Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Baada ya yote yaliyotokea, la msingi ni vyama vya upinzani kujitafakari, kujenga mshikamano kwa wale watakao baki ili kuwe na upinzani imara Tanzania. Kwa hili la Lowasa kuna ambao tulijiuliza huyu mheshimiwa ana simamia nini kitu gani hapo CDM, hadi leo sijapata jibu. Ni wakati wa CDM na washirika wake kujibrand upya kwa maneno na vitendo zidi ya Lichamadola. MUNGU WETU HAJA WAHI KUSHINDWA.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

Rudi nyumbani kumenogaaaa
 
Kwa wana ccm tuwe makini na huyu mtu , tunaweza furahi kumpokea lakini kilichoko kichwani mwake ni siri nzito.

Watu kama hawa sio wa kuchekea chekea hata kidogo ndani ya chama, yawezekana ni mkakati wa siri wa ndugu yetu membe na kundi lake pamoja na lowassa.

Time will tell, nimekaa siti ya mbele huku

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Membe akiwa RAIS we unaumia nn mbona una chuki kama amekuchukulia bwana ako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂😂😂😂💪💪💪😎
Hapana manengelo usimlaumu mzee Lowasa hata kidogo, laiti ingewezekana kufungua yaliyo nyuma ya pazia ungemhurumia mzee wa watu, siasa za afrika ni ngumu sana hususani kwa mtu mzima kama mzee Edo ambae hata hali yake ya afya haiko sawa.
Mimi nampongeza sana mzee kwa kuonyesha uthubutu wake wa kuweza kutoka tu chama tawala na kuhamia upinzani, mzee ni mwanademokrasia wa kweli, amepambana kwa uwezo wake wote ila mazingira yamemuwia vigumu kubaki katika msimamo wake, shinikizo lilikua ni kubwa kuweza kuhimili mikikimikiki aliokua anapitia kutokana tu na kua nje ya ngome kuu, mzee ameamua kustaafu kwa njia hio ili kuamua kuepusha shari.

Maendeleo hayana chama
 
Lowasa, Magufuli na "upotevu" wa trillion zetu ndio CCM hiyo, chama cha MAFISADI PAPA
 
Nadhani Mh. JPM ameshtukia kuhusu possibility ya Lowassa kuungana na Membe upinzani ingekuwa hatariiiiiiii sana kwa CCM, hivyo akamuwahi kumrudisha home kw gharama yoyote ile..!!
Kwa hiyo unafikiri lowassa amenunuliwa? Mnajidanganya hadi mnaamini uongo wenu..ndio yule chizi lissu akamwambia steve sacker wa hardtalk eti wabunge wao wananunuliwa na ccm akidhani anaisema ccm kumbe anakidhalilisha chama chake. Wabunge gani wananunuliwa au wanajiuza kama bidhaa.
 
Back
Top Bottom