Edo Kumwembe na mhariri Mwananchi muwaombe radhi wakazi wa mkoa wa Mara

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
EDO KUMWEMBE NA MHARIRI MWANANCHI MUWAOMBE RADHI WAKAZI WA MKOA WA MARA

Nimesoma Makala ya Edo Kumwembe, ijulikanayo kama UCHOKOZI WA EDO, kwenye ukurasa wa 22 wa gazeti la Mwananchi, toleo na: 6938 (ISSN 0856-7573) la Tarehe 5 Agosti 2019, yenye kichwa cha habari: MKOA WA MARA NITAENDELEA KUUSIKIA REDIONI.

Katika Makala hii fupi, Mwandishi Edo Kumwembe ametumia visa kadhaa vya uhalifu vinavyotokea mkoa wa Mara kuhoji je Mkoa wa Mara uko Tanzania?, akaendelea kuandika “kwa nini watu wake wako hivyo? Pia kaandika “Kila unapofungua redio au televisheni kusikia taarifa ya habari unakutana na mambo mawili. Kama sio kukamatwa na bangi, basi utasikia mauaji yaliyohusisha silaha kali ama panga au mshale. Mara imekwama wapi?”.

Pia katika hitimisho la Makala yake kaandika “Kuna mikoa sijawahi kugusa hii nchi. Mara, Singida, Tabora, Kigoma, Rukwa na michache mingineyo. Natamani siku moja nifike nifanye utalii wa ndani. Hata hivyo kati ya mikoa yote hii, naomba mkoa wa Mara niendelee kuusikia redioni tu kuutazama katika televisheni, naomba wageni mnaokwenda huko mniwakilishe”. Mwisho wa kunukuu baadhi ya sehemu katika makala hii.

Ukiisoma makala hii, utagundua kuwa Edo Kumwembe, kwa kukusudia au kwa bahati mbaya lengo kubwa la makala yake ni kuwaonyesha Watanzania na watu wengine wa dunia kuwa mkoa wa Mara kwanza haustahili kuwepo Tanzania, ama tabia zinazofanyika hazipatikani sehemu nyingine Tanzania, hivyo unakosa sifa ya kuwepo ndani ya Tanzania. Lakini pia kamaanisha kwa nini watu wake wako hivyo? Tafsiri yake rahisi ni kuwa watu wote wa mkoa wa Mara ni katili, wakamatwa na bangi, na wauaji, je huu ndio ukweli kuhusu mkoa wetu?

Pia katika hitimisho Edo kaandika kuwa yuko tayari kutembelea mikoa yote ila sio mkoa wa Mara, yeye kama mwandishi ambaye maandishi yake yanasomwa na watu wengi, wengine miongoni mwao wanakusudia kuutembelea mkoa wa Mara kwa ajili ya Utalii (Butiama, Serengeti n.k), Biashara, Makazi, Elimu, au shughuli za kijamii kama kuoa/kuolewa na nyinginezo. Maana yake ni kuwa anawapa hawa watu tahadhari kuwa mkoa huu haufai kutembelewa na watu wake sio watu wema.

Akumbuke mbuga ya Wanyama kubwa Afrika nzima ni Serengeti, moja ya mapato makubwa kwa Taifa na Mkoa kwa ujumla ni hifadhi hii ya Serengeti, anapotokea mwandishi asiye na maarifa ya kupima anachoandika na athari zake kiuchumi, kijamii ni hatari sana kwa umoja wetu kama Taifa, hali inayoonyesha ubaguzi wa waziwazi dhidi ya jamii ya sisi watu wa mkoa wa Mara.

Je ni kweli kila unapofungua redio utakutana na habari za mauaji na kukamatwa na bangi pekee? Huu ni upotoshaji wa wazi na huenda mwandishi huyu ana malengo makubwa kuutangaza mkoa huu kama sehemu isiyofaa hapa Tanzania. Kama jamii ya watu wa mkoa wa Mara wasingekuwa na habari yoyote njema, au isingekuwa na watu wazuri au wema je ingeweza kuzaa, kuzalisha, kulea na kumkuza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa letu, na mtu aliyepigania usawa duniani, na kuendesha harakati za ukombozi wa nchi mbalimbali toka Utumwani na kutawaliwa na Wakoloni? Kiongozi ambaye hadi leo kanisa la Roman Catholic limemtangaza kuwa ni Mwenye Kheri na wana mchakato kumfanya kuwa miongoni mwa Watakatifu wa kanisa lao (kwa mujibu wa taratibu zao).

Juzi limetokea tukio baya, la mtu kumuua mkewe hadi kumchoma kwa moto, je tukio hili limefanywa na mtu wa mkoa wa Mara? Laiti lingefanywa na mtu wa mkoa wa Mara basi Edo na watu wenye nia kama yake wangeandika makala kwa mwaka mzima kuhusu tukio lake. Je ukatili wa kijinsia au wa aina yoyote kwa hapa Tanzania hufanyika tu mkoa wa Mara? Jibu ni rahisi tu kuwa hapana. Uhalifu wa watu katika jamii hauwezi kuubinafsisha uwe wa mkoa mzima au wa watu wote wa mkoa wa Mara.

Tumewahi sikia matukio kama ya uchunwaji wa watu Ngozi mkoa wa Mbeya, lakini hakuna aliyeandika huu mkoa je upo Tanzania na pia haufai kutembelewa. Hivi juzi kulikuwa na wahuni wanachinja Watoto huko Njombe, hakuna aliyesema watu wa Njombe wa namna gani au kuhoji kuwa kweli mkoa huo uko Tanzania? Yametukia matukio mabaya katika baadhi ya mikoa kama mauaji ya Vikongwe na wenzetu wenye ulemavu wa Ngozi, matukio ambayo ni mabaya na sijawahi sikia yakitokea mkoa wa Mara, lakini sikumuona Edo au mwandishi yeyote kuyahusisha matukio haya na watu wote wa mikoa hiyo wala kuhoji je mikoa hiyo iko Tanzania?

Kiufupi nikuelimishe ndugu Edo, uhalifu upo dunia nzima, ndio maana kuna majeshi, mahakama, pia magereza. Nchi ya Marekani kwa mfano, kwa mwaka huu matukio ya matumizi ya bunduki, toka Januari hadi Agosti 6, matukio ya watu kupigwa risasi ni 33,307, idadi ya vifo ni 8,837, majeruhi 17,489, Watoto waliojeruhiwa au kuuwawa (umri 0-11) ni 396, vijana miaka 12-17 waliouwawa kujeruhiwa ni 1,813. Chanzo (www.gunviolencearchive.org) haya ni matukio ya mwaka huu tu na bado haujaisha katika taifa kubwa la Marekani, lakini hakuna mwandishi wa huko anayesema Marekani sio sehemu salama ya kuishi. Hii ikujengee uwezo na uelewa juu ya matukio ya uhalifu duniani, na hapa nimekupa mfano mmoja.

Kwa kuwa hauna uelewa kuhusu mkoa wa Mara, kwanza ningependa kukuelimisha kuwa watu wa mkoa wa Mara ni wakarimu, wenye akili, wachapa kazi, wenye upendo, wasio wanafiki, wasiopenda kujivuna, waaminifu, wanaoipenda nchi yetu, na kwa ujumla wenye sifa njema tofauti na ulivyotaka kuwajengea watu hofu kuhusu kuutembelea mkoa wa Mara. Pia mkoa una mambo mengi mazuri, uoto wa asili, Mto Mara, madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu na mengine, mbuga za Wanyama Serengeti, Ziwa Victoria, Utalii ikiwepo mahali alipozaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere n.k. Hivyo ni mkoa uliobarikiwa na Mungu, tuna ardhi yenye rutuba na kwa mwaka tunalima hadi mara tatu, hapa ni kwa ufupi tu.

Pia nakukaribisha utembelee mkoa wa Mara, ila pia kama utaendelea na moyo wako wa kibaguzi hata usipokuja hakuna utakachokipunguza maana mkoa wetu kwa nyakati tofauti umetembelewa na Watanzania toka sehemu mbalimbali za nchi yetu na viongozi wa nchi mbalimbali duniani. Mkoa wetu umepokea watu maarufu waliokuja kutembelea hifadhi ya Serengeti, watu mashuhuri kama David Beckam, Will Smith, Nicole Isaacs, Terrence J, Bill Gates, Justin Timberlake, Jessica Biel, Oprah Winfrey, Steadman Graham, George Clooney, Amal Alamuddin, Naomi Campbell, Tom Cruise, na wengine wengi.

Hitimisho, kama kicha cha makala hii, kama mkazi na mtu wa Mara nakutaka kwa uzito ule ule ulioutumia kuandika na kwenye kurasa yako utuombe radhi watu wa mkoa wa Mara, ninakupa siku 7 kutoka leo kufanya hivyo wewe, pamoja na Mhariri wa gazeti la Mwananchi ambaye ameruhusu makala kama hii yenye malengo ovu na ya kibaguzi kuchapishwa kwenye gazeti lake. Baada ya siku hizo kupita bila kufanya hivyo nitachukua hatua stahiki dhidi yako na gazeti la Mwanachi.

Mwandishi wa Makala hii ni:
Jina: Deo Meck
Email: dmecky@hotmail.com
Simu: +255715481628
 
nimesoma hiyo makala ya eddo nikabaki nashangaa,hivi mamlaka husika hazilioni hili gazeti wakalifungia?yani serikali ya mkoa inatumia pesa nyingi kuwashawishi investors kuwekeza mkoa wa mara huku kuna mataahira mengine yanahamasisha watu wasiende mara!
kumbe yule jamaa kichwani empty kabisa.
 
Edo yupo sahihi.Coverave ya taarifa za mkoa wa Mara zimepungua kwa kuwa saizi Camera zote zimehamia ikulu na kwenye ccm.matukio ya maana yanayojitokeza nchini hayapewi kipaombele.Naamini bado Mara matukio hayo yapo ila hayaripotiwi kama awamu ilopita.
Lakin hakuna mkoa au watu ambao ni purely perfect.Mkoa wa Mara lazima wakubali kubadilika,hata sisi wa mikoa Mingine tuna la kujifunza zuri tu kutoka Mara.Ila mkiambiwa mabaya yenu msione ni tusi maana ni kawaida yenu ninyi sisiemu mkiambiwa ukweli mnaona kama ni tusi lakin sio tusi.
NB:maneno ya edo yanaweza kuwa na udhaifu lakin 90%ni kweli tupu
 
Watanzania wengi wanasumbuliwa na ugonjwa ujulikanao kama CGD (Chronic Generalization Disorder) yaani ni hali ya kutumia mtu/watu wachache kama reflection ya jamii nzima kuhusu tabia fulani hasa ikiwa ni mbaya.

Edo kumwembe anahoji kwanini watu wa mkoa wa mara wako hivi akimaanisha kwamba ni wakatili/wasiojitambua anasahau kuwa huo huo mkoa wa Mara ndio umemtoa mtu aliyeongoza harakati za kulikomboa taifa hili kutoka kwenye mikono ya mkoloni. Leo hii ana huru wa kuandika pumba kadri anavyojiskia sababu za juhudi za mwana Mara!

Halafu eti huyu ni mmoja wapo ya influential people waliopo nchi hii
 
Edo yupo sahihi.Coverave ya taarifa za mkoa wa Mara zimepungua kwa kuwa saizi Camera zote zimehamia ikulu na kwenye ccm.matukio ya maana yanayojitokeza nchini hayapewi kipaombele.Naamini bado Mara matukio hayo yapo ila hayaripotiwi kama awamu ilopita.
Lakin hakuna mkoa au watu ambao ni purely perfect.Mkoa wa Mara lazima wakubali kubadilika,hata sisi wa mikoa Mingine tuna la kujifunza zuri tu kutoka Mara.Ila mkiambiwa mabaya yenu msione ni tusi maana ni kawaida yenu ninyi sisiemu mkiambiwa ukweli mnaona kama ni tusi lakin sio tusi.
NB:maneno ya edo yanaweza kuwa na udhaifu lakin 90%ni kweli tupu

usikute wewe ni mtu wa Kaskazini
unadhani Mara ni makabila mangapi yapo huku?
Kishule, kikazi n.k
Hiyo migodi ya North Mara unajua makabila mangapi yapo hapo?
unasupport ujinga tu
wengine hadi wameoa na kujenga huku huku

Mkoa wa Mara
Wilaya moja tu Tarime inazidi mkoa wa Dsm kwa ukubwa wa Eneo

Huwezi tumia tabia za Waroma kuwasema wakristo wote
(coz humo kuna walokole, wasabato, walutheri,n.k)
Pia
Huwezi kutumia tabia za wamachame kuwasema wachaga wote
(coz humo kuna wamarangu, warombo, kibosho, n.k)

Mkoa wa Mara siku zote nitaupenda
Very proud kuzaliwa Mara
Huu ndiyo mkoa wangu
 
wewe na huyo Edo ni wapuuzi tu
wajinga fulani
usikute wewe ni mtu wa Kaskazini
unadhani Mara ni makabila mangapi yapo huku?
Kishule, kikazi n.k
Hiyo migodi ya North Mara unajua makabila mangapi yapo hapo?
unasupport ujinga tu
wengine hadi wameoa na kujenga huku huku

Mkoa wa Mara
Wilaya moja tu Tarime inazidi mkoa wa Dsm kwa ukubwa wa Eneo

Huwezi tumia tabia za Waroma kuwasema wakristo wote
(coz humo kuna walokole, wasabato, walutheri,n.k)
Pia
Huwezi kutumia tabia za wamachame kuwasema wachaga wote
(coz humo kuna wamarangu, kibosho, n.k)

Mkoa wa Mara siku zote nitaupenda
Very proud kuzaliwa Mara
Huu ndiyo mkoa wangu
Umejibu kwa hasira chief pole sana

Kunywa maji kidogo chief

Kuna siku nilikufa kisa kubishana hivi hivi
 
Umejibu kwa hasira chief pole sana

Kunywa maji kidogo chief

Kuna siku nilikufa kisa kubishana hivi hivi

Kweli rafiki yangu nimeudhika sana
Hahaha sawa wacha ninywe maji
Ahsante
But mtu kuusema mkoa wangu vibaya
au wilaya hata kijiji dah naumia sana
coz watu wasiwe wanapenda ku-generalize vitu
sasa Jamaa anasifia ujinga

Mikoa kibao ina mabaya zaidi but hatuisemi coz watu wa Mara huwa hatuna huo muda wa kijinga
au kisa watu wa Mara hawasemi ujinga na uovu wa mikoa mingine ndiyo maana?
NA
watu wa Mara kibao wapo mikoa mingine
na hao wa mikoa mingine nao kibao wamejaa hapa Mara
 
Nshawahi kaa mara mzee

Kuko poa sana

Ila mzee alkua ananiambia saa kumi na mbili niwe ndani

Wayback zaman sana
 
Hawezi kuandika mambo ya ajabu juu ya mkoa wa wastaarabu, mkoa usiopenda bugudha. Huu ni mkoa ambao una mbuga kubwa nchini lakini mamlaka inayosimamia hiyo mbuga ipo mkoa jirani wa kaskazini na watu wa mara wametulia tu. Au huo ndo ujinga wao. Na hii wilaya ya SERENGETI haina hata kilomita moja ya lami.Huo ndo ujinga wa watu wa mara. Huuu ni moa uliotoa rais wa kwanza wa nchi hii na hata barabara inayoenda nyumbani kwa raisi huyo aliyengatuka mwa 1985 ndio inawekewa lami sasa na haijakamilika. Huu ndo mkoa unatoa watu mashujaa. Kuna majerali wanne wako pale wamestaafu kwa heshima . Halafu kajitu kanakuja kusema vibaya huo mkoa.
Eddo waombe radhi watu wa mara haraka
 
Inawezekana mada ina makosa na ina hoja za kugawa watu.

Lakini Edo na gazeti wana haki za kikatiba za kujieleza.

Kama huoendi, susia gazeti. Ndivyo mfumo wa siko huria unavyofanya kazi. Gazeti likikosa wa kulinunua kwa sababu hii kitajirekebisha au kufa.

Kama wamevunja sheria, wafungulie kesi mahakamani. Ndivyo mfumo wa utawala wa sheria unavyofanya kazi.
 
nimesoma hiyo makala ya eddo nikabaki nashangaa,hivi mamlaka husika hazilioni hili gazeti wakalifungia?yani serikali ya mkoa inatumia pesa nyingi kuwashawishi investors kuwekeza mkoa wa mara huku kuna mataahira mengine yanahamasisha watu wasiende mara!
kumbe yule jamaa kichwani empty kabisa.
Duuh na huyu nae mwataka apewe kesi? Kuweni na huruma hata chembe
 
Edo yupo sahihi.Coverave ya taarifa za mkoa wa Mara zimepungua kwa kuwa saizi Camera zote zimehamia ikulu na kwenye ccm.matukio ya maana yanayojitokeza nchini hayapewi kipaombele.Naamini bado Mara matukio hayo yapo ila hayaripotiwi kama awamu ilopita.
Lakin hakuna mkoa au watu ambao ni purely perfect.Mkoa wa Mara lazima wakubali kubadilika,hata sisi wa mikoa Mingine tuna la kujifunza zuri tu kutoka Mara.Ila mkiambiwa mabaya yenu msione ni tusi maana ni kawaida yenu ninyi sisiemu mkiambiwa ukweli mnaona kama ni tusi lakin sio tusi.
NB:maneno ya edo yanaweza kuwa na udhaifu lakin 90%ni kweli tupu

yaani unasema mara ni CCM !!!! hebu taja ni mkoa gani Tanzania kuna wabunge watatu wa CHADEMA ukiacha Mara. makamasi unamjua John Heche, unamjua ESTER MATIKO , unajua ESTER AMOS BULAYA unajua wanatokea mkoa gani? Hebu acha dharau
 
nimesoma hiyo makala ya eddo nikabaki nashangaa,hivi mamlaka husika hazilioni hili gazeti wakalifungia?yani serikali ya mkoa inatumia pesa nyingi kuwashawishi investors kuwekeza mkoa wa mara huku kuna mataahira mengine yanahamasisha watu wasiende mara!
kumbe yule jamaa kichwani empty kabisa.
Pale juu si wameandika UCHOKOZI WA EDDO???
Sasa unakasirika nini?
 
Mshaambiwa uchokozi wa Edo. Mnapanick nini? Si mnapenda kusifiwa wazaliwa wa mkoa wa mara, basi mkubali na kasoro zenu. Huo ni uchokozi, kama vipi nanyinyi kaanzisheni uchikozi wenu.

Tuwasifu tu kisa Nyerere alitoka huko? Nyerere alikua Mkurya kama nyie mnaolialia hapa?

Hehehehee amang'ana muraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu usiwatafutie watu ban bure hapa, huu mkoa ndiyo Engine ya Taifa, mkoa wenye watu wasiopenda ujinga , mkoa tajiri kirasilimali, mkoa wenye baraka zote na umetoa viongozi makini kabisa nchini. Sasa sijui hiyo Mara yako ni ipi?
Nasisitiza Mara ndiko kuna wapumbavu wengi zaidi.. hawatumii akili kwenye maamuzi yao..
MF. SIRRO, LUGOLA
 
Back
Top Bottom