- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kuna video inayomuonesha Edna Cintron akipunga mkono akiwa ghorofani baada ya shambulizi la septemba 11, 2001 nchini Marekani je aliokolewa au alifariki pale pale?
- Tunachokijua
- Shambulio la Septemba 11 ni miongoni mwa matukio makubwa yaliyowahi kutokea nchini marekani, tukio hilo la kigaidi lilitokea Septemba 11 mwaka 2001 ambapo washambuliaji wa kujitoa muhanga waliteka ndege nne za Shirika la ndege la Marekani na kuzitumia kufanya mashambulizi kwa kuzibamiza kwenye majengo mawili ambayo ni jengo la kibishiara la World Trade Center maarufu kama Twins towers na jengo la Pentagon, makao makuu ya jeshi la Marekani. Tukio hilo lilisababisha maelfu ya watu kujeruhiwa na wengine kufariki.
Video na picha mbalimbali zilirekodiwa siku ya tukio hilo ambazo zimeendelea kuwa kumbukumbu kwa kile kilichotokea ikiwa ni miaka 23 sasa tangu shambulizi hilo kutokea.
Hivi karibuni kumekuwepo na kipande cha video kikisambaa mitandaoni kikimuonesha mtu akiwa kwenye ghorofa linalowaka moto na kutoa moshi mzito akipunga mkono kuashiria kuhitaji msaada huku taarifa zinazoambatana na video zikieleza kuwa mtu huyo anayepunga mkono ni mwanamke Edna Cintron aliyekuwa akiomba msaada mara baada ya jengo la World Trade Center kushambuliwa 11 Septemba, 2001.
Ukweli upoje.
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia njia ya mtandao na kwa kutumia google image reverse imegundua video hiyo ni ya kweli na imekuwepo mtandaoni kwa muda mrefu sasa mathalani video hiyo inapatikana katika moja ya chaneli za mtandao wa Youtube ambapo iliwekwa miaka 13 iliyopita, video zote hizo zimekuwa zikimtaja Edna Cintron kama mwanamke shujaa aliyekuwa akijaribu kuyaokoa maisha yake baada ya jengo alilokuwepo kubamizwa na ndege na kuanza kutoa moshi mzito ulioambatana na moto siku ya shambulizi katika Jengo la World Trade Center.
Edna Cintron ameelezewa na machapisho mbalimbali kama miongoni mwa watu jasiri waliokua wakiyatetea Maisha yao siku ya shambulizi la septemba 11, katika Jengo la World Trade Center. Tovuti ya gazeti la Daily Mail kwenye Makala yao wamemuelezea Edna Cintron ‘Waving woman who never lost hope’ kuwa ni miongoni kati ya maelfu ya watu wanaokumbukwa katika kumbukizi ya miaka 23 tangu kutokea kwa shambulizi la septemba 11, 2001.
Edna alikuwa mfanyakazi katika katika ofisi ya Marsh & McLennan ambaye picha na video zilimuonesha akiomba msaada kutokea kwenye uwazi uliosababishwa na shambulizi kwenye ghorofa ya 93 katika jengo la World Trade Center upande wa Kaskazini kabla ya Jengo hilo kudondoka na kupelekea Edna kupoteza uhai muda mfupi baada ya jengo.
Mume wa Edna aliyefahamika kwa jina la William Cintron alipokuwa akihojiwa alisema kuwa mkewe alikuwa mwanamke bora sana kwani alikuwa akiijali familia na alikuwa naye bega kwa bega alipokuwa na uraibu wa pombe, Edna alimsaidia mpaka alipoachana na uraibu huo. Mume wa Edna, William Cintron alimtambua mkewe baada ya kuona picha za mwanamke aliyekuwa akipunga mkono katika ghorofa lile kwa kutokana na rangi ya nywele, nguo na uvumilivu wake.
Lakini pia yupo mwanaume mwingine ambaye alifahamika kwa jina la na yeye pia alidai kuwa mwanamke huyo hakuwa Edna bali alikuwa ni mchumba wake huku akidai kuwa nguo alizovaa mchumba wake wakati anaeda kazini siku hiyo ndizo ambazo alizokuwa amevaa mwanamke ambaye alikuwa anapunga mkono akijulikana kwa jina la Karen Juday.