mxsdk
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 3,585
- 2,049
EBU LITAMBUE HILI NA ULIWEKE KICHWANI MWAKO (BABY NUMBER ONE).
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.
Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwa sababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.
Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.
Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.
Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini.
Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini? Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.
Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.
Na ukiona mwanamke wako hayupo angalau kidogo tu ya hayo niliyotaja hapo juu basi jikatae kwake mapemaaa, sio baadae nikiandika status kuhusu wanawake hapa unakuja kutoka povu ooh wanapenda pesa ooh wanapenda vitu vya gharama ooh sijui nini.
Hutakiwi kulalamika, wanawake wa aina hiyo unaowalalamikia ni wajasiriamwili na wewe sio level yao, ambao ni level yao hawaoni tabu kuhonga wanaweza kuhonga hata meli. Mariah Carey pete yake tu ya kidoleni aliyopewa na Mchumba wake bilionea wa Australia ni takribani Tsh Bilioni 15 za Kitanzania.
Kama umeona hapo sio level yako wewe jikatae mapema, huwezi pigana na ukuta mwisho wa siku utaumia wewe, mwache aendelee kuchimba bwawa kama ndio maisha aliyoyachagua.
Wanawake wenye upendo wa kweli wapo. Ukimpata jifanye kipofu kwa wengine wote, ila ona kwake tu! Kilicho kizuri kitunze kidumu.