EATV, "ndutu" ya Joyce Kiria Nkongo ni tusi badilisheni

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,323
6,810
Mtangazaji wa EATV mwanadada Joyce Kiria kuna maneno haya anayatumia kwenye kipindi chake cha sinema za ki-Tanzania.."indutu-nnyo" maneno haya yote mawili yanamaanisha kiungo cha uzazi cha mwanamke kwa baadhi ya makabila yetu hapa nchini.

Na kuna kila dalili mtangazaji huyu anajua maana ya maneno hayo kwani inasekana kuna watu mitaa ya Kinondoni walimwita Indutu!!!! alikasirika vibaya sana!! Huyu mtangazaji inasemekana pia ameishawahi kufungwa jela na ndiko alijifunzia tabia hii.

Sio ustaarabu bwana, hata kama eti kwa ki-lingala yana maana nyingine, si watafute jina lingine?? Kuna watu wanakimbia Lunninga zao wakisikia maneno hayo!
 
Mhhh!
Makabila mangapi yanatumia maneno hayo kama tusi?
EATV ina'cover eneo gani...EA FYI!
Any word can be an INSULT in some other tribe's language!
Tusiwe unnecessarily waoga mazee!
 
kwani analitumi kama tusi au analitumia mahala gani, mi sielewi. kama mtu anaweza kutaja au kuweka sentensi zenye neno mb** bila sababu za msingi....tena hewani.
 
Indutu ni dudu ya Mwanamke katika kabila la wanyakyusa, hilo la pili sijui.
Na impact yake ni kubwa kwa sababu kabila la wanyakyusa ni kubwa na wapo sehemu mbalimbali duniani. (Wabadilishe mara moja)
Isije mtu nimekaa na mama mkwe wangu sebuleni halafu mtu anatamka Indutu mbele yake, nitavunja TV
 
ipo dhana moja katika matusi na lugha.
ikithibitika mzungumzaji anajua kuwa neno analotamka lina tafsiri mbaya basi hayo ni matusi, ikidhihirika kuwa mzungumzaji hajui kama ni matusi, hakika hayo si matusi, ila anamaanisha kile anachomaanisha kwa wasikilizaji wake.
kwa mfano yupo mchezaji wa soka wa Timu ya Taifa ya Cameroon anaitwa EMANA, hilo neno kwa Kihaya ni tusi la sehemu za siri za kike.........ila kwa wazazi wa Emana hawakumaanisha sehemu nyeti za kike, hivyo litabaki kuwa jina sahihi na zuri hadi pale watakapo kuwa wanawasiliana katika lugha moja na mantiki moja na wahaya.
Lugha na mazingira, lugha na wazungumzaji wake.
 
Mhhh!
Makabila mangapi yanatumia maneno hayo kama tusi?
EATV ina'cover eneo gani...EA FYI!
Any word can be an INSULT in some other tribe's language!
Tusiwe unnecessarily waoga mazee!

Indutu - kinyakyusa
Nyo - kisukuma
Yote mawili yana maanisha kizalio cha mwanamke.
Tena yeye huwa ana sisitiza kabisa ..mfano; "kina dada msizitoe bure hizo indutu zenu, zipeni heshima yake". eti akimaanisha sinema zao!!!!!
 
Hata nnyo pia linamaanisha Uke kwa makabila mengi tu....Hivi(swali la kizushi) ni kwa nini inapotokea mtu kataja jina la kiungo cha uzazi cha mwanamke au mwanaume inaonekana ni tusi???,mbona tunapoonge kiingereza tunayataja kwa urahisi tu bila kujiuliza mara mbilimbili?,ni utamaduni ama?...Iifikie kipindi tubadilike sasa maana inakuwa ngumu hata kwa wazazi kuwapa watoto wao elimu ya uzazi i.e viungo vya uzazi na kazi zake(ambayo yaweza kuwasaidia kujikinga na magonjwa kama Ukimwi na yale mengine ya kujamiiana,pia kuepukana na Mimba zisizotarajiwa)
 
Kuna maneno soft mengi tu yanaweza kutumika kumaanisha maana ileile, ndiyo maana badala ya kutamka ******, kuna maneno kama Kujamiiana nk, yote ni katika kufanya vipindi viangaliwe na watu wa rika na jinsia tofauti bila kuleta usumbufu.
 
Ni kwa nini tusiyatumie maneno halisi tu badala ya kuzungukazungukaaa...Maana hakuna kipya hapa..ni unafiki????????????
 
Ni kweli, lakini hatujafikia hatua ya kuharibikiwa kiasi hicho, Heshima ni kitu cha bure tusiipoteze kwa sababu za utandawazi
 
Ni kwa nini tusiyatumie maneno halisi tu badala ya kuzungukazungukaaa...Maana hakuna kipya hapa..ni unafiki????????????

Mkuu vipi? inawezekana kweli hali hiyo?? maana hata wewe umeshindwa kuzitaja hizo sehemu waziwazi kwa lugha ya moja kwa moja!!
Mh, hapana bwana siyo hii jamii yetu.
Yule dada anajua anacho kimaanisha ndiyo maana hugeuka mbogo akiitwa Indutu-nyo, nini kinamkera?
 
lakini,huyu dada aliwahi kufafanua ya kwamba maana ya maneno hayo ni kisigino kwa lugha ya kimasai.Kilichopo hapa ni kuwa tolerant na wala si vinginevyo
 
Mkuu vipi? inawezekana kweli hali hiyo?? maana hata wewe umeshindwa kuzitaja hizo sehemu waziwazi kwa lugha ya moja kwa moja!!
Mh, hapana bwana siyo hii jamii yetu.
Yule dada anajua anacho kimaanisha ndiyo maana hugeuka mbogo akiitwa Indutu-nyo, nini kinamkera?

Si kwamba nimeshindwa kuzitaja nina weza kuzitaja,tatizo ni kwamba hairuhusiwi hapa jamvini(JF) so nikizitaja nitakuwa navunja sheria kwa makusudi ilhali nazijua...Ninachojiuliza ni kwa nini inakuwa vigumu kuvitaja viungo hivi(kwa kiswahili) wakati kwa kiingerza tunavitamka waziwazi bila hata ya kuumauma maneno?,utakuta mtu akimsikia mwenzie katamka k... ama m... anamwambia katukana baadae utamsikia mtu huyo huyo anayemwambia mwenzie katukana anavitaja viungo hivyo kwa kiingereza kwa uwazi kabisa bila kujiumauma
 
Mkuu umenena, sasa kama hapa JF ambapo tuna-dare ku-talk openly inakuwa ngumu kuzitaja itwezekanaje kwenye jamii zetu zenye maadili kibao!?
La pili, ya Waingereza niyao na ya Waswahili ni yetu.......mie naamini kama kingereza kingekuwa lugha ya taifa kama kilivyo kiswahili bado viungo hivi visingetamkika kirahisi katika jamii zetu.
 
Heheeeeeeeeeee,haya bana..Pa1
 
Ni kwa nini tusiyatumie maneno halisi tu badala ya kuzungukazungukaaa...Maana hakuna kipya hapa..ni unafiki????????????
Mkuu ukitumia lugha yako ya kwanza kutamka neno lolote uzito unakua mkubwa zaidi....inawezekana ni kwa sababu tumekua katika malezi ya kwamba ni vibaya kutamka maneno hayo hadharani, na hii ni tangu unazaliwa.
Haya ya kiingereza ama kitaliano tumeyajua ukubwani, kipindi cha yale malezi kishapita.
Ni rahisi kwako kutamka tusi kwa kinyakyusa kuliko kutamka kisukuma (kama wewe ni msukuma)
 
Nimekusoma kiongozi,lile lilikuwa ni swali la kizushi tu...Pa1
 
Huyu dada anatukana kwa makusudi kabisa.

Mie hapa nafikiri anaongea Kinyamwezi/Kisukuma kabila ambalo ni robo ya asilimia 15 ya Tanzania. Kinyamwezi, Indoto maana yake Mbichi na mengine wameshaeleza wengine.

Ila kusema ukweli hili lilishajadiliwa sana nikiwa Tanzanet. Tukaambiwa hadi kampuni kama Ford hutumia kama laki 3 kwa mwaka kufanya utafiti kama hilo jina la gari halina maana mbaya sehemu fulani duniani.

Kwa mfano neno SOKO au MASOKO, kwa Kilingala ni Makalio. Neno Kona kwa Kireno ni hilo neno anasema huyo mdada. Kuna siku niliona restaurant imeandikwa Mavi, sikutaka hata kuingia ndani....... Ni ngumu sana kuzuia ila ni vema akafahamu kuwa hili neno litakuwa linaleta kizaazaa kama Video clip ya Rose Mhando ya Nibebe....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom