Edward Lowassa ahojiwa Dodoma


M

Msharika

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
937
Likes
4
Points
35
M

Msharika

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
937 4 35
  • Ni kuhusiana na mgawanyiko ndani ya CCM
  • Sitta amshukia Rostam kuhusu Richmond
  • Ripoti ya Kamati ya Mwinyi kuzua mtafaruku
Na John Daniel, Dodoma

WAKATI macho yote ya Watanzania yako Dodoma kuangaza mustakabali wa Chama cha Mapindzui juu ya mgawanyiko miongoni mwa wabunge wa chama hicho na Serikali, baadhi ya vigogo waliitwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa na Kamati ya Maadili ya CCM juzi kuhusiana na mgawanyiko katika chama hicho.

Mmoja wa vigogo waliohojiwa ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Edward Lowassa, ambaye habari zinasema, alihojiwa kuhusiana na mgawanyiko wa hivi karibuni ndani ya CCM ambao umezidisha uhasama miongoni mwa wabunge wa chama hicho na kuisumbua serikali.

Mgawanyiko ulioko miongoni mwa Wabunge wa CCM wenyewe na Serikali yao ulisababisha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho kuunda Kamati maalum ya kuzungumza na wabunge wanaodaiwa kutofautiana kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi nchini.Kamati hiyo inaongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

“Mheshimiwa Lowassa aliitwa na kuhojiwa na Kamati kwa takriban saa tatu. Hii inatokana na uamuzi wa Chama kwamba suala la mgawanyiko miongoni mwa wabunge wa CCM na Serikali lazima mambo yote yamalizwe kwa sasa na tukitoka hapa tunaanza ukurasa mpya,”kilisema chanzo chetu.

Majira ilipowasiliana na Bw. Lowassa kuhusiana na kuitwa kwake kwenye kamati alisema kwa ufupi kwamba hana cha kusema katika vyombo vya habari kwa sasa. Alipoombwa kuthibitisha kama aliitwa kweli alijibu tena kwa ufupi: "Nimesema sina cha kusema, waulize haohao waliokwambia,” alisisitiza.

Hata hivyo taarifa zaidi kutoka ndani ya kikao hicho cha maadili zinaeleza kwamba taarifa yao ya kazi iliwasilishwa jana katika kikao cha Kamati Kuu kulichoketi jana hadi usiku kwa ajili ya kufanyiwa kazi kabla ya kuwasilishwa rasmi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho leo.

Wakati vigogo hao wakihojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM, kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichoanza jana asubuhi kiliendelea hadi saa 10 na wajumbe walipotoka walirejea tena saa 12 kuendelea na kikao hadi usiku huku suala la maridhiano kati ya Katibu Mkuu wa CUF Bw. Seif Sharif Hamad na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Abeid Amani Karume ikitajwa kuwa ni miongoni mwa ajenda zilizozua mjadala mkali.

Ajenda nyingine iliyoelezwa kuzua mjadla makali CC ilitajwa kuwa ni taarifa ya awali ya Kamati ya Mzee Mwinyi ambayo ina mapendekezo lukuki juu ya kumaliza mpasuko miongoni mwa wabunge wa CCM na kati ya Bunge na Serikali. Pia taarifa na mapendekezo ya Kamati ya Mmaadili ilielezwa kuwa ni miongoni mwa ajenda zilizozua mjadala mkali na wa muda mrefu.

Ajenda nyingine iliyotajwa kuzui mjadala mkali ni mpango wa uchaguzi Mkuu ujao ambapo kikao hicho ndicho kinachotakiwa kutoa mwelekeo wa taratibu mbalimbali za uchaguzi unatarajiwa Octoba mwaka huu.

“Lakini taarifa ya Mzee mwenyewe tutapewa taarifa ya awali jioni bado haijawasilsihwa, hatujui itakuwaje kama bado kutakuwa na dalili ya mgawanyiko kama ilivyokuwa katika kikao kilichopita cha NEC au la,” kilisema chanzo chetu mara baada ya wajumbe kutoka mapumziko ya muda mfupi.

Katika kikao cha NEC iliyopita wajumbe kadhaa wanaodaiwa kuwa ni miongoni au wanatumiwa wa mafisadi walizua hoja kali ya kutaka Spika wa Bunge Bw. Samwel Sitta, avuliwe uanachama kwa madai kwamba makucha yake ni makali mno kwa Serikali hivyo anahatarisha uhai wa CCM.

Hata hivyo hoja hiyo iliishia angani baada ya wajumbe wanaotafakari mambo kwa makini akiwemo Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete, kubaini kuwepo kwa chuki za wazi binafsi na maslahi binafsi ndani ya hoja hiyo.

Pia taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya Richmond kufungwa na Bunge ilitajwa kuwa ni moja kati ya masuala yaliyochukua muda kwa wajumbe wa CC kutafakara na kujadili hasa kipengele kilichoweka na Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge kwamba kiongozi wa juu wa nchi ndiye aamue hatma ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Bw. Edward Hoseah.

Katibu wa NEC Bw. John Chiligati, hakuweza kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hizo na badala yake alisema hawezi kuzungumza lolote hadi mwisho wa kikao cha CC au baada ya kikao cha NEC. “Jamani chakula bado kipo jikoni, sasa utakula vipi wakati bado kinapikwa, subiri tu, kikiiva mtakula, tu,”alisema Bw. Chiligati.

Taarifa ya Mzee Mwinyi ambacho ni lazima ijadiliwe kwa kirefu na NEC katika kikao chake kinachoanza leo hadi kesho Jumatatu ndio itatoa dira ya mpasuko wa CCM au uimara wa chama hicho.

Wakati huohuo Spika wa Bunge Bw. Sawele Sitta, amemshukia Mbunge wa Igunga Bw. Rostama Aziz, kuhusu maoni yake kwamba Bunge halijawatendea haki Watanzania kumaliza suala la Richmond.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika ukumbi wa CC jana, Bw. Sitta alisema kama kuna mtu yeyote anahoji uhalali wa Bunge kufunga mjadala huo ni kosa kwa kuwa haiwezekani mtu yeyote kuanza tena suala hilo.

"Hata Mahakama huwezi kupeleka suala ambalo Bunge limeshafunga ukaanzisha tena, kama ni hivyo basi hata miswada tunayopitisha Wabunge wasioridhika wangekuwa wanafungua kesi, hiyo ni kutapatapa tu,"alisema Bw. Sitta.
 
kimatire

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Messages
373
Likes
19
Points
35
kimatire

kimatire

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2008
373 19 35
The future for you, me and us all never just happened. It was created. To promote co-operation and teamwork, remember; People tend to resist that which is forced upon them. People tend to support that which they help to create. Achieve your goals, objectives desires by reaching out to those first who need your help before they help you.......

Unfortunately in this mad race against time, in this race to acquire wealth, power, position we forget the every people who we need to connect at all times, the very people that will ensure long lasting peace, the very people that help us to realize our dreams and beyond...
 
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2007
Messages
1,372
Likes
7
Points
135
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2007
1,372 7 135
kimatire.. u need to get off that reefer son.lol. I know from ur words, u blaze.lol
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Walikuwa wapi kumhoji siku zote hizo?wanamhoji sasa wakati ana nguvu za kujitetea baada ya Bunge kuuchuna kwenye issues kadhaa zilizokuwa zinamhusu.It is too late kumhoji yeye kwa sasa na ni upuuzi mkubwa..
 
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
850
Likes
4
Points
0
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
850 4 0
You got the human race, you got the horse race, you got the dog race.....but this is a rat race!!
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,874
Likes
314
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,874 314 180
Mi nilifikiri thread imeandikwa " EL atimuliwa CCM" kumbe kuhojiwa tu - hakuna kitu hapo wakuu, sina uhakika hata kama atapata barua ya karipio toka CCM makao makuu.
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
ni ujinga tu wote na CCm yao imeoza kwa rushwa
 
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,849
Likes
29
Points
145
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,849 29 145
Kapongezwa kwa dili zake ila kaombwa apunguze wadanganyika wanaanza kuelimika....lol.
 
R

Ronaldinho

Member
Joined
Aug 7, 2009
Messages
69
Likes
0
Points
0
R

Ronaldinho

Member
Joined Aug 7, 2009
69 0 0
The saga continues...."tulimuita tukamuhoji akajielezea tukaona kuwa ni vyombo vya habari tu ndivyo vilivyokuza huo mgawanyiko,kwa sasa CCM tuko safi na tunaendeleza mapambano,asema kiongozi mmoja wa ngazi za juu"
 
B

Big Dady

Member
Joined
Nov 10, 2009
Messages
59
Likes
0
Points
0
B

Big Dady

Member
Joined Nov 10, 2009
59 0 0
Humo ndani kuna genge la mafisadi, unatarajia nini. Wa tz tutaendelea kuzugwa kila uchao. Ingekuwa enzi za Mwalimu, kweli tungetarajia watu kuwajibishwa, sasa serikali ya kishikaji hii, hamna lolote.
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
It is all about a politics and all are political animals like others
 
T

Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,350
Likes
1,125
Points
280
T

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,350 1,125 280
Lowassa and co. are king makers. Nobody will dare removing them from CCM.
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
64
Points
135
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 64 135
Ni nani mwenye ubavu na jeuri ya kumwita na kumhoji. Lowassa ndio mwenye uwezo huo, naweza kukubaliana na kauli kuwa Lowassa aliitwa kuombwa msamaha, hata kamati ya bunge haikuwa na ubavu wa kumwita na kumhoji, sembuse chama.
 
T

TANURU

Senior Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
162
Likes
0
Points
0
T

TANURU

Senior Member
Joined Jan 13, 2010
162 0 0
ni nani mwenye ubavu na jeuri ya kumwita na kumhoji. Lowassa ndio mwenye uwezo huo, naweza kukubaliana na kauli kuwa lowassa aliitwa kuombwa msamaha, hata kamati ya bunge haikuwa na ubavu wa kumwita na kumhoji, sembuse chama.
mwisho wa reli.
 
K

Kachero

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Messages
216
Likes
1
Points
0
K

Kachero

JF-Expert Member
Joined May 25, 2009
216 1 0
Wimbo ni ule ule wa siku zote,tangu mwanzo tulisema serikali hii ya CCM haikuwa makini kulishughulikia suala hili la Richimond.Sasa wanamuita EL ili kumuhoji nini,ni nani ndani ya CC au NEC mwenye ubavu wa kumuhoji EL ilhali hata JK mwenyewe anamgwaya.

Hiki ni kiini macho tuu na hii ndiyo picha halisi ya CCM kwamba hawako serious na issues zinazowaumiza watanzania walio wengi.

Matumaini ya maendeleo kwa watanzania yapo mahali pengine na sio CCM.
 
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2008
Messages
280
Likes
5
Points
0
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2008
280 5 0
Nani wa kumfunga paka kengele, Lowasa kabla hajajiuzulu alisema endapo kila mtu hapa akianza kuchunguzwa hamna atakayebaki. Akiwa na uhakika hakuna aliye msafi na hiyo ndiyo hali halisi. lets wait and see.
 
K

Kidogo chetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2009
Messages
1,428
Likes
803
Points
280
K

Kidogo chetu

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2009
1,428 803 280
Kwanza kikwete mwenyewe akisikia ati kuna agenda ya kumkemea tu mamvi wallah aliyeipeleka atafute pa kwenda
 
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2008
Messages
280
Likes
5
Points
0
manenge

manenge

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2008
280 5 0
Suluu ya kweli inaweza kupatikana tu endapo kutakuwa na tume huru ambayo itachunguza madudu yote yaliyofanywa na kuyaanika sio kwa nia ya kufunga mtu jela bali iwe somo kwa jamii ili kuepuka kuyarudia tena kwa vizazi vijavyo otherwise kuhojiana mtu mmoja mmoja ni kutaka kufunika kombe mwana haramu apite.
 

Forum statistics

Threads 1,251,231
Members 481,615
Posts 29,763,626