Tetesi: Edward Lowasa ahaha kusaka bilioni 10 alizokopa kwa Rostam kugharamia Uchaguzi Mkuu wa 2015

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Hii sasa inaitwa kama mbwai na iwe mbwai. Taarifa rasmi nilizopata ni kwamba Rostam Aziz yupo nchini Afrika ya Kusini ambako ameamua kuweka maskani yake. Taarifa zinasema kuwa kwa sasa biashara zake hapa nchini zinasimamiwa na mdogo wake ambaye pia amepewa jukumu la kusimamia mradi wa kitega uchumi pale Oysterbay Police. Rostam ameamua kuondoka nchini kutokana na biashara zake kutoenda vizuri hasa kutokana na ukweli kwamba zilijengwa kwa misingi ya kubebwa na sasa fursa hiyo haipo tena baada ya Rais Magufuli kuweka misingi ya biashara halali.

Hadi anaondoka nchini, Rostam Aziz alikuwa amemkopesha swahiba wake, Edward Lowasa shilingi bilioni 10 kwa awamu mbili tofauti. Awamu ya kwanza alimpa shilingi bilioni 5 Mwezi Julai 2015 wakati ambapo Lowasa alikuwa na mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE ya kuhamia UKAWA. Fedha hizo ni miongoni mwa zile Bilioni 10 ambazo Lowasa alimpa Mbowe ili kurahisisha safari yake ya kugombea Urais kupitia UKAWA.

Awamu ya pili Lowasa alipokea shilingi bilioni 5 Mwezi Agosti 2015 ambazo zilienda kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, MBOWE kwa lengo kugawa kwenye majinbo yote ambayo CHADEMA walisimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, inadaiwa kuwa fedha hizo hazikwenda kama ilivyotarajiwa ambapo Mbowe aliamua kugawa shilingi milioni 50 tu kwa kila jimbo kwa majimbo 30 tu.

Makubaliano ya Rostam na Lowasa ni kwamba, ikiwa Lowasa angeshinda Uchaguzi huo, angempa swahiba wake zabuni ya kuendesha mitambo ya kufua umeme pale Kinyerezi. Aidha, katika makubaliano hayo, waliafikiana pia kuwa ikiwa Lowasa hatafanikiwa kushinda Urais, fedha hizo zirejeshwe kwa njia ya kampuni za Rostam kupewa Zabuni kwenye Halmashauri zitakazoongozwa na CHADEMA. Lowasa alimhakikishia Rostam kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa kama walivyokubaliana. Hii ni kwa sababu, Lowasa alikuwa na mtandao mpana wa ma DED ambao walipata dhamana hiyo kwa ushawishi wake ambao alikuwa na uhakika kuwa hawatamwangusha kwenye Uchaguzi huo.

Hata hivyo, baada ya Lowasa kuangushwa kwenye Uchaguzi na mtandao wake wa Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio uliofanikisha CHADEMA kushinda kwa baadhi ya majimbo kuvunjwa, Lowasa anahema na kutweta. Bilioni 10 alizokopa kwa Rostam zinamtesa. Hajui wapi pa kuzitoa na Rostam anasisitiza kuwa lazima Lowasa atekeleze vipengele vya makubaliano yao. Kazi ipo
 
Viwanda vimeshindikana,sukari imekwama sasa fyatueni watoto
 
Attachments

  • IMG-20160821-WA0000.jpg
    IMG-20160821-WA0000.jpg
    14.7 KB · Views: 37
Ww hujui propaganda
Tafuta mume akuoe tatizo ni kuvizia vi bwana vya watu huko ccm na io sura mbaya ndo kabisaa utaishia kuwa kuu kuu
Humjui lowasa ww
Muulize mwinyi mkapa kikwete watakwambia kama lowasa ni mtu wa kukopa vihela vya chai ivo
Mwaka 1972 account ya lowasa ilikuwa na shilingi laki 3 mshahara wa raisi nyerere ulikiwa ni 4000 kwa mwezi unataka kutuambia nn ww
Humjui lowasa wala rostam kaa kimya
 
Lizaboni huyo na hekaya motomoto. Baada ya kuona Nairobian ametunga hadithi bora zaidi, ameamua kuja na utunzi wa Kinyerezi. Nia ya Lizaboni kuja harakaraka na hii story za kuungaunga ni kuhakikisha hafunikwi na watunzi wapya kama akina Nairobian.
 
Jamaaa unavyosumbuliwa na LOWASSA asiye na madaraka yoyote ni hatari.

Mwambie MAGUFULI afanye kazi, aache matamko ya ajabu ajabu utadhani si Rais
Mf" Sasa fyatueni - arudishe hela za kampeni za uzazi wa mpango. Mchanga wa dhahabu marufuku kwenda nje.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Hii sasa inaitwa kama mbwai na iwe mbwai. Taarifa rasmi nilizopata ni kwamba Rostam Aziz yupo nchini Afrika ya Kusini ambako ameamua kuweka maskani yake. Taarifa zinasema kuwa kwa sasa biashara zake hapa nchini zinasimamiwa na mdogo wake ambaye pia amepewa jukumu la kusimamia mradi wa kitega uchumi pale Oysterbay Police. Rostam ameamua kuondoka nchini kutokana na biashara zake kutoenda vizuri hasa kutokana na ukweli kwamba zilijengwa kwa misingi ya kubebwa na sasa fursa hiyo haipo tena baada ya Rais Magufuli kuweka misingi ya biashara halali.

Hadi anaondoka nchini, Rostam Aziz alikuwa amemkopesha swahiba wake, Edward Lowasa shilingi bilioni 10 kwa awamu mbili tofauti. Awamu ya kwanza alimpa shilingi bilioni 5 Mwezi Julai 2015 wakati ambapo Lowasa alikuwa na mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE ya kuhamia UKAWA. Fedha hizo ni miongoni mwa zile Bilioni 10 ambazo Lowasa alimpa Mbowe ili kurahisisha safari yake ya kugombea Urais kupitia UKAWA.

Awamu ya pili Lowasa alipokea shilingi bilioni 5 Mwezi Agosti 2015 ambazo zilienda kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, MBOWE kwa lengo kugawa kwenye majinbo yote ambayo CHADEMA walisimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, inadaiwa kuwa fedha hizo hazikwenda kama ilivyotarajiwa ambapo Mbowe aliamua kugawa shilingi milioni 50 tu kwa kila jimbo kwa majimbo 30 tu.

Makubaliano ya Rostam na Lowasa ni kwamba, ikiwa Lowasa angeshinda Uchaguzi huo, angempa swahiba wake zabuni ya kuendesha mitambo ya kufua umeme pale Kinyerezi. Aidha, katika makubaliano hayo, waliafikiana pia kuwa ikiwa Lowasa hatafanikiwa kushinda Urais, fedha hizo zirejeshwe kwa njia ya kampuni za Rostam kupewa Zabuni kwenye Halmashauri zitakazoongozwa na CHADEMA. Lowasa alimhakikishia Rostam kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa kama walivyokubaliana. Hii ni kwa sababu, Lowasa alikuwa na mtandao mpana wa ma DED ambao walipata dhamana hiyo kwa ushawishi wake ambao alikuwa na uhakika kuwa hawatamwangusha kwenye Uchaguzi huo.

Hata hivyo, baada ya Lowasa kuangushwa kwenye Uchaguzi na mtandao wake wa Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio uliofanikisha CHADEMA kushinda kwa baadhi ya majimbo kuvunjwa, Lowasa anahema na kutweta. Bilioni 10 alizokopa kwa Rostam zinamtesa. Hajui wapi pa kuzitoa na Rostam anasisitiza kuwa lazima Lowasa atekeleze vipengele vya makubaliano yao. Kazi ipo
***
TALES OF ALFU-LELA-ULELA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom