Edward Hosea, constructive engagement uliyonayo itaua TLS. Serikali ikiwanyima fedha mtajiendesha vipi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nadhani TLS Ina wanachama wasio na akili na mawazo yakujitegemea;wanachama wengi wana mawazo kama yalivyo maono ya Watumishi wa Umma kwamba serikali ikupe posho,salary,nyumba,matibabu nk lakini pamoja na vyote hivyo mtumishi huyu anashindwa kujenga japo nyumba huku asiye na kazi aliyepo Kijijini akifanikiwa kujenga.

Dr.Hosea ni mtumishi wa Umma ambaye kwake kujitegemea siyo kipaombele Wala maono Bali kujitegemea serikali ndio proud kwake. Lakini anashindwa kuelewa kwamba wakati anaomba pesa serikalini anazifanya fedha hizo zisijenge Shule,hospital na kununua madawa apewe yeye ambaye anaongoza wasomi wanaoweza/wanaoweza kujitegemea wakapata kipato. Chama Cha wasomi kinaposhindwa kujiendesha kikaja n sera za constructive engargement ni chama mfu na akipaswi kuitwa Chama Cha wanasheria.

Nchi maskini kama yetu tunatenga bajeti yakusaidia wasomi kuendesha shughuli zao? Tunatenga fedha kuofset fee za wasomi? Wasomi wanaacha kuumiza kichwa kuipatia fedha Nchi wanaumiza kichwa namna yakukaa meza Moja na watawala kula Kodi za walala hoi na wanajipongeza? Huu ni ufinyu wa fikra.

Leo TLS inashindwa Nini kutoza fees and subscription Kwa seniority? TLS inashindwa nini maandiko ya miradi yatakayogharimia baadhi ya activities zake?

Serikali itenge billion kuwasiadia watu wanaotoza mamilioni wananchi Kwenye kesi? Nadhani Dr. Hosea hii constructive engargement hapana huu ni ufikiri wa kiwango Cha chini sana Kwenye Taifa letu.

SAWA umepata hizo Kodi za wananchi,je utaweza kumweleza ukweli huyo mtoa fedha Kwa kuzingatia ñguvu aliyonayo kikatiba? Kenya Mawakili wanalindwa na katiba Nini hizi fedha umezipata Kwa constructive engargement,siku mkizikosa overnight mtajiendeshaje? Au mtaenda mahakamani kuzidai?

Ni fedhea Kwa wasomi kuacha Kuishi Kwa sera za kujitegemea wakaishi Kwa sera za kutegemea. Lini mtakuwa huru? Hakuna watu Kati yenu wamesoma uchumi,miradi, uwekezaji, diplomasia nk wawasaidie kujikwamua hapo mlipo? Kwamba you believe you can have sustainable TLS Kwa ruzuku ya serikali? Seriously?

No nachelea kuwaita wasomi,iishie kusema TLS inajinyonga Kwa mikono yake yenyewe. Sidhani kama young wanasheria wanaambulia chochote Kwa aina hii ya ufikiri. Miaka sitini Tanzania iwe maskini na TLS iwe maskini? Nimegundua kwanini serikali inaajiri Mawakili kutoka nje, thinking ya Mawakili haitoshi hata kidogo kutetea maslahi ya Taifa. They are not thinking big.

Poleni wategemezi wa constructive engargement
 
TLS ilizaliwa miaka zaidi ya 60 iliyopita huko nchini Tanzania zama hizo ikiwa Tanganyika. Imejaaliwa kupata watoto zaidi ya elfu kumi; watoto kadhaa wamebainika TLS ilizaa na serikali (Watumishi wa Umma), watoto kadhaa wamebainika mzazi wao mmoja taarifa zake hazipo weli known (wasio practice) na watoto takribani elfu (wanaopractice) wamebainika ni watoto wa ndoa.

Pamoja na TLS kuzaa watoto elfu kumi lakini inapofika umri wa kustaafu watoto wanagombania mafao ( uwezo wa kujiendesha) badala ya watoto japo hao elfu kusimama na mzazi aanzishe japo biashara yakumfanya aishi vizuri uzeeni.

Matokeo yake baada ya TLS kubaini kwamba ana mzazi mwenzie (serikali) ameamua kwenda kumbembeleza amsaidie kuilea familia yake bila kujali ugumu wa masharti atakayopewa.

Tumeshuhudia wazazi wanaotegemea watoto wa kambo wanavyopita vipindi visivyo tabirika,Leo wanapendwa kesho hata chakula wananyimwa. Ni vigumu wazazi wa aina hii kuwa na say kuwakanya watoto Kwa sababu misaada itakatwa.

Dr. Hosea alichofanya yeye ni kuipeleka TLS Kwa mzazi mwenzie mwenye mamlaka ya kusema tunakula nini na wote tukala hicho hicho, hakuna kuhoji maana chakula chaweza kumwagwa.

Nikiri wazi chama changu kimeanza kufa, kimekufa Kwa sababu tumeamua kukiua wenyewe; burihani TLS
 
This question is directed to you members of THE TANZANIA LAW SOCIETY. What did you expect when you elected a CCM mole to be your President?
 
Tanzania ngumu sana aisee..

inawezekana kabisa serikali ikawa na matatizo yake na waliopo kwenye mifumo.

Lakini pia jamii nzima ya Tanzania kama watanzani tuna matatizo makuubwa sana aisee ambayo kama jamii inahitaji re-shape.

Sisi tulioko uraiani tunawanyooshea sana vidole walioko madarakani na kwenye system lakini hata sisi wengi wote Kama sio wote ukitupima pia utagundua ni walewale na hatuna tofauti yeyote na wale walioko madarakani...

Mwisho wa siku utagundua Tatizo la Tanzania ni watanzania woote tu wajingawajinga..

Mtanzania ameathiliwa sana na siasa kiasi kwamba kila jambo kwake ni siasa..
Mtanzania ameathiriwa sana na udini na anaishi kwenye dini zaidi kuliko Utanzania wake na watanzania wenzie..
Mtanzania ameathiriwa sana na ukabila, YES, ukabila japo tunaamini Mwalimu Nyerere alilizika hili lakini hapana liko mitaani na kwenye mioyo ya watu na watu wanaishi sana kwa ukabila.
Mtanzania ni mwizi na mnafiki...

Tumuombe sana Mwenyezi Mungu aisee..
 
Back
Top Bottom