Educated TZ Immigrants in US in tough Situation

Mazee....karatasi za XXXXXXXL hazina ugumu, mizengwe wala masharti mengi. Sharti pekee na muhimu ni penzi tu! Ukiwa nalo hilo karatasi kama unalia vile. Hizo njia zingine wengine zinaweza zikawapa shida kidogo...au unasemaje wewe mazee? Maana najua umeshajivinjari anga za XXXXXXL......LOL....natania mazee

LOOOOOOOOL !! Mazee zile XXXXXL mimi siziwezi kabisa maana mpango wa kuwa na tochi kule ni SOO hahahahah. Ziko hapa size bomba kabisa yaani makini na zinatoa karatasi bila ya matatizo hahahahaha.
 
1.Elimu--Elimu ya Marekani, tofauti na watu wakitoka Tanzania, hufikiri ni rahisi, lakini inakuwa na Homework za kila siku, kwa hiyo discipline ya Kusoma na kujituma ni kubwa tofauti na kusomea mithihani nyumbani..

Elimu ya majuu ni rahisi kuliko ya Bongo, I have had the opportunity kusoma Mlimani na kupiga Masters yangu ulaya. Hizi shule nyingi za mamtoni unaingia darasani mara moja ua mbili kwa wiki? Unaweza kumudu kusoma huku unapiga mzigo zaidi ya masaa arobaini na viwanja unajirusha kama kawa. Hakyanani nigekuwa nafanya hivi enzi zangu za mlimani- wangekula kichwa!Tukumbuke pia shule zetu za kibongo walimu wana mitihani ile ya kukomoana, wanafunzi wengi wakifeli mwalimu ndio anajiona mjanja, mara ngapi umewahi kukutana na maswalli kwenye mtihani ya topics ambazo hata mwalimu hajawahi kufundisha?Enzi hizo tena kulikuwa hakuna hata system ya semister,unafanya UEs za masomo sita na maswali yanacover topics zote ulizosoma kwa whole accademic year!
 
endeleza kwenu--Kijiji chako ni jukumu lako, sio la Serikali..Tunasema : Nyumbani Nyumbani..

Ngurudoto ndugu yangu naona unataka kufufua azimio la Arusha! Nyumbani ni kokote pale ambapo wewe na familia yako mko happy and comfortable. Naweza kurudi kijijini kwetu nikajenga bungalow la nguvu lakini, I believe, as an individual siwezi kujivutia umeme, maji au kujenga zahanati- haya ni majukumu ya serekali.
 
Kalamu, kama hujaelewa topic hii kasome topic nyingine!. Hii topic kuna baadhi ya watu hawataielewa lakini kuna watu nimewaguswa na wananielewa vizuri sana. Hii siyo siasa na madongo hayatasaidia hapa. Kama una mawazo yatoe lakini kama huna kasome topic nyingine.
 
LOOOOOOOOL !! Mazee zile XXXXXL mimi siziwezi kabisa maana mpango wa kuwa na tochi kule ni SOO hahahahah. Ziko hapa size bomba kabisa yaani makini na zinatoa karatasi bila ya matatizo hahahahaha.

Lakini mazee hizo za small na medium sio reliable. Ziko macho juu sana. Hazikawii kukutosa katikati ya safari. Mwenzio nshashuhudia machizi wakitoa machozi hivi hivi....kisa...? Jamaa mwenye rims kachukua....ahahahahahahhhhh...kwa hiyo bado nadhani XXXXXXXL ni safe na reliable......kwikwiwiiiii
 
Noma sana mtu anapoingia mitini katikati ya Safari Mazee noma sana hahahahahahha unakuta mtu anakuwa mpole kama nini maana inabidi kuanza upya.
 
Jamani mbona karatasi zipo za kirahisi sana nashangaa watu wanahangaika bila ya kuwa na karatasi hahahahahaha.

Nyani kuna karatasi kibao bila ya kuchukua mademu XXXXXXL ha ha ha ha.

Jamani mbona karatasi za xxl hazina noma? XXl watamu sana! halafu juu yake karatasi hilo! mbona bongo mademu wanene tulikuwa tunawachangamkia tu? bila karatasi wala nini! na juu yake tulikuwa tunawatoa out vilevile. wengine ilikuwa katika kuchagua demu mwembamba au mnene tulikuwa tunachagua mnene, tunaona ameiva;)mwembamba tunaona ana ngoko au miwa;)

Wazee mbele kwa mbele. Kuna demu mmoja pale Arusha mpaka Pepe kalle alimwimbia nyimbo za Hidaya waangu!watu walikuwa wanamtamani kwa sababu alikuwa bonge la XXL.
 
Hii mada nimeifurahia sana. Mimi nilichokuja kugundua katika Tanzania ni kwamba tumekuwa na uelewa mdogo sana kuhusu maisha katika nchi za kigeni kwa ujumla.

Hii hatuwezi kulaumu mtu yeyote hila ni siasa tulizojengewa, baada ya kubadilika gafla hatukuweza kwenda na wakati kwa muda uliostaili.

Nasema hivi kwa sababu mpaka sasa vijana bado wanafanya strugle kubwa kuona wanaondoka nchini lakini kitu kikubwa mara nyingi huwa hawajui huko waendako wanaenda kufanya nini?

Vile vile ukikaa Tanzania ukaangalia vijana wanasoma hata wanaosoma vyuo vikuu huwa hawajui haswa wanasoma ili iweje? Kwa mfano vijana wengi unaweza kukuta wanatumia muda mrefu kujadili jinsi watu waliokwenda marekani/Uingereza na nchi mbali mbali wamefanikiwa bila kujua energy kiasi gani wametumia katika kupata mafanikio hayo. Hivyo unakuta struggle kubwa ni kuhakikisha anafika huko lakini akifika anakuta upepo ni tofauti. Vile vile hii haiana tofauti na vijana kutoka vijijini wanavyofikiria kuja BOngo.

Vile vile kama masanja alivyojadili, hata tanzania maisha yamekuwa siyo mchezo, wakati mwingine ni bora mahala pengine maana hata ukipewa kazi ya box hata kama una masters huwezi kuona kama ni taabu. Lakini Bongo mwanangu hii inaweza kukumbusha mbali.

Kikubwa ninachoona ni kufanya kazi kwa bidii, ambacho nashukuru kuona vijana waliowengi sasa hata bongo unakuta mtu siku hizi ana kazi mbili tatu hivi(part time jobs). Halafu wengine wamehamua kujiendeleza wakati huo huo wakiendelea kupiga mizigo yao kama kawaida. Kuna watu siku hizi anasoma masters bongo huku akifanya kazi yake kama kawaida.

Hizi initiative za kufanya kazi mbili/tatu, kujiendeleza wakati unachapa mzigo zitapunguza hata muda wa kwenda vijiweni kama R/garden, nk.Duniani kote siku hizi hakuna lelemama labda mtu anayekwenda nchi za kijamaa(scandnavia countries) ambazp ukijilipua ukafanikiwa ni kama umegraduate higher degrees
 
Kithuku samahani nisingeweza kueleza vizuri kwa kiswahili baada ya miaka kumi na moja na sua sua na misamiati.

Samahani sana, usisesme hujui kuandika Kiswahili sanifu. Mimi nimekaa nje miaka 20 sasa, naongea Kiingereza na lugha ya hapa kila siku, lakini kamwe sijasahau kuandika kwa Kiswahili! Wewe huandiki barua nyumbani? Mfano mmoja, mpwa wangu siku moja alimleta kijana mmoja nyumbani kwetu. Kijana kuingia akatuambia , 'Hi'! Mie nikamuuliza, 'Are you a Tanzanian?' Kanijibu yeye ni mtanzania lakini amekaa nje miaka minne kwa hiyo hajui kuongea kiswahili vizuri. Nikmuonyesha binti yangu ambaye nilikuja naye huku akiwa na niaka miwili, na nadhani wakati huo alikuwa na miaka 17, binti yangu anaongea Kiswahili kizuri tu ingawa lafudhi (accent) yake ndio ya kigeni!! Hii tabia ya kusema huwezi kumudu lugha yako, jamani tuaiache maana sio kasumba nzuri! Wale tulio na watoto tuwasemeshe Kiswahili kwa vile atakuwa anaijua lugha yao ya myumbani na lugha zingine za pale. Hiyo itampa kujitambua yeye ni nani na kuweza kujenga utu (character) yake na kuleta hali ya kujiamini. Kujiamini ni moja ya vigezo vikubwa mtu anavyokuwa navyo katika kujiendeleza kimaisha, k.m kuweza kumudu vizuri zaidi maisha ya huku ughaibuni.
 
Mkuu Kamundu, heshima mbele nia ya mada yako ni njema sana, isipokuwa tu una ka-bias flani hivi against baadhi ya wabongo walioko US, na pia hujaona mengi sana duniani, lakini ninaheshimu kuwa nia yako bado ilikuwa njema, But:-

1. Ni lazima kuelewa sababu kwanza iliyomfanya mtu kwenda US in the first place, halafu pia uwezo wa yule mtu kufikiri, exposure aliyonayo kimaisha, anatokea maisha gani bongo, maana elimu sio kila kitu, nikiwa na maana kuwa Us kuna wa-Mexico, wanauza maua tu njiani na wanatuma hela kwao kila siku na wana maisha kuliko Blacks wengi wanaolipwa mishahara mikubwa!

2. Si kweli maneno uliyosema as a general ststement, isipokuwa kuna some isolations ishus, lakini most of the times wa kulaumiwa ni wabongo wenyewe kwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu maisha, mazingara walikotoka na mazingara waliyomo sasa, yaani ya US, wengi wanaenda kule na mawazo kuwa bado wako bongo off course maisha yatakuwa ni magumu hata uwe na elimu, hivi unajua ni wamarekani wangapi wenye degree na wanaendesha tax na wana maisha bora na ya uhakika? West Africans wako kibao, wanaendesha tax na wana elimu nzito, lakini ukiongea nao watakwambia kuwa the best decision they ever made katika maisha yao ilikuwa kusoma na kufanya kazi wanayo fanya walipo yaani kuendesha tax.

3. Wa-Tanzania tunasumbuliwa sana na kasumba ya waingereza, ya kufikiri kuwa ni lazima uvae suti kwenda kazini ili uwe na maisha mazuri, ukweli ni kwamba US kuna ubaguzi mkubwa sana, kazi za elimu na malipo makubwa zimetengwa kwa ajili ya wazungu kwanza, halafu weusi wachache kwa ajili tu ya ku-balance na kuwa politically correct on corporate side, lakini hizi kazi sio kwa wageni, hizi ni facts ambazo ni lazima uzifahamu kwa undani kabla hujaenda US kuishi, ukiwa umesoma au hukusoma it does not matter!

4. Kabla ya ku-make a final decision ya kwenda kuishi US, kama inawezekana jaribu kutembelea na nchi zingine kwanza hata Kenya tu ukasafishe macho, sio unatoka Kigoma na Bukoba, pruuuuu stop ya kwanza US, hata Dar'Salaama unapita tu kwenda airport, wengine wanapandia ndege Kampala, I mean unategmea nini huko Us kila kitu kitakuwa maajabu tu, yes ninasema hivyo kwa sababu nimeishi US 20 years, tena yote New York kwenye mambo yote kwa hiyo siongei hadithi ila ninaongea reality, wabongo huenda huko macho juu mno, wengine hata kazi hawajawahi kufanya inawachukua at least miaka mwiwili ya kwanza kutulia chini na kuanza kufikiri maan muda wote huo uliopita mnaona jamaa yupo tu kumbe bado analewa na ulaya, kutoka Mlimani na degree peke yake hakuwezi kukufanya ukaishi "unavyotaka" au "Ulivyotegemea" US,

5. Binafsi kabla sijaamua kwenda US, nilikuwa nimeshatinga melini in the process ya kazi hiyo nilipata bahati ya kutembela almost dunia nzima, kwa hiyo I had an-idea ni nchi gani inafaa kwenda kuishi kwa ajili ya kutafuta maisha na yanawezekana, guys hakuna nchi kama USA, that is it hata kama huna papers, bado maisha yake sio sawa na nchi yoyote duniani, yes I said nitajie nchi unayodhani ina maisha mazuri kwa mbongo hata kwa asiyekuwa na makaratasi, na elimu kama USA? Kama ukishindwa kuyaweza maisha US basi wewe huwezi mahali popote, tena ukirudi bongo utakufa mapema sana, lakini msilaumu nchi wala maisha!

6. Wabongo muache kudanganyana kuhusu USA na ulaya kwa ujumla, nimewaona wabongo wengi sana kule US, wengi wao hata ile idea ya kwa nini wameeenda kule hawana kabisa, I mean absolutely no clue, wavivu, wazembe, at one time mimi nimewakaribisha jamaa ndio kwanza wameingia toka bongo, ninafanya kazi masaa 16 kwa siku kuanzia J'matatu mpaka Jumapili, Ijumaa na jumamosi jioni ninapiga disco kwenye club, nikitoka pale ninaingia kazini moja kwa moja, wao wanajimwaga tu mangoma na kufanya kazi masaa manane tena madukani, na kunishangaa mimi kuwa ninajitesa sana, ebo! wewe ndio kwanza umeingia nchi ya watu huna lolote, ni lazima ukazane kwanza ili ujiweke sawa, baadaye ndio utatulia na kutafuta kazi unayoitaka, au ya shule, lakini lazima uwe na msingi mzito kujua kufanya kazi kwa bidiii, kwa sababu hata kama ukipata hiyo kazi ya elimu kama huna work ethics, ni bure, sasa yes maisha yatakuwa magumu sana huko majuu, maana kwanza utaridhika mapema na chochote unachopata badala ya kuhangaika,

7. Mabadiliko ya maisha hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, yanakuja kwa kuhangaika, ukifika kwanza unaaanzia chini hata kama umesoma, hiyo ni sheria ya kwanza ambayo watu wa West Africa wanaielewa sana kuhusu US, then pole pole unaaanza kujifunza mazingara, huku ukitafuta kusonga mbele, regardless ya makaratasi, ukiona mtu analilia makaratasi mapema ujue ni mviovu huyo, wakuu ngoja niwaambie ukweli wabongo niliowaona nilipokuwa US, waliokuja na kudai wanatafuta makaratasi kwanza, 80%, walishia kurudi bongo kwa kushindwa maisha, 10% waliishia jela kwa kujaribu kutafuta papers kwa nguvu, 5% waliyapata lakini hawakupata kazi walizoziomea, 5% waliishia kuwa deported,

lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what I did, I can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu,

Naomba kwa sasa niishie hapa, hakuna nchi njema duniani kama USA, usome usisome it does not matter, lakini ni lazima uwe umekwenda for the right reasons, na uwe the right person, US na Ulaya, sio kwa kila mtu, halafu kama ulishindwa maisha bongo hata kidogo tu basi uwezekano wa kutofanikiwa majuu ni mkubwa sana, kama umekwama uliza wengine wakusaidie, tuache uvivu na uzembe wa kufikiri, mind is a terrible thing to waste maana popote utaishia kuchekesha tu, kabla huja-give up uliza kwanza acha kitu wa-giriki wanaita egoooooo(Ego) na pride zisizokuwa na msingi, be humble na kubali kuelimishwa, lakini usiruke tu na conclusion especially a sensitive kama hiii, kwa wale walioko bado hapa bongo wanataka kwenda huko ninawaambia kuwa huko US ni safi na hakuna noma yoyote!

Ahsante Wakuuu!
 
3. Wa-Tanzania tunasumbuliwa sana na kasumba ya waingereza, ya kufikiri kuwa ni lazima uvae suti kwenda kazini ili uwe na maisha mazuri.

4. wabongo huenda huko macho juu mno, wengine hata kazi hawajawahi kufanya inawachukua at least miaka mwiwili ya kwanza kutulia chini na kuanza kufikiri maan muda wote huo uliopita mnaona jamaa yupo tu kumbe bado analewa na ulaya, kutoka Mlimani na degree peke yake hakuwezi kukufanya ukaishi "unavyotaka" au "Ulivyotegemea" US,

6. Wabongo muache kudanganyana kuhusu USA na ulaya kwa ujumla, nimewaona wabongo wengi sana kule US, wengi wao hata ile idea ya kwa nini wameeenda kule hawana kabisa, I mean absolutely no clue.

lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what I did, I can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu.

Mkuu hayo ni mawe tupu!!!
 
ukiona mtu analilia makaratasi mapema ujue ni mviovu huyo, wakuu ngoja niwaambie ukweli wabongo niliowaona nilipokuwa US, waliokuja na kudai wanatafuta makaratasi kwanza, 80%, walishia kurudi bongo kwa kushindwa maisha, 10% waliishia jela kwa kujaribu kutafuta papers kwa nguvu, 5% waliyapata lakini hawakupata kazi walizoziomea, 5% waliishia kuwa deported,

lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what I did, I can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu,

Nimependa hii (ingawa umetoa full pointi kwenye jibu lako).
 
Kithuku samahani nisingeweza kueleza vizuri kwa kiswahili baada ya miaka kumi na moja na sua sua na misamiati.

Duh hii kali,kama kweli pole vinginevyo una kind of personality disorder and defending mechanism unayotumia kuonyesha your not inferior is to make the use of english language.
But I get knew for you fellow ;english is just language like other language where we have all kind of people speak this language ie.intelligent people,lazy people ,crazy people ,pathological liars,paranoid ...etc. So Attitude which is all what we need here has nothing to do with language.Nobody take you as special for english.
By the way hoja yako uliyoweka ni nzuri sana nimeipenda na unaweza kutumia lugha yoyote hali ukiona unaowapelekea ujumbe watakuelewa nadhani ndivyo tulivyo jifunza kwenye Communication skills ,umetumia english kwangu sawa tu but dont tell me you good in english than you do in Kiswahili it is disgusting since its your first language.Misamiati gani uliyohitaji kwenye poster yako ya kukushinda damn!
 
Mkuu Field Marshall ES

Hiyo makala yako hili kuwasaidia vijana wa Bongo ingetakiwa ichapishwe katika baadhi ya magazeti hili iweze kusaidia vijana wenye mawazo mbali mbali kabla ya kwenda nchi za kigeni na pia jinsi ya kufanikiwa mahala popote duniani hata Bongo.

Kwa asimilia mia moja na ishirini, ni ukweli mtupu.

Kupata SOMO(SHULE) siyo lazima uende darasani na ndio maana baadhi yetu ukipoteza siku hujasoma kwenye board hii unajihisi kama kuna kitu umepoteza
 
Heshima yako Mkuu FMES,
Shule uliyomwaga hapa si ya kitoto naiunga mkono 100%. Kama alivyoshauri Kakindomaster ingekuwa vizuri ikachapishwa kwenye magazeti yetu wengi zaidi wakanufaika nayo.
 
Mkuu Kamundu, heshima mbele nia ya mada yako ni njema sana, isipokuwa tu una ka-bias flani hivi against baadhi ya wabongo walioko US, na pia hujaona mengi sana duniani, lakini ninaheshimu kuwa nia yako bado ilikuwa njema, But:-

1. Ni lazima kuelewa sababu kwanza iliyomfanya mtu kwenda US in the first place, halafu pia uwezo wa yule mtu kufikiri, exposure aliyonayo kimaisha, anatokea maisha gani bongo, maana elimu sio kila kitu, nikiwa na maana kuwa Us kuna wa-Mexico, wanauza maua tu njiani na wanatuma hela kwao kila siku na wana maisha kuliko Blacks wengi wanaolipwa mishahara mikubwa!

2. Si kweli maneno uliyosema as a general ststement, isipokuwa kuna some isolations ishus, lakini most of the times wa kulaumiwa ni wabongo wenyewe kwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu maisha, mazingara walikotoka na mazingara waliyomo sasa, yaani ya US, wengi wanaenda kule na mawazo kuwa bado wako bongo off course maisha yatakuwa ni magumu hata uwe na elimu, hivi unajua ni wamarekani wangapi wenye degree na wanaendesha tax na wana maisha bora na ya uhakika? West Africans wako kibao, wanaendesha tax na wana elimu nzito, lakini ukiongea nao watakwambia kuwa the best decision they ever made katika maisha yao ilikuwa kusoma na kufanya kazi wanayo fanya walipo yaani kuendesha tax.

3. Wa-Tanzania tunasumbuliwa sana na kasumba ya waingereza, ya kufikiri kuwa ni lazima uvae suti kwenda kazini ili uwe na maisha mazuri, ukweli ni kwamba US kuna ubaguzi mkubwa sana, kazi za elimu na malipo makubwa zimetengwa kwa ajili ya wazungu kwanza, halafu weusi wachache kwa ajili tu ya ku-balance na kuwa politically correct on corporate side, lakini hizi kazi sio kwa wageni, hizi ni facts ambazo ni lazima uzifahamu kwa undani kabla hujaenda US kuishi, ukiwa umesoma au hukusoma it does not matter!

4. Kabla ya ku-make a final decision ya kwenda kuishi US, kama inawezekana jaribu kutembelea na nchi zingine kwanza hata Kenya tu ukasafishe macho, sio unatoka Kigoma na Bukoba, pruuuuu stop ya kwanza US, hata Dar'Salaama unapita tu kwenda airport, wengine wanapandia ndege Kampala, I mean unategmea nini huko Us kila kitu kitakuwa maajabu tu, yes ninasema hivyo kwa sababu nimeishi US 20 years, tena yote New York kwenye mambo yote kwa hiyo siongei hadithi ila ninaongea reality, wabongo huenda huko macho juu mno, wengine hata kazi hawajawahi kufanya inawachukua at least miaka mwiwili ya kwanza kutulia chini na kuanza kufikiri maan muda wote huo uliopita mnaona jamaa yupo tu kumbe bado analewa na ulaya, kutoka Mlimani na degree peke yake hakuwezi kukufanya ukaishi "unavyotaka" au "Ulivyotegemea" US,

5. Binafsi kabla sijaamua kwenda US, nilikuwa nimeshatinga melini in the process ya kazi hiyo nilipata bahati ya kutembela almost dunia nzima, kwa hiyo I had an-idea ni nchi gani inafaa kwenda kuishi kwa ajili ya kutafuta maisha na yanawezekana, guys hakuna nchi kama USA, that is it hata kama huna papers, bado maisha yake sio sawa na nchi yoyote duniani, yes I said nitajie nchi unayodhani ina maisha mazuri kwa mbongo hata kwa asiyekuwa na makaratasi, na elimu kama USA? Kama ukishindwa kuyaweza maisha US basi wewe huwezi mahali popote, tena ukirudi bongo utakufa mapema sana, lakini msilaumu nchi wala maisha!

6. Wabongo muache kudanganyana kuhusu USA na ulaya kwa ujumla, nimewaona wabongo wengi sana kule US, wengi wao hata ile idea ya kwa nini wameeenda kule hawana kabisa, I mean absolutely no clue, wavivu, wazembe, at one time mimi nimewakaribisha jamaa ndio kwanza wameingia toka bongo, ninafanya kazi masaa 16 kwa siku kuanzia J'matatu mpaka Jumapili, Ijumaa na jumamosi jioni ninapiga disco kwenye club, nikitoka pale ninaingia kazini moja kwa moja, wao wanajimwaga tu mangoma na kufanya kazi masaa manane tena madukani, na kunishangaa mimi kuwa ninajitesa sana, ebo! wewe ndio kwanza umeingia nchi ya watu huna lolote, ni lazima ukazane kwanza ili ujiweke sawa, baadaye ndio utatulia na kutafuta kazi unayoitaka, au ya shule, lakini lazima uwe na msingi mzito kujua kufanya kazi kwa bidiii, kwa sababu hata kama ukipata hiyo kazi ya elimu kama huna work ethics, ni bure, sasa yes maisha yatakuwa magumu sana huko majuu, maana kwanza utaridhika mapema na chochote unachopata badala ya kuhangaika,

7. Mabadiliko ya maisha hayaji kwa bahati mbaya au nzuri, yanakuja kwa kuhangaika, ukifika kwanza unaaanzia chini hata kama umesoma, hiyo ni sheria ya kwanza ambayo watu wa West Africa wanaielewa sana kuhusu US, then pole pole unaaanza kujifunza mazingara, huku ukitafuta kusonga mbele, regardless ya makaratasi, ukiona mtu analilia makaratasi mapema ujue ni mviovu huyo, wakuu ngoja niwaambie ukweli wabongo niliowaona nilipokuwa US, waliokuja na kudai wanatafuta makaratasi kwanza, 80%, walishia kurudi bongo kwa kushindwa maisha, 10% waliishia jela kwa kujaribu kutafuta papers kwa nguvu, 5% waliyapata lakini hawakupata kazi walizoziomea, 5% waliishia kuwa deported,

lakini 99.9%, ya wale wabongo waliokwenda kuchapa kazi ili wajiondoleee umasikini wao ambao wanaujua wenyewe, walifanikiwa sio tu maisha mazuri, but in the process za kuhangaika waliishia hata kupata makaratasi, ambayo wengi wao yalijileta yenyewe kwa njia mbali mbali wao wakiwa wanahangaika na maisha, and that is exactly what I did, I can go on and on kuhusu wabongo na kutokuwa serious, kutoelewa, kutojishughulisha, halafu kulaumu tu majuu,

Naomba kwa sasa niishie hapa, hakuna nchi njema duniani kama USA, usome usisome it does not matter, lakini ni lazima uwe umekwenda for the right reasons, na uwe the right person, US na Ulaya, sio kwa kila mtu, halafu kama ulishindwa maisha bongo hata kidogo tu basi uwezekano wa kutofanikiwa majuu ni mkubwa sana, kama umekwama uliza wengine wakusaidie, tuache uvivu na uzembe wa kufikiri, mind is a terrible thing to waste maana popote utaishia kuchekesha tu, kabla huja-give up uliza kwanza acha kitu wa-giriki wanaita egoooooo(Ego) na pride zisizokuwa na msingi, be humble na kubali kuelimishwa, lakini usiruke tu na conclusion especially a sensitive kama hiii, kwa wale walioko bado hapa bongo wanataka kwenda huko ninawaambia kuwa huko US ni safi na hakuna noma yoyote!

Ahsante Wakuuu!

Mkuu FMES,

Naona ulichoandika hapa ni msahafu na mimi nitakuwa naitumia kuwapatia vijana wote wanaotaka kuja Ulaya au USA.

Yaani haka ni kakitabu kadogo ka maisha. Ulichosema mkuu hapa ni nyundo kichwani yenye ukweli wa asilimia 100.

Tunahitaji mawazo mengi kama haya kwa faida ya vijana.
 
Back
Top Bottom