Edward Lowasa aongea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Edward Lowasa aongea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MushyNoel, Jan 31, 2011.

 1. M

  MushyNoel Senior Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waziri mkuu aliachia ngazi kwa kashfa ya richmond nae ameongelea masuala mbalimbali yanayohusu nchi hii.Akiwa monduli katika hafla ya wahitimu wa chuo kimoja cha ufundi mjini humo Mheshimiwa lowasa ameusia umuhimu wa kuangalia suala la ajira kwa vijana ambalo tatizo limeongezeka mara dufu licha ya ahadi ya ajira milioni moja zilizoahidiwa na chama chake (CCM).Pia amesema wananchi wanaweza kujadili mambo muhimu mengine kama richmond na dowans.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Lowassa anaanza kuiandaa njia ya kuwa mgombea wa CCM kwa ulazima.Imeelekezwa mgao wake wa DOWANS ugawanywe nusu kwa nusu apewe PINDA kwa kulazimisha malipo jambo ambalo LOWASA hajaliafiki hivyo yupo tayari wakose wote.Ndio maana anataka ishu irudi bungeni amuumbue mkuu wa kaya kwa namna alivvyoshiriki in RICHMOND, pia atawaumbue wengine.LOWASA ni bingwa wa propaganda na mitandao na ataigharimu serikali kama mgao wake utagawanywa.
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ajira milioni moja ziliahidiwa 2005 - 2010.
  Ili kujiridhisha wakachakachua takwimu, hata kama ulikuwa unauza karanga stendi ya Ubungo nawe ulihesabiwa kwamba CCM imekutengenezea ajira hiyo.
  Tanroads kabla ya uchaguzi wanatuonyesha hata barabara zilizolimwa kwa jembe la mkono, eti sasa Tanzania barabara zote zinapitika - Sh***nzy taipu. (kunradhi Mods)

  Lowasa nae aache kurejea kwa kupitia uani. Ametuhumiwa kwenye kadhia nyingi and it would have been noble if he came out clean. Ajitakase atakasike, watanzania Mungu kawatunuku moyo wa rehema watampima kama toba yake ni ya kweli.
  Sasa hivi kila akiongea anazungumza ambacho watanzania tunataka kusikia, EL unatutega????

  Pengine ni vizuri wanasiasa wa sasa wakajua kuwa hatuhitaji longo longo nyingi sasa hivi, watanzania wanataka vitendo.
  Ukiongelea barabara za juu tuone magreda yanafanya kazi;
  Ukizungumzia usafiri wa boti tegeta hadi mjini, tuone umeanza kujenga gati;
  Tunaambiwa shida ya umeme kuwa historia, huku watu wako ndo wanataka kwenda kujadili hilo Urusi;
  Elimu bora kwa wote, wakati wadogo zetu wanaambulia Div 0 hii yote kutuongezea mizigo kwenye familia zetu tu;
  Kama ni ztatizo la kina mama wajawazito suluhu sio bajaji 400, jenga zahanati; bajaji 400 ni karibu billion 2.4 mtu anataka ziende kukuza uchumi wa India (tumerogwa????????????)

  Wakati EL anasifika kwa utajiri cha ajabu naye anaishia kuwa mchuuzi tu kama kina sie weye senti za kuunga unga. Taita kama EL anafungua biashara za pharmacy na Dry cleaner??.
  Hivi akikata bilioni 5 kati ya nyingi alizonazo akafungua kiwanda cha nyama Monduli asingetengeneza soko la mifugo na ajira kibao kwa watanzania na pesa ya kigeni juu.
  Supamaketi zimajaa baked beans toka nje wakati mbeya maharage ya kumwaga

  Wenye viwanda hapa Tanzania ukiondoa wachache kama Bakhresa, Mengi n.k waliobaki wote ni watanzania wenye passport mbili mbili. Akiba zao wanaweka canada na uingereza ili siku rais kawa mtikila wanakwea pipa.

  Tunachoka na matamko; Huyu kasema, yule kasema....everyday!!!!!!!!!!!
   
 4. M

  Msharika JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  panga na shoka nimeshanoa vipo Tayari kwa kazi ikibidi. waache walikoroge kisha watakutana nami kama baba ubaya vile:clap2:
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Huyu kabaki historia. Atakuwa anakosea kama anafikiri kila kitu kinanunulika kwa pesa.
   
 6. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Lowassa just to let you know huo muda hautaufikia kamwe angalia yanayoendelea Egypt ndipo uje uongee. Hizi ndoto za mchana WATANZANIA WAMECHOKA NA NINYI WATU KITAELEWEKA SIKU ZA KARIBUNI KAA MKAO WA KULA USIJIDANGANYE. Cha msingi ni bora ungeendelea kukaa kimya kuliko unavyozidi kupayuka payuka unazidi kutujaza hasira. Ajira ajira ulikuwa wapi miaka yote kujua vijana wanakosa ajira ni leo ndio umegundua kuna vyuo Tz. Kaeni majumbani mwenu tuachieni hii nchi tutajua wapi tunaipeleka kulia au kushoto.
   
 7. P

  Pokola JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mimi ni bare knuckles tu kwa EL na RA. Hadi wanye. Nasubiri tu kipenga, kazi ikianza ntajituma wajameni.:sick:
   
 8. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  achen chuki binafsi Lowassa ana quality za good leader na ni mchapakazi ni bora mara elfu ya mkwere na kazi yake inaonekana mtasema saana 2015 huyo ikulu mpende msipende for once rais anatokea Rchuga
   
Loading...