Ebu leo tubadilishane uzoefu hapa..

son of king john2

Senior Member
Jan 11, 2014
131
33
Jamani ebu tukumbushane ugumu ambao huwa unakutana nao wakati wa kusubiria kitu fulani hasa vile vyenye matokeo ya aina mbili tu.Ntawapa uzoefu wangu niliowahi kukutana nao katika kusubiri!!!

1.wakati wa kusubiri matokeo yangu ya kidato cha nne ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu..hasa pale nilipoambiwa matokeo yametoka alafu sina uwezo wa kuyaona kwa wakati huo..Da naomba niishie hapo juu ya hilo maana ilikuwa ni hali mbaya ya ajabu ila nilipo yaona nilikuwa nimefaulu.

2.Wakati nasubiri matokeo baada kupima ukimwi ....weeee hapa jasho lilikuwa linalowanisha shati tena kwa kasi ya ajabu...yani nesi aliponiita kwenda kusikiliza majibu nilikuwa na hali mbaya balaa...

3.wakati mwingine mgumu ni pale nilipokuwa nasubiri kupata jibu la ndiyo au hapana kutoka kwa beby baada ya kuwa nimetuma maombi kwa zaidi ya miezi kadhaa bila kuwambiawa jibu la maana siku hiyo kanambia leo nataka kuongea na ww kuhusu ile inshu yako..Aisee ilikuwa siku ngumu ...hiyo ikapita siku beby kasema anakuja kuleta mchezo wa kwanza aisee ilikuwa siku ndefu maana alisema kama leo kwamba atakuja kesho jioni..weee kazi zilikuwa haziendi siku nzima..

4.kwa walioa kwa kufunga harusi naomba mnambie siku ya harusi ukiwa unasubiri ajitokeze mtu wa kupinga juu ya ndoa yenu ....haha haha najua jasho linakuwa la kutosha.

5...naomba na wewe unipe kitu ambacho kilikupa wakati mgumu kukisubiri.......
au kama nimekitaja basi sema ulikuwa unajisikiaje katika suala hilo
 
Back
Top Bottom