Eazy View.....

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,744
Points
1,500

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,744 1,500
KAMPUNI ya Multi choice Africa inayojihusisha na huduma za utoaji wa huduma ya Chaneli za TV kwa malipo barani Afrika, jana ilizindua huduma mpya inayojulikana kama DStv Easy View, ambayo itamuwezesha mteja kupata huduma kwa gharama nafuu.

Akizungumza jana kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Multi choice Tanzania, Peter Fauel alisema kuwa huduma hiyo ambayo itamuwezesha mtumiaji kuona chaneli mbalimbali duniani, itamgharimu shilingi 36,000 kwa mwaka, ikiwa ni sawa na sh 3,000 kwa mwezi, jambo ambalo halijawahi kutokea hapa nchini na barani Afrika.

Alisema mteja atakayeingia katika DStv Easy View, atapata nafasi ya kuona chaneli mbalimbali zaidi ya 10, zikiwamo za watoto, michezo, filamu mbalimbali, muziki na habari.

Fauel alisema huduma hiyo imeanza kutolewa tangu Februari 14 ambako mteja atakayeingia katika huduma hiyo, ndani ya miezi mitatu tangu kuanza kwa huduma hiyo atapata nyongeza ya miezi mitatu.

Alisema kuwa pia mtumiaji wa Easy View ataweza kujiunga na chaneli za Premium, family na Compact ambazo nazo zitamuwezesha kuona huduma mbalimbali za vituo vya televisheni duniani.

Source: TZ Daima
 

DMussa

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
1,314
Points
1,225

DMussa

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
1,314 1,225
Mimi naona suala kubwa kwa DSTV ni gharama za kujiunga na sio ada ya kila mwezi. Je aliongelea kuhusu hili suala???

Currently nafikiri DSTV are still doing very well hapa bongo na kama tutapata easy view i'm sure hata hawa GTv watapata kazi kucompete.
Good start DSTV..2008
 

Forum statistics

Threads 1,364,302
Members 520,697
Posts 33,311,367
Top