Edo Kumwembe: Kesi ya Chriss Kope Mutshimba Mugalu ni ngumu, anahitaji kuvumiliwa

Mugalu Kuna kitu anapitia so bure.

Lakini Kuna goli alikosa akiwa na kipa ,Hilo forward yoyote angeweza kukosa!

Pale kipa wa Vita alipunguza Holi...kimsingi pale ilikuwa no uhodari was kipa!

Alichotakiwa kufanya Mugali ni kumpa aliyekuwa kushoto jwake afunge!

Hii ninkea mujibu uzoefu wangu was soka was darasa la tatu!
Unamaanisha zile kosakosa za kujirudia ambazo alitakiwa tu kujifunza trick ya kuuchop mpira past a goalkeeper
 
Japo haujaniuliza mimi, naomba kukuuliza kitu pia, wewe una nini na Mugalu, mbona unaumia sana anaposemwa vibaya? Kila thread wewe unamkingia kifua, huoni kasoro zake kabisa.
Kwa sababu najua ni mchezaji mzuri na kwenye mpira hiyo kila mchezaji anapitia, kama Messi au aubameyang anakaa mechi 7 hajafunga ye Mugalu ni Nani? Au ukiskia Messi hajafunga mechi 7 unazani waga hapati chances za kufunga?

Mugalu hakuwa hivo na uwezo wake unajulikana ndomana kocha bado anaendelea kuwa na Imani nae, mpira ni mchezo wa psychology, the way mchezaji anakuwa mentally fit ndo jinsi anavopafom uwanjani, mchezaji akiyumba kidogo Tu psychological anapotea mazima maana anacheza na pressure ya nje ya uwanja

Me namtetea kwakuwa najua class is temporary Ila class ni permanent, uwezo aliokuja nao Mugalu sio huu hivo kujiamini kumepungua lakini pia hatuwezi jua nini anapitia, mlio wengi mnamjaji Mugalu kishabiki maandazi na sio kimichezo, na uzuri ni kwamba anatimiza majukumu ya kocha ata kama hajafunga na kocha anataka kumpa confidence upya ili awe clinical tena, kumpiga bechi sio dawa. Nazani nimeeleweka

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
ALIPOFIKA nchini mtu mmoja wa Simba alininong’oneza kitu kuhusu mshambuliaji anayeitwa Chris Mugalu. Aliniambia; “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”. Hii ilikuwa kauli ya kurahisisha kwa mtu anayetaka kumjua Mugalu.

Niliambiwa kuwa aliyesema hivyo ni kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri ambaye huwa anawasaidia watu wa Simba kuwajua wachezaji waliowahi kucheza soka katika ardhi ya Zambia. Kumbuka kwamba Phiri yupo Zambia kwa sasa.

Mechi zake za kwanza nchini niliamini kilichosemwa. Alifunga mabao maridadi ya mshambuliaji halisi. Ungeweza kuamini kwa urahisi. Nilijua kwamba Simba ilikuwa imepata mtu ambaye anaweza kuwaweka benchi Bocco na Kagere.

Lakini sasa Mugalu huyu sio yule aliyefika nchini. Watu wa Simba wanamzomea. Anapitia wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote ule. Anatia huruma. Hata yeye mwenyewe anaonekana kuchanganyikiwa. Anakosa mabao ya wazi kupitiliza. Pambano la Simba dhidi ya Vita aligeuka kuwa kichekesho uwanjani baada ya kukosa mabao mengi ya wazi kisha akaondolewa.

Nyakati kama hizi kichwa cha Mugalu kinakuwa na mambo mawili. Kwanza kabisa kichwa chake kinakosa kujiamini. Mshambuliaji akikosa mabao ya wazi tena na tena anajikuta haamini tena katika uwezo wake, wakati mwingine anaogopa hata kujaribu kupiga.

Kwa wazungu, mshambuliaji wa aina hii huwa wanapambana na kichwa chake. Wanajaribu kumrudishia uwezo wa kujiamini ndani na nje ya uwanja. Wakati mwingine anapewa hata penalti yoyote inayotokea uwanjani ili mradi afunge kwa urahisi na aweze kujiamini tena.

Lakini kuna jambo jingine. Katika kichwa cha Mugalu kwa sasa anaweza kuwa anaamini kuwa amerogwa. Mara nyingi inatokea kwa wachezaji wa Afrika hasa wale ambao wanafika katika nchi kama Tanzania na kusikia simulizi hizi kutoka kwa mashabiki au wachezaji wakiwa kambini.

Hili la pili siliamini sana ingawa lipo na inasemwa kwamba hata katika vitabu vya dini imeandikwa kwamba uchawi upo. Sisi wengine sio kazi yetu kuamini katika hili, tunachojua ni kwamba ikitokea Mugalu akafunga bao moja tu basi ari ya kujiamini itarudi kwake.

Hauwezi kuwa mchezaji mbovu au mzuri kwa usiku mmoja. Haiwezekani Mugalu niliyemuona mimi katika siku za kwanza ghafla akawa mchezaji mbovu. Kuna washambuliaji walikuja nchini na tukajua kwamba hawana lolote kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho. Mmojawapo ni Yikpe.

Kile kiwango cha Mugalu wakati anafika hakikuwa cha bahati mbaya. Kile ndio kiwango chake halisi. Nadhani hata Simba walitumia pesa nyingi kumnasa baada ya kumchunguza na kujiridhisha kwa kauli ile ile niliyosema hapo juu kwamba “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”.

Kinachotakiwa kwa watu wa Simba kwa sasa ni kuendelea kumjengea imani. Inabidi wamshangilie kwa nguvu kwa namna yoyote ile. Wakati mwingine huwa tunawaua wachezaji wazuri kwa sababu ya kukosa busara. Hii ni kuanzia kwa mashabiki hadi viongozi.

Mchezaji wa aina ya Mugalu ni wa kupewa moyo na sio kuzomewa. Ni mchezaji wa kupigiwa makofi hadi anapokosea. Atakapoona watu wa Simba wamesimama nyuma yake ndipo uwezo wake wa kujiamini utakaporudi.

Vinginevyo kuna minong’ono mingi kwamba huenda Simba ikasaka mshambuliaji mpya. Hauwezi kubadilisha wachezaji kila siku. Hawa washambuliaji huwa wanapitia nyakati hizi na bado huwa wanapewa mikataba mipya. Kitu cha msingi ni kujua tu kwamba mshambuliaji wa aina yake anapokuwa fiti huwa anakuwa ni mchezaji wa aina gani.

Vinginevyo unaweza kujikuta unabadilisha wachezaji kila uchao. Haifai kuwa hivi. Labda kama mchezaji ataendelea kuwa na fomu mbovu kwa misimu miwili unaweza kujikuta katika nafasi ya kuachana naye. Ushauri wangu Simba wasifikirie kuachana na Mugalu kwa haraka haraka. Wafuatilie tu kitu kinachomsibu.

Pale mbele anawapa nguvu kubwa ya umiliki mpira hata kama hafungi. Ukame kama huu alionao huwa wanaupata akina Sergio Aguero, Pierre Emerick Aubameyang, Luis Suarez na washambuliaji wengine mahiri duniani.

Katika usajili wa wachezaji Tanzania nimegundua aina tofauti tofauti za wachezaji. Kuna mchezaji ambaye tangu siku ya kwanza mnahisi kwamba mmepigwa. Huyu ndiye kama Yikpe. Halafu kuna mshambuliaji ambaye anakaa katika uchunguzi zaidi. Huyu ni kama Michael Sarpong.

Kuna mchezaji ambaye anaonyesha makali yake tangu mwanzo lakini ghafla makali yake yanapotea. Huyu ndiye kama Mugalu. Kunakuwa na mambo mengi nyuma yake. lakini pia kuna mshambuliaji ambaye anaanza taratibu lakini baadaye akizoea anakuwa moto. Mfano ni Donald Ngoma.

Ngoma alipokuja Yanga alianza taratibu lakini makali yake yakaimarika kila uchao na baadaye akaibuka kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora nchini. Mwanzoni mashabiki wa Yanga walikuwa wakimfananisha na mshambuliaji wao wa zamani, Idd Mbaga. Baadaye walijikuta wakimuheshimu zaidi.

Hii kesi ya Mugalu ndio ambayo inakuwa ngumu zaidi. Mchezaji anaonyesha makali halafu ghafla anakuwa wa kawaida. Huwa ni kesi ngumu ambayo inawaacha wachambuzi, makocha, viongozi na mashabiki wakiwa hawana majibu ya moja kwa moja.

EDO KUMWEMBE
Sarpong revisited
 
Mugalu kiwango chake ndo hicho na atabaki hivyo hivyo.

Nadhani umri umefika maana ni mzito kama jiwe.

Akifika golini anafumba macho kabisa.

Alipasiwa mpira yeye na goli, mita tano, kipa kasimama, Mugalu akapiga nje karibia na kibendela cha kona.

Mugalu anabebwa na mido za Simba, angekuwa Yanga angesha fungashiwa virago.
Kama yanga wameweza kuwavumilia Ykipe, Sarpong na Nchimbi wangeweza kweli kumfukuza Mugalu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom