Economic diplomacy: Hivi Tanzania tunataka nini toka China?

Robot tatu ya uzi umeongea mwenyewe kwa kuuliza maswali na kujijibu hii no dalili kuwa wewe ni dalali wa wachina.

China sio nchi nzuri sana kuwekeza sera yao ya madeni ni hatari hasa kwa nchi zetu hizi ambazo hazina intelligence nzuri. Anakukopesha then anakufanyia sabotage ushindwe kulipa deni achukue miundombinu yako.

Nashauri selikari isiwekeze mradi wowote wa kimkakati na China.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mkuu uwekezaji na mikopo ni vitu viwili tofauti kabisa. Hapa tunazungumzia uwekezaji na sio mikopo. Sasa uwekezaji unasababishaje mikopo?

Halafu hata hili suala la kukopa na ku attach mali, kisha unashindwa kulipa mali inachukuliwa, sasa wakulaumiwa ni aliekopesha, au aliyekopa bila umakini? Ndio maana mjadala unauliza ni ni ni tunataka, ili tusije ku claim ambacho hatutaki.

Kwa maoni yako, tunatumia vizuri uhusiano wetu na China? Kama bado, ni vitu gani tunaweza kufanya ili tunufaike zaidi?
 
Mbona jibu Mama alishasema kwenye hotuba yake tunataka ajira kuwe na mzunguko wa pesa...

Ushasema kwamba watanzania tuna misitu na ardhi lakini hatuna mitaji na technology ya kuzalisha kwa wingi na ubora ilituweze kuuza nje na pia tunawasomi ambao hawana ajira, wapo tu ni watazamaji wa matukio ya maendeleo na siasa za dunia...basi sisi tuzidi kuomba Mungu tupate nchi “muwekezaji” atakae tupenda sana atutatulie tulipokwama..maana uwezo sisi hatuna sisi ni maskini....
Mama ashasema, na mimi nimesema hapo nilichosema lakini sio lazima alichosema au nilichosema au atakachosema mwingine kiwe kinajitosheleza. Inawezekana bado kuna mawazo mengine mazuri zaidi ambayo bado hayajasemwa na ndio lengo hasa la mjadala.
 
Hayo yote uliyoyaeleza ni mazuri ila China inataka tenda za ujenzi wa barabara, madaraja, flyovers, majengo na kuchota maliasili tu.
 
Hayo yote uliyoyaeleza ni mazuri ila China inataka tenda za ujenzi wa barabara, madaraja, flyovers, majengo na kuchota maliasili tu.
Mkuu, sio tu kwamba China inataka tenda za ujenzi, kupitia mpango huo wa'belt and road' ambapo China hujenga miundombinu baharini na nchi kavu kuiunganisha China na dunia, Makampuni ya kichina pia ndio hutumika kujenga miundombinu hiyo.

Sasa hiyo ni strategy yao wao kwa sababu wanajua vizuri ni nini wanataka duniani na wanapataje wanachokitaka na wanatekeleza.

Katika muktadha huo, ndio hapo mjadala wa sasa tunataka nini kutoka kwao unakuja. Kumbuka sio jukumu lao wao kutambua sisi tunataka ni ni bali wao wanataka nini na jukumu lao wanalifanya kwa usmart wa hali ya juu.

Kwa hiyo mada hii ni muhimu sana katika mazingira hayo.
 
watu wengi hufikiria kuwa nchi hujengwa na wazawa tu!
Hauwezi ijenga Tanzania sisi wenyewe lazima tuwe na mashirika ya kigeni kikubwa ni kuangalia ni mambo gani ya watu wetu yana takiwa kulindwa!
Uko sahihi sana mkuu. China yenyewe pamoja na ukomunisti wake, ilianza kupata maendeleo baada ya Xioping kuja na sera za kuifungua China kiuchumi na kukaribisha wawekezaji. Uchumi wake ulikuwa kwa kasi zaidi miaka ya 2000's baada ya kuongeza kwa kasi kubwa kiwango cha uwekezaji wa nje na ndani.

Hata sasa China yenyewe ina wawekezaji kibao wakigeni hasa Makampuni toka marekena yakiwemo Apple Na.k.

Kwa hiyo suala la umuhimu wa uwekezaji kwenye uchumi hiyo ni mujarab wala halina utata. Suala tu ni kwa namna gani uwekezaji huo unaweza kuwa na tija zaidi.
 
Leo mnawageuka tena wakomunist wenye sifa ya kutokuwa mabeberu🤷
Unakusudia nini mkuu? Kwa maoni yako unahisi tunanufaika vywa kutosha kutokana na uhusiano wetu ukizingatia nafasi ya China kwenye profile ya dunia kwa sasa? Kama hapana, unadhani kama taifa tufanye nini cha zaidi ili tuweze kunufaika zaidi?
 
Sababu kubwa ya mataifa mengi ya kiafrika kushirikiana na China ni kwa sababu sera ya mambo ya nje ya China inakataa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ni mawazo yangu
 
Sababu kubwa ya mataifa mengi ya kiafrika kushirikiana na China ni kwa sababu sera ya mambo ya nje ya China inakataa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ni mawazo yangu
Pamoja na hilo, unadhani kuna namna tunaweza kufanya ili kunufaika zaidi na uhusiano wetu na nchi ya China ambayo ni fursa kubwa ya soko duniani, kitovu cha teknolojia na uchumi?
 
Back
Top Bottom