Economic diplomacy: Hivi Tanzania tunataka nini toka China?

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mwaka jana, kuna mtafiti mmoja kutoka kitengo cha utafiti wa utekelezaji wa sera za nje za China alituuliza ' hivi Africa inataka nini China?' Akiwa na maana waafrica tungetamani kunufaikaje na diplomasia ya kiuchumi kati ya nchi zetu na China ambayo kwa sasa Inaongoza kwa uchumi,teknolojia na upana wa soko duniani. Ukweli ni kwamba hatukuwa na jibu lililonyooka kwamba ni nini hasa tunataka.

Sasa labda niwaulize wenzangu, hivi ni nini Tanzania tunataka kutoka China?

Ikumbukwe pamoja na mambo mengine, China inatekeleza mpango wake mkubwa wa 'Belt and Road' ambao unahusisha kujenga miundombinu kabambe kupitia baharini na nchi kavu kuiunganisha China na mabara mengine ikiwemo Africa ili kufikisha bidhaa zao sokoni kwa wepesi. Wakati huo huo Africa hakuna cha maana tunachouza China kwenye soko la watu 1.3 b.

Kwa sasa kuna hatua nzuri sana zinachukuliwa kuwashawishi Makampuni ya Kichina yaje kuwekeza hasa kwenye viwanda vizito vya electronics, magari na.k ambapo washakubali kufanya hiyo kupitia kampuni zao zaidi ya 800 ambapo tutapata manufaa mbalimbali makubwa kwa kiasi flani.

Pamoja na hiyo, tunashauri maeneo mengine ya kuimarisha ushirikiano kama ifuatavyo;-

1. Tuone namna ya kuwashawishi waweke mtaji na teknolojia kwenye kilimo, mfano cha soya halafu sisi tunachangia ardhi na nguvu, soko liko China. Kwa hiyo pamoja na watu wetu kupata ajira lakini pia tunakuza uchumi kwa namna hiyo. Kila mtu anatoa kile alichonacho kutengeneza faida.Ikumbukwe kwa sasa USA ndio huuza matani na matani ya Soya China na bado uhitaji ni mkubwa sana.

2. Tuwashawishi wawekeze mtaji kwenye ufugaji nyuki kwa kutoa vifaaa halafu watanzania wanafuga kwenye mapori yetu halafu asali tunauza China. Ikumbukwe tuna mapori ya kutosha na ufugaji nyuki hauharibu mazingira.

3. Tutulie tujiulize hivi tunataka nini kutoka China kwenye soko la watu 1.3 b, Kitovu cha teknolojia na uchumi duniani, kisha tuboreshe sera zetu za nje ipasavyo ili kuweza kunufaika zaidi na uhusiano wetu na hawa rafiki zetu.

Nimalizie kwa kuwauliza tena ndugu zangu, hivi tunataka nini kutoka China?
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kwa maoni yangu, China ni sawa na tajiri alie ibuka katikati ya kijiji cha watu maskini. Sasa badala ya kumuangalia kama kitisho, tunatakiwa kumuangalia kama fursa mpya kijijini na kuona namna tunavyoweza kumtumia kwa akili kulingana na mazingira yetu na kwa faida ya pande zote.

Ikumbukwe kushindana naye hatuwezi maana hata USA imekaa. Ijapokuwa waafrika tuna hulka ya kutamani kushusha walioko juu ili tufanane huku chini badala ya kupandisha walioko chini ili tufanane huko juu, hawa jamaa hatuwezi kuwashusha.

Sasa tunawezaje kushirikiana kwa manufaa ya pande zote, au angalau tukawatumia kupanda kuwafuata?
 

Hechinodemata

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,080
2,000
Mzee vp?, mbona unajiulizahalafu unajijibu sisi tukuelewe vp sasa, au umetumwa na wachina au jobo team
Kwa maoni yangu, China ni sawa na tajiri alie ibuka katikati ya kijiji cha watu maskini. Sasa badala ya kumuangalia kama kitisho, tunatakiwa kumuangalia kama fursa mpya kijijini na kuona namna tunavyoweza kumtumia kwa akili kulingana na mazingira yetu na kwa faida ya pande zote...
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kuhusu manufaa tunayoelekea kuyapata kutokana na hatua zinazochukuliwa kwa sasa tumeyajadili kiasi hapa Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360

Hata hivyo, naona kama bado hatujaitumia vyakutosha fursa ya uhusiano wetu na China. Yaani bado naona ni kama tunaenda kuchota maji ziwani kwa kijiko halafu tunaenda nayo jangwani.

Watanzania tunataka nini kutoka China? Hili swali ni very important. Kuna fursa inatupita hapa.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mzee vp?, mbona unajiulizahalafu unajijibu sisi tukuelewe vp sasa, au umetumwa na wachina au jobo team
Kwani yale maswali ya essay ya kutoka kidato cha 2 kwenda cha 3 yanayokuambia 'discuss' wewe ulikuwa una discuss vipi peke yako?

Kwa maoni yako, unadhani Tanzania tunahitaji nini kutoka China specificaly? Unadhani tunaitumia fursa ya uhusiano wetu na China ipasavyo? ukizingatia China ndio soko kubwa zaidi duniani, ina uchumi mkubwa zaidi na inaongoza kwa teknolojia!?
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
9,611
2,000
Kwa maoni yako, unadhani Tanzania tunahitaji nini kutoka China specificaly? Unadhani tunaitumia fursa ya uhusiano wetu na China ipasavyo, ukizingatia China ndio soko kwa zaidi duniani, ina uchumi mkubwa zaidi na inaongoza kwa teknolojia?
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Ikumbukwe pia msimamo wa China ni kushughulika na Nchi za kiafrika kama watu wazima wenzao. Yaani kuangalia kila mmoja apate 'win win'

Lakini ni muhimu tutambue na kuweka vizuri ni nini hasa tunataka, kwa sababu kwa upande wao, wao wanajua vizuri ni nini wanataka lakini hawawezi kujua ni nini sisi tunataka hasa kutoka kwao.

Aidha, tusipotulia, tunaweza tukawa tuna 'claim' kwato kwenye ng'ombe mzima. Yaani tunapata fursa kubwaaa ila tuna extract kidogoooooo.

Ni kwa muktadha huo tafakuri na mjadala huu unakuwa muhimu sana.
 

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,856
2,000
Kuhusu manufaa tunayoelekea kuyapata kutokana na hatua zinazochukuliwa kwa sasa tumeyajadili kiasi hapa Maono ya Rais mama Samia kuhusu uwekezaji nchini kwenye nyuzi 360

Hata hivyo, naona kama bado hatujaitumia vyakutosha fursa ya uhusiano wetu na China. Yaani bado naona ni kama tunaenda kuchota maji ziwani kwa kijiko halafu tunaenda nayo jangwani.

Watanzania tunataka nini kutoka China? Hili swali ni very important. Kuna fursa inatupita hapa.
Teknolojia, soko la mazao yetu, nidhamu ya kazi.
 

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,486
2,000
Wanakufilisi je mkuu? Any way badala ya nini wewe unashauri iwe nini?

Maana pia tuna tatizo la watanzania ambao wataki kilichopo wala kinachotaka kufanyika lakini wakati huo huo hawajui wanataka nini.
Tatizo limeanzia juu yaani serikali haiamini wenye vipaji.
Kuna watu wangefundishwa kutumia rasilimali zetu wangeweza kufanya maajabu.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Tatizo limeanzia juu yaani serikali haiamini wenye vipaji.
Kuna watu wangefundishwa kutumia rasilimali zetu wangeweza kufanya maajabu.
Kwa mantiki hiyo, unadhani Tanzania tunataka nini kutoka China? Au tunavyoitumia fursa ya uhusiano wetu na China inatosha?
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
"Tanzania haitaki nini kwa china sema china ndo inataka nini kwa Tanzania" ~kinyume chake ni sahihi
Dah! Wewe ukiwa na mchumba, halafu yeye anajua anataka ni ni kwako nalafu wewe hujui unataka nini kwake wala hutaki kujua, unatarajia huyo mchumba akufanyie ni ni? Na akikufanyia nini utalalamika kwa nini?

Anyway, nafikiri suala la kwamba hakuna tunachotaka purse' sio sahihi. Sualani kwamba tunatumia hiyo fursa chini ya kiwango, kwa hiyo ni vyema tukafikiria maeneo mengine zaidi ambayo tunaweza kutumia uhusiano huo kwa manufaa zaidi.
 

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,486
2,000
Dah! Wewe ukiwa na mchumba, halafu yeye anajua anataka ni ni kwako nalafu wewe hujui unataka nini kwake wala hutaki kujua, unatarajia huyo mchumba akufanyie ni ni? Na akikufanyia nini utalalamika kwa nini?

Anyway, nafikiri suala la kwamba hakuna tunachotaka purse' sio sahihi. Sualani kwamba tunatumia hiyo fursa chini ya kiwango, kwa hiyo ni vyema tukafikiria maeneo mengine zaidi ambayo tunaweza kutumia uhusiano huo kwa manufaa zaidi.
Uhusiano wetu na china kwetu unamanufaa kidogo, sema wao ndo wanafaidi hatari
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Uhusiano wetu na china kwetu unamanufaa kidogo, sema wao ndo wanafaidi hatari
Yeah, tunaenda vizuri sasa. Mjadala 'tufanyeje sasa ili tunufaike zaidi kulingana na mazingira yetu?' Ikumbukwe ishu sio kunufaika sawa maana hilo haliwezekani, ishu ni tunufaike zaidi kwa kadiri iwezekanavyo.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kudos, Azizi

Umetengeneza points valid sana.

Unfortunately, hate yangu kwa China ita cloud opinion yangu kwenye hili.

Wacha niangalie mjadala from the sidelines
Kwa nini unawachukia mkuu? Sema tu inawezekana mma una hoja ya msingi, au ni mtizamo tu ambao uko nini ya kichwa chako, ila kupitia mjadala huu, ukifunguka unaweza kupata picha mpya kabisa ambayo hukuwa nayo hapo kabla.
 

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,486
2,000
Yeah, tunaenda vizuri sasa. Mjadala 'tufanyeje sasa ili tunufaike zaidi kulingana na mazingira yetu?' Ikumbukwe ishu sio kunufaika sawa maana hilo haliwezekani, ishu ni tunufaike zaidi kwa kadiri iwezekanavyo.
Tanzania yetu ijizatiti katika kukuza elimu hasa elimu inayotumia rasilimali zetu yaani hapo watafute watalamu kutoka nchini wakapate mafunzo maalum
 

1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,206
2,000
Mwaka jana, kuna mtafiti mmoja kutoka kitengo cha utafiti wa utekelezaji wa sera za nje za China alituuliza ' hivi Africa inataka nini China?' Akiwa na maana waafrica tungetamani kunufaikaje na diplomasia ya kiuchumi kati ya nchi zetu na China ambayo kwa sasa Inaongoza kwa uchumi,teknolojia na upana wa soko duniani. Ukweli ni kwamba hatukuwa na jibu lililonyooka kwamba ni nini hasa tunataka....
Tuna hamu ya kubakwa...tunatamani kubakwa.....Yaani kubakwa kiuchumi...unalo swali jingine?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom