Ebu skia hii!!

Hance Mbuya

Member
Apr 11, 2012
45
12
Maisha ni mzunguko,katika hali inayoshangaza ni kuwa unaweza ukaamua jambo na baadae kushindwa kufanikisha au kutokulifanya kabisa.

Jambo lenyewe linaweza kuwa ni la urafiki kati ya mwanamke na mwanaume.Urafiki naouzungumzia hapa ni ule wa kimapenzi.Mwanzo wa urafiki huu huwa mzuri sana mpaka wakati mwingine unamuuliza,ulikuwa wapi siku zote?.Hufikia hatua ya kuwekeana ahadi kwamba nitakuoa,ww ndio chaguo langu la mwisho hakuna lingine.

Kiukweli maneno hayo hutoka moyoni kwa mwanaume,wakati mwingine mwanaume husema,''daah niliwahi kuwa na dem lakini huyu anawafunika woote niliowahi kuwa nao''bila kujua hata wale mwazo wao ulikuwa kama huu.

Yote hayo hufanyika mwanzo kabisa wa mahusiano,ikifika katikati ya mahusiano hapa kila mmoja kashamzoea mwenzake,zile sms zinapungua kama zilikuwa zitumwa kila asubuhi na jioni zitatumwa jioni tu,na kama alikuwa na mazoea ya kuja nyumbani mara kwa mara atakuja mara moja kwa wiki tena umuombe.Inapofika stage hii ndo dalili za kuachana zinakaribia.

Hatua inayofikia ni kuachana,mipango yote ya kuoana imeishia hapo na kila mtu anaangalia ustaarabu wake.Unaweza kujiuliza ni kwann haya hutokea lakini ukweli ni kwamba wanawake wana dharau sana baadhi yao,akiwa anasumbuliwa kila kukicha na wanaume wenye hali zaidi kuliko ww huwa wanaanza dharau na wakati mwingine wanakunyari kana kwamba unaweza kumuhudumia weye?

NB:Dharau si nzuri,heshima umepewa na Mungu hununui popote,tunza heshima yako ili uheshimiwe na wengine hata watoto usipowaheshimu nao hawatakuheshimu..

The end.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Vipi ndugu umeongea kwa uchunguuu,nani kakudharau mpaka umevunja ahadiii?pole mwaya
 
aisee, kwahiyo sababu ya mapenzi kuisha ni 'dharau za wanawake' eeh.
 
aisee, kwahiyo sababu ya mapenzi kuisha ni 'dharau za wanawake' eeh.
dharau za wanawake pale wanapokutana na mtu mwenye kuwazidi wapenzi wao hela.
He is very specific, naona kuna kitu kimemkaa rohoni amekosa pa kukitemea...
 
ni kweli unayosema ndugu lakini unajua kaika mahusiano jaribu kutengeneza mazingira ya kutozoeana ili ahadi zenu zitimie.

binti wa kuoa utamwona ata mwonekano wake, yupo simple, anafahamu maisha i mean hayupo after pesa sana.
tatizo ninyi manatongoza kwa kupitia vitu ka pesa, gari na mali nyingine hamtafuti mapenzi ya kweli ndiyo sababu ya kuchokana..
kumbuka pesa zinaisha au kupungua, gari linachoka, akija mwenye zuri zaidi nitafuata.

acheni kutongoza kwa kutumia vitu ili mpate mapenzi ya kweli,....
 
Hapo napo ni pakuzingatia!
 
dharau za wanawake pale wanapokutana na mtu mwenye kuwazidi wapenzi wao hela.
He is very specific, naona kuna kitu kimemkaa rohoni amekosa pa kukitemea...

nilimiss hiyo sababu. LOL
Mleta mada, pole sana; yaani sometimes sisi wanawake sijui tukoje tu. Ila usijali, waliosema akunyimaye kunde .......si wajinga. one day yes utapata mdada ambaye atakuona wewe hizo ulizonazo ni NYINGI.
 
Mrs lyimo nimekupata nitazingatia ulichosema,ila inauma hasa pale unamuwaza asie na mpango na ww!!daah
 
nilimiss hiyo sababu. LOL
Mleta mada, pole sana; yaani sometimes sisi wanawake sijui tukoje tu. Ila usijali, waliosema akunyimaye kunde .......si wajinga. one day yes utapata mdada ambaye atakuona wewe hizo ulizonazo ni NYINGI.

Poa ila inachukua muda kumpata kama yule!!
 
Kaka tumekusikia, na umetufikia Ujumbe! Cha msingi watu kubadili tabia sasa....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom