Edward Lowassa ampongeza Rais Dr. John Magufuli

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,806
12,221
Waziri Mkuu wa awamu ya 4 Ampongeza Dr. John Magufuli.
Aliyekuwa Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Edward Lowassa ampongeza Rais John Pombe Magufuli kwa hatua aliyoichukuwa ya kusimamia rasilimali za nchi kikamilifu huku akidai kuwa tiba ya matatizo yote hayo ni upatikanaji wa katiba mpya



“Nimpongeze sana Mhe Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi na hatua ambazo amechukua kuhusu jambo hili, na hasa pale anapowashirikisha wananchi, ni jambo muhimu sana.

Maneno hayo yamesema leo na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la mchanga wa madini (makinikia) ambalo limeonyesha kuwa Tanzania impoteza zaidi ya trilioni 100 tangu mwaka 1998 hadi Machi mwaka 2017.

Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alisema anampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA kwani kipindi anazunguka kuomba kura kwa wananchi alipopita maeneo yenye madini aliyazungumza haya yanayotekelezwa leo.

“Nampongeza kwa kutekeleza yale maamuzi ambayo ni ya UKAWA. Nilipokuwa kwenye kampeni ya kuomba kura, hata pale Geita, nilieleza jambo hilo, nikasema hivyo hivyo alivyosema yeye kwamba nikiingia madarakani nitaunda tume ya kuchunguza jambo hili ili mtanzania awe ndiye anapata sehemu kubwa ya faida kuliko mgeni.”

Aidha, Lowassa amesema kuwa, ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na hata yeye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa na na kuzungumza, lakini jambo gumu lilikuwa ni kamba, mikataba ukishaiweka saini inakuwa migumu sana kubadilisha.

Lowassa alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo mirahaba lakini haikutosha.

“Matumaini yangu ‘figure’ (namba) hizo ni za kweli, kama ni za kweli, tumeliwa kweli kweli,” alisema Lowassa alipokuwa akizungumzia mahesabu yaliyowasilishwa katika ripoti za uchunguzi kuhusu kiasi cha fedha ambazo Tanzania imepoteza.
 
Hapana Kuna Vyeo Kama ukivishika Utaendelea kuwa navyo


Balozi Hamis Kagasheki
President Obama
Secretary Hillary Clinton
Waziri Mkuu Lowassa
Judge Lubuva
President Bush
President Kikwete
Rais Mwinyi
Hata hivyo siyo wa awamu ya tano kama mleta hoja anavyosema!!
 
MZEE NAKUOMBA UJE UMCHUKULIE HATUA KALI SANA KUBENEA , KUMBE UNAHEKIMA HIVYO, ALITUHAMINISHA WEWE NI FISADI. KWAHILI NAKUUNGA MKONO
MWANAHALISI.jpg
 
Haya na nyumbu nao watabadilisha na kufuata kupongeza maadamu aliyeshika akili zao keshasema, utamuona Tundu, Mbowe, Msigwa, na takataka wengine wakibadilisha mawazo!
Hahahaha takataka yeuwii!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom