Eddo: Hata Pierre Nkuruzinza na Hussein Rajabu hawakukutana barabarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eddo: Hata Pierre Nkuruzinza na Hussein Rajabu hawakukutana barabarani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by watenda, Oct 20, 2011.

 1. w

  watenda Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana nimemshuhudia Edward Lowassa akiirejea kauli yake ya miaka miwili iliyopita akidai kwamba yeye na Rais Kikwete hawakukutana barabarani, akimaanisha kwamba urafiki wao huo ambao unadaiwa kudumu kwa miongo takribani mitatu na ushee, hauwezi kumalizwa hivi hivi. Maana yake ni kwamba hata akimfanyia hujuma za namna gani, hata akikosa uadilifu kiasi gani, na hata akiwa na sifa mbaya ya uongozi iliyopitiliza hapaswi kuchukuliwa hatua kwa sababu tu hawakukutana barabarani.

  Hili likanikumbusha uswahiba uliokuwa umekolea kati ya Rais wa sasa wa Burundi Pierre Nkuruzinza na mshirika wake Hussein Rajabu ambaye hapa tunapozungumza yuko gerezani akilazimika kwenda haja kubwa na ndogo kwenye ndoo. Hawa walipanga wote kuingia msituni na kuendesha harakati zilizowawezesha kushika uongozi wa nchi, Nkuruzinza akiwa Rais wa nchi na Rajabu akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CNDD-FDD. lakini kwa sababu za kutovumilia kile ambacho Rais alikiona ni hujuma dhidi yake, utawala wake na ustawi wa nchi (kwa maoni ya Rais huyo) alichukua hatua za siyo tu kumvua madaraka ya chama Rajabu na kuwavua uongozi wa kiserikali wafuasi watiifu wa Rajabu, alimfikisha mahakama na kumshitaki kwa mashitaka mbalimbali, yakiwemo ya uhaini na hatimaye kuhukimiwa kifungo jela. Swali: Kama hawa nao walikuwa washirika wa muda mrefu na wa karibu, wakiendesha harakati pamoja na bado hatua zikachukuliwa kwa maslahi ya Taifa, nini kinachomfanya Lowassa adhani kwamba urafiki wao huo usio wa kukutana barabarani ndiyo uwe kinga yake dhidi ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa maovu yanayohusishwa naye?

  Lowassa ajifunze kuelewa yale ya nchi za wenzetu kwani hata Besigye na Museveni walikuwa washirika wa karibu sana toka msituni mpaka ikulu ya Nakasero. Ona yanayotokea leo! Asijidanganye!
   
 2. n

  ndutu Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umempa dozi kali ya mwaka na sisi wengine tuliyasahau mambo haya. Hivi kurejea rejea kauli hiyo ni kumtisha Muungwana au ni nini? Halafu anaunga mkono uasi wa vijana wake wahuni na kuomba eti wasuluhishwe na chama na kutolea mfano wa yaliyotokea wakati ule wa miaka ya 70 wakati hoja za vijana wakati huo zilikuwa za kiitikadi na hakukuwa na uchochezi kama huu wa watu waliopewa fedha ili waasi uongozi wa nchi na kukiuka katiba na maadili ya umoja wao. Jana kathibitisha kwamba kumbe wahune wale wanaoijiita UVCCM wana baraka zake.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kumbe ndio maana akawaita waandhishi wa habari kuongea nao ili mkuu wa kaya akimuona asimuadhibu kweli tz undugu na urafikilization utatuponza..
   
 4. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tanzania, mmmmmhhhhh,, hawawez kufanya hvo!"""""

  Livingston Lusinde- Mwana wa baba

  Nape Nnauye- Mwana wa Baba

  January Makamba- Mwana wa Baba

  Bakar Malima- Mwana wa Baba

  Husein Mwinyi- Mwana wa Baba


  twende kwa urafiki......

  Huko ni balaaaaa, mawazir, wakuu wa mikoa, wakurugenz..........WASHKAJI ZANGUUUUUUUUUUU
   
 5. T

  Tiote Senior Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mna uhakika kwamba kweli huyu jamaa aliitisha mkutano wa waandishi wa habari akiwa nyumbani kwake au akiwa hospitali. Siamini kama waziri mkuu 'mstaafu' na rais mtarajiwa anaweza kusumbua watu halafu asizungumzie mambo ya msingi na kurudia singo yake iliyochuja ya kutokukutana na rais barabarani akaacha hoja zenye mashiko kama Richmond, binti yake Dowans na kuvuliwa gamba. Akawa bize kutisha waandishi wa habari wakati umma unaelewa na wenyewe wakisijifu kwamba wamenunua vyombo vyote vya habari. Anazungumzia vyombo vipi vya habari vilivyobaki? Si avinunue hivyo navyo amalize mchezo ili neno lake liwe kama andiko takatifu? Na waandishi wale waliokodiwa ndege kutoka Dar wakawa pale kama wapagazi, wasijue la kufanya na kuuliza maswali ya kitoto kama mtu aliyeshikwa ugoni. Aibu gani hii!
   
 6. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huo ndo ujamaa unaoimbwa kila kukicha tanzania, na ukizingatia Sheria za nchi yetu hazina menu ni balaa tupu, Pierre wa Burundi alifanikiwa kumtia nguvuni swahiba wake kutokana na kutoendekeza ujamaa usiyo kuwa na maana yoyote ktk maendeleo ya nchi na wananchi hilo wanalitambua. Sisi huku hilo hatuna tunasubiri matukio tu na wala hatuna mipango thabiti ktk kupambana na waarifu wa nchi..
   
 7. A

  Al Adawi Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Mimi nadhani ni Kikwete ndo anayemtuma "wambie hatukukutana barabarani"..
   
 8. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  amesema amechoka kuchafuliwa na kupakaziwa. na kuanzia sasa atachukua hatua. NAONA MOVIE YA URAISI INAANZA.
   
 9. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  mwana wa baba Vita Kawawa ....... Mwana wa baba Edward sokoine....... Mwana wa baba Riz1 kikwete.......
   
 10. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,967
  Trophy Points: 280
  Mie narudia kusema lowassa alikuwa anapima upepo hakuwa na lolote la maana la kusema hawezi kunyea kambi, anaihitaji ccm hiihii kutimiza lengo lake kuwa Rais.Kuhusu kutokutana na kikwete barabarani nafikiri anajaribu kutuambia hata ile nafasi ya Uwaziri mkuu hakustahili alipewa kwa sababu wametoka mbali.Kweli inatisha!
   
 11. n

  ngwini JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bakari Malima mchezaji wa zamani wa Yanga?
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,359
  Trophy Points: 280
  hawakukutana barabarani....lazima walikutana lang'ata au DDC kariakoo enzi hizo.,maana prezidaa kwa kuparty noma..
   
 13. b

  banyimwa Senior Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi anamaanisha kwamba kutukana viongozi wa kitaifa kama Rais na familia yake na wale wote walio na misimamo tofauti na yeye ni jambo linalohitaji kukaliwa kikao na kulijadili? Mbona hakuendesha suluhu kati ya Millya na Ole Sendeka walipoparurana kwenye mkutano alioupanga yeye kule Monduli? Yeye si ndiyo kiongozi wa wamasai hao mahasimu? Kauli hii imebainisha wazi kwamba yanayotokea Arusha yana mkono na baraka zake! Anajifanya kutoa reconciliatory messages ili aonekane ni peace maker kwa vurugu anazoziasisi, kuzifadhili na kuziratibu. Hiyo "Alibi" yake ya kwamba alikuwa nje ya nchi haina mashiko. Alipanga kabla ya kwenda na huko alikokuwa alikuwa akitoa maelekezo!
   
 14. b

  banyimwa Senior Member

  #14
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Au jembe ulaya kwa jina li kimichezo. Huyu beki alikuwa noma hasa katika harakati za kuua mnyama!
   
 15. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Una maana Kikwete Rais? Basi ndugu yangu kapimwe kichwa. Yaani rais abariki kutukanwa na kushambuliwa kwa familia yake, taasisi ya urais na hadhi ya chama halafu amtume muasisi wa hujuma hizo aongee hilo. Nadhani wengi wetu hatumjui Kikwete the President!
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wengi tulishaanza kumsahau na kusahau mabaya na madhila yake kwa uchumi wataifa hili. Sasa kama mtu aliyelogwa vile anatutonesha vidonda hivi. Wacha tu watu wamtandike maana kayataka mwenyewe.
   
 17. M

  Marytina JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  lowassa alikuwa anataka kujivua gamba akatishwa na ikulu ikabidi apige porojo zingine
   
 18. m

  mudavadi Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka mbaali sana! Enzi za mzee wa Mchinga na bendi yake ya Mchinga Sound na wimbo wake wa gunia la misumari. Jamaa anajificha kwenye kivuli cha mpapai wakati wa mvua yenye upepo mkali. Sasa akayafanya yote haya, likiwemo lile la kutaka kumpindua mwenyekiti ili achukue yeye au mshirika wake. Sasa anageuza kwende nje ya nchi kama "kivuli chake cha mpapai" lakini hakitafua dafu maana mvua hii ni cyclonic.
   
 19. m

  mudavadi Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Contradictory! Rais aliasisi hoja ya kujivua gamba. Ikulu ipi imtishe wakati kujivua gamba kwake ni long overdue?
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hata marehemu Mzee Kasela Bantu hakukutana barabarani na Mwl, na ndio aliye mu-introduce mwl kwa wazee wa TAA, lakini mwisho wasiku Mzee Kasela Bantu alitiwa kizuizini asitoke Tabora
   
Loading...