Ebola yatia fora Sierra Leone

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
141107105806_ebola_paciente_950x633_bbc_nocredit.jpg

Mgonjwa huyu aliwakimbia wahudumu wa afya.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa ripoti juu ya nchi ya Sierra Leone kuzipiku kitakwimu nchi za Afrika Magharibi hasa jirani zake Liberia ikiwa ni nchi yenye idadi kubwa ya watu walioathirika na ugonjwa huo.

Who inasema kwamba imeorodhesha watu wapatao elfu saba na mia nane walio na virusi vya ugonjwa wa Ebola,idadi ambayo inaizidi kidogo nchi ya Liberia,wakati nchi Guinea kuna wagonjwa wenye maambukizi wapatao elfu mbili.

Kitengo cha umoja wa mataifa kimeripoti juu ripoti za siku za hivi karibuni kwamba watu wapatao elfu sita miatatu na thelathini na moja wametambuliwa kafariki dunia kutokana na ugonjwa huo idadi hii inajumuisha nchi zote tatu za Afrika Magharibi.


Chanzo:BBC
 
Back
Top Bottom