Ebu hii tuiweke sawa…tatizo kubwa la Tanzania ni MIFUMO au WATU?.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ebu hii tuiweke sawa…tatizo kubwa la Tanzania ni MIFUMO au WATU?..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Mar 14, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu zimezuka hoja nyingi humu jf kwamba hujadiliwa mno watu na matatizo yatokanayo na WATU…..mfano ufisadi etc…na kusahau hoja zinazohusu mifumo/sera……..

  My takes:
  • Mabadiliko ya kweli TZ yataanza na mabadiliko ya fikra za watu wa Tanzania…..hata mabadiliko na usimamizi wa mifumo/sera bora italetwa na watu waliobadilika TZ. …hata kama tukiwa na mifumo/sera nzuri (on paper)..kama watu wa TZ wasipobadilika itakuwa kazi bure …..maana wasimamizi wa mifumo/sera ni watu na wanaovuruga mifumo/sera nzuri ni watu..Kwa hiyo watu wanapoanza kuhoji utendaji mbovu wa watu nchi hii tusiwabeze…kwani naona ni dalili nzuri ya mabadiliko katika fikra za watu…to me. For a real change to happen in TZ, we need people to change first……jadili..

  • Tujadili tukifanya reference ya mifumo/sera iliyopo TZ sasa na jinsi inavyosimamiwa na watu….mfano: .mfumo wa katiba,..azimio la Zanzibar,..siasa ya ujamaa…mfumo wa kupambana na rushwa(takukuru)..mfumo wa elimu ya msingi/secondary..sera mpya ya madini..etc..etc…Bado naamini kuwa mifumo/sera nzuri zenye tija kwa taifa zitaletwa na kusimamiwa na watu wazuri….hata mfumo wa katiba mpya tunaotaka kuunda tayari pameshaonekana dalili za watu kutaka kuuvuruga kwa maslahi fulani…Huwezi kutibu tatizo bila kuondoa chanzo cha tatizo…matatizo ya watanzania yamesababishwa na watu wa TZ….jadili…

  • Pale ambapo watu wanachaguliwa/ kuteuliwa kwenye nafasi za kiutendaji /kisiasa kwa misingi ya rushwa,kujuana, undugu, ukabila, udini, etc etc ….katika ngazi mbalimbali TZ ..watawezaje kusimamia utekelezaji wa mifumo/sera zenye kuleta manufaa kwa wote??..watu lazima wabadilike……

  • Mwalimu Nyerere aliwahi kutuambia TZ kuwa..ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu,siasa safi na uongozi bora..Je watanzania ni watu wa namna gani???hili swali tunalijibuje leo??..hata siasa safi na uongozi bora vinahusisha watu…hata tukiwa na katiba nzuri,inabidi isimamiwe na watu….mifumo/sera nzuri inaweza kuwekwa na watu makini lakini ikasimamiwa na watu wabovu……..pia mifumo/sera mbovu inaweza kuwekwa kwa mashinikizo toka nje(kifisadi)ili kunufaisha watu wachache….jadili…

  • Mifumo/sera inaweza kuwa adopted(kuchukuliwa)kutoka nchi nyingine ilipotumika kwa mafanikio lakini utekelezaji wake hapa nchini utategemea utendaji wa watu wa TZ….na pia ipo mifano ya sera zilizotengenezwa TZ na kuwa adopted na implemented katika nchi nyingine kwa mafanikio makubwa wakati hapa TZ zimeonekana ku fail….mfano…nina taarifa (sijathibitisha)kuwa master plan ya mji wa Dodoma unaotakiwa kuwa mji mkuu wa TZ ndio iliyotumika kujenga mji wa Abuja(Nigeria)…..sasa hapa tatizo liko wapi TZ???

  • Napotafakari haya yooote….nafikia conclusion kuwa ..hakika TZ haitabadilika kama WATU wake hawatabadilika(kifikra)……..nakumbuka jamaa humu jf mwenye signature ya msingi sana ..NN..inayosema.."Miafrika ndivyo tuliyo"….mimi hapa naamua kuwa more specific kwa case ya TZ na kusema kuwa…"Mitanzania ndivyo tulivyo"..maana nchi nyingi sana za afrika zinaizidi TZ kimaendeleo...pamoja na potential tuliyonayo......God Bless!
   
Loading...