa Lowassa kumuomba agombee urais. Laigwanani amempoteza mtu muhimu sana.
Mbona Willium Shelukindo alikuwa hamtaki Lowassa na ni mmoja wa wabunge machachari walioshinikiza kamati ya bunge ya uchunguzi wa RITCHMOND iundwe yeye akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini? Inakuwaje watofautiane na mkewe kipenzi?
 
HABARI kuu hapa ni Maziko ya Beatrice (RIP) au mahidhurio ya Lowassa?

Unaonesha unamuota sana huyu Mzee. Au kama walivyo CCM wengi, mnatafuta kiki kupitia kwake!
Suala la maziko haliwezi kuwa ni habari kuu coz ni tukio la kawaida. Ila hilo tukio la Lowasa kunong'onezana na Ole Sendeka hakika ni habari kuu.
 
Sijaona mafuriko ya Makamanda wakimsindikiza bosi wao tofauti na walivyofanya kule Kilimanjaro mwaka jana
 
Mbona Willium Shelukindo alikuwa hamtaki Lowassa na ni mmoja wa wabunge machachari walioshinikiza kamati ya bunge ya uchunguzi wa RITCHMOND iundwe yeye akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini? Inakuwaje watofautiane na mkewe kipenzi?
Unajua kwanini marehemu amezikwa Arusha kwa wazazi wake na siyo Tanga kwa mumewe?
 
Kosa langu nini? Nimeichukua kama ilivyo kutoka kwenye social networks, labda hizo social networks ndo zinamuota. Kwangu mimi Lowassa ni sawa na punje ya ulezi.

Ha ha ha, Mkuu basi wewe ni mtu Mkubwa sana. Kama EL ni kama punje ya mchele! Alipata asilimia zaidi ya 36 ya kura za watanzania wote, na bado ni kama punje ya mchele kwako? You must be the king of Zamunda.
 
Fisadi yeyote popote alipo, kwangu mimi ni wa aina hiyo, hajalishi amepata kura ngapi , Lowassa hata angechaguliwa kuwa rais, bado angekuwa kama punje ya ulezi.nchi yetu ingekuwa ina aibu kimataifa, wananchi wake tungekuwa tunatembea kwa aibu mbele ya watu wa mataifa mengine kwa kuongozwa na rais FISADI.
 
Back
Top Bottom